Hamu hakuna | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamu hakuna

Discussion in 'JF Doctor' started by Kafuta, Mar 9, 2012.

 1. K

  Kafuta Senior Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wandugu kupitia jukwaa hili naomba kuuliza kama hii hali inayojitokeza kwangu ni tatizo au la.. Mm ni mwanamme umr miaka 31 ni kwamba nimekua na takriban miez miwil na zaid bila kua na hamu hata kidogo ya tendo la ndoa..yaan mzuka zero..doro mtalimbo..cjaenda spital bado..nimeanza na jf kwanza..naomba kujua chochote kutoka kwenu.
   
 2. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Inaweza kuwa psychological
  Una stress? depression?
  Una relationship problem?
  Kuna ishu inakupunguzia kujiamini?

  Inaweza ikawa hormonal.
  Labda hormonal imbalance

  Inaweza ikawa side effect ya madawa
  Kama kuna madawa unatumia jaribu kuangalia kama hayana side effect ya hii kitu.

  Maradhi.
  Kuna maradhi yanaeffect somehow libido ya mtu e.g kisukari, BP e.t.c.


  N:B nina F ya biology form 4, usiniamini kiviiiiiiile. Tumsubirie Dr Ndokeji kwa ufafanuzi zaidi. Dr Riwa inaonekana yupo kwenye mgomo
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kwa Matatizo yako Kutojisikia hamu nakushauri tumia Asali kila siku kunywa asali kabla ya kula kitu kutwa mara tatu kwa muda wa mwezi mmoja jaribu kisha utanipa Feedback.

  Licha ya sifa yake ya kuwa na utamu wa asili usio na madhara hata kwa wagonjwa wa kisukari, asali pia ni tiba ya magonjwa mengi, pia ni kinga ya maradhi yanayosababishwa na bakteria, fangasi na mengine mengi. Asali mbichi ndiyo bora zaidi kuliko iliyopikwa.

  Kwa ujumla asali ina faida nyingi katika mwili wa binadamu, kwani ni chanzo kikubwa cha vitamini na madini. Inaelezwa kuwa asali ni chanzo kizuri cha vitamin B2, B6, madini ya chuma na manganizi (manganese). Anza sasa mazoe ya kula asali, ila hakikisha una pata asali halisi, siyo feki.

  KIJIKO KIMOJA CH ASALI KINGA YA SIKU NZIMA
  Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, asali ina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya vidudu nyemelezi ambavyo husababisha magonjwa mbalimbali mwilini pale mwili unapokuwa hauna kinga. Hivyo kijiko kimoja cha chakula cha asali kikitumiwa kila siku huwa kinga tosha (antioxidants).

  Tumia Asali Mbichi Safi ambayo haija pikwa itakusaidia matatizo yako nakushauri mimi MziziMkavu.
   
 4. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  miezi miwili tu ? Mbona kidogo sana je ss wenye kama 7 yrs tusemeje??.

  Kwani usipo du unakufa au kuna kitu kimepungua mwilin mwako??.
  Umeoa au unampenzi au ndiyo wale wale wazee wa kona bar??
   
 5. M

  Marukangasi Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 13, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza jaribu kubadilisha chakula unachokula,vipo vyakula vinavyoaminika kuongeza nguvu za kiume(aphrodisiac food) ulaji wa chakula cha Karanga haswa wakati wa usiku,matumizi ya Karanga kumeonekana kumsaidia mlaji kuongeza nguvu za kiume,kula samaki kwa wingi especial of see food,punguza kula nyama haswa viungo vya ndani Kama maini,utumbo,figo,ulimi nk kwani huwa na kiasi kikubwa cha rehemu (cholesterol ) ongeza kula matunda kama embe mafuta(avocado )tikiti maji( water Mellon) nyanya,ndizi.usiende kujamiana wakati umeshiba kwani inapunguza mzunguko wa damu kwenye sehemu za Siri,damu nyingi hubakia tumboni kwahali hiyo inafanya uume usipate damu ya kutosha na kusababisha udhaifu wa utendaji kazi wake,basi chakula ikishindikana tutakwenda kwenye hatua nyingine:lock1:
   
 6. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  mkuu pole sana wanaume sikuhizi matatizo kama hayo yanatupata.
  ni kweli litakuwa ni tatizo kwani kwa biologia ya kawaida inasema ndani ya muda wa siku 30 mwanaume mara nyingi lazima ejaculate either 1)kwa kulala na mwanamke
  2) kupitia ndoto
  3)punyeto(masturbation)
  kutokuwa na hamu ya kufanya mapenzi mara nyingi ni huwa nitatizo linalosababiswa na matatizo ya kisaijologia na kibiologia .
  kisaikologia kama
  .DEPRESION
  .WASIWASI
  .HOFU
  mara nyingi tatizo la kutokuwa na hamu ya mapenzi huwa ni kwasababu ya upungufu wa homoni ya testosteron ,ni homoni inayofanya mwanaume kuwa na hamu ya mapenzi na kazi zingine kama kuzalisha mbegu za kiume.upungufu wa homoni hii hufanya kukosekana kwa uchochezi wa hamu kwenye ubongo na kusababisha nerva za uume wa mwanaume kushindwa kutoa nitric oxide kwa ajili ya kutanua mishipa ya damu kuruhusu damu ipite na kujazana kwenye uume ,kwa hiyo sasa inapotokea hali kama hiyo hufanya hata uume kushindwa kusimama .kwa upande mwingine upungufu huu mara nyingi hutokana na
  1)unywaji wa pombe mara kwa mara
  2)unene
  3)magonjwa kama .kisukari,cancer, magonjwa ya moyo,HIV reference klorockwine
  4)madawa ya kulevya kama bange,cocaine
  5)kutofanya mazoezi
  6)upungufu wa virutubisho kama vitamini B Kutokana na lishe duni
  7)lishe duni
  mara nyingine hali hiyo husababishwa na kufanya punyeto kupita kiasi

  TIBA
  JITAIDI KULA CHAKULA KIFUATACHO ILI KUONGEZA HOMONI YA TESTOSTERONI
  1)PARACHICHI(AVACADO) KILA SIKU MARA TATU KWA SIKU
  2)NDIZI
  3)CHOCOLATE
  4)TIKITI MAJI
  5)MAYAI
  6)ASALI NA MDALASINI
  7)SUPPREMENT KAMA CHRYSIN SUPPREMENT, NA L-ARGININE SUPPREMENT NENDA SUPERMAKET AU PHARMACY KUBWA UTAPATA

  DAWA
  1)VIAGRA
  2)CIALIS (TADALAFIL)
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kula matunda yasiyokuwa na ukakasi na hasa yale yenye umbo la yeti za kiume au pumbu za kiume kama ndizi, parachichi, matikiti maji, papai , juisi ya karoti n.k.

  Punguza kula matunda yenye ukakasi kama maembe, mananasi, malimao, machungwa, machenza, nk.
   
 8. Maayo

  Maayo JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 319
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapa mh...!
   
 9. mtoto mpole

  mtoto mpole JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 679
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  pia juice ya maziwa fresh ukichanganya na tende..yaan unatoa kokwa zilizopo kwa tende then unablend tende pamoja na maziwa na kunya glass moja kila asubuhi mda wa siku saba...tiba tosha pia epuka kua na msongo wa mawazo na kufanya kazi na mazoezi kupita kiasi.....Godbless u
   
 10. Avatar mok

  Avatar mok JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 3,199
  Likes Received: 2,696
  Trophy Points: 280
  Chemsha majan ya mchongoma na unywe kila siku asubui na kabla ya kulala.. Matokeo utayaona bada ya wik2 so nice dose
   
 11. O

  Obinna Senior Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ushauri mzuri, kumbe kuna pu***bu za kike??
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Samahani kama ni dada, jibu langu ni kwa muuliza swali
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280

  Kuamsha tamaa ya kiume au ya kike


  Tumia Juisi ya Tangawizi nusu kijiko pamoja na yai la kuku wa kienyeji nusu iliochemshwa na Asali Safi mbichi. Tumia kila siku kwa muda wa mwezi mmoja.
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Mar 15, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Mchongoma....!!
  Tusijelishana sumu jamani...
   
Loading...