Hamu imepungua CCM: wanukuliwa kusema hawataki tena kugombea urais

UWEZO_WAKO

Member
Nov 17, 2010
39
4
HAMU URAIS.png

Utafiti wa awali unaonyesha ugomvi wa kugombea urais ndani ya ccm umepungua na utazidi kupungua hasa wanachama na viongozi wengi wanapozidi kuhamia cdm. mmoja wa wa makada wa ccm waliohojiwa alinukuliwa na utafiti huu wa kujitegemea akisema...sasa wewe unaniuliza nini wewe huna macho ya kuona..sasa utatamani kugombea urais wakati wapiga kura wanahamia upinzani. Lakini pia kuna mkakati wa kuifaulisha ccm katika chama kingine ambacho kwa kifupi kinaitwa CHM...Hata hivyo utabiri wa utafiti huu umeonyesha chama hicho itakichukua miaka mingi kupata ukubali wa wanachi hasa wakati ambapo CDM watakapoanza kuvurunda.
 
Attachments

  • HAMU_URAIS.bmp
    1.7 MB · Views: 103
Magamba hawaamini mpaka sasa kuwa wame poromoka. Msikieni Nape na Chiligati wanavyo ongea kana kwamba wako kwenye mioyo ya watu. Wamekuwa kama Thomaso wa kwenye Biblia aliye sema kuwa haamini Yesu amefufuka mpaka aguse kwenye viganja vyake. Na wao hawaamini kama watu wana hama. Sasa hawa magamba wanaona kama mzaha vile mpaka yatakapo wakuta. Au matunguli na mipete wanayovaa ndiyo inawapa matumaini?
 
Mkuu nimecheka sana has pale kwenye kuifaulisha, hongera kwa ubunifu huu lakini ndiyo ukweli ambao hawanabudi kuukubali na kuachia liende!
 
Magamba hawaamini mpaka sasa kuwa wame poromoka. Msikieni Nape na Chiligati wanavyo ongea kana kwamba wako kwenye mioyo ya watu. Wamekuwa kama Thomaso wa kwenye Biblia aliye sema kuwa haamini Yesu amefufuka mpaka aguse kwenye viganja vyake. Na wao hawaamini kama watu wana hama. Sasa hawa magamba wanaona kama mzaha vile mpaka yatakapo wakuta. Au matunguli na mipete wanayovaa ndiyo inawapa matumaini?

Tabia za madikteta ni kupiga kelele hata kama dunia nzima inajua umezingirwa na hutapona. Tuliona hili kwa Sadam, Gaddafi, Osama na wengine unaoweza kuwataja.
 
Satanic_Verses nimeipenda hiyo kwenye red, lakini sidhani kama Nape na Chiligati ni Madikteta labda jina jingine lenye kupungua kidogo makali.
Tabia za madikteta ni kupiga kelele hata kama dunia nzima inajua umezingirwa na hutapona. Tuliona hili kwa Sadam, Gaddafi, Osama na wengine unaoweza kuwataja.
 
Chadema daima kitakuwepo,misingi na sera zake zitadumu karne 1000.siyo magamba miaka 50 choka zaidi ya mbaya.
 
Back
Top Bottom