Hamissa Mobetto: Natongozwa na wanaume wa nje zaidi kuliko wa kibongo

Nesi mkunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2022
701
1,840
Usiku wa Julai 15, Msanii Barnaba alifanya sherehe ya kusherehekea ndoa ambayo aliifunga na mpenzi wake wa muda mrefu Raya, ambapo shughuli hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo wasanii na Mastaa kadhaa. Miongoni mwa wasanii ambao walihudhulia katika sherehe hiyo ni pamoja na Hamissa Mobetto ambaye hivi karibuni ameamua kumuanika mpenzi wake hadharani baada ya kumficha kwa muda mrefu.

Alipoulizwa na Wanahabari jinsi alivyompata mpenzi wake huyo, Hamissa amefunguka kuwa, kwanza huyo ni Mwanaume wake wa kwanza ambaye anamu-enjoy kuliko Mwanaume yoyote ambaye amewahi kuwa naye huko nyuma, ni Mwanaume mwenye mapenzi ya dhati, anajua kuhudumia na wanaongea lugha moja ya mapenzi.

Amesema siyo mara yake ya kwanza kuwa kwenye mahusiano na mwanaume ambaye siyo Mtanzania na hii inatokana na kwamba anatongozwa sana na wanaume wa nje kuliko wa Kibongo ndiyo maana anajikuta ameangukia huko. Pia Mobetto ameongeza kuwa yeye na Mpenzi wake hawajaanza leo wala jana, ni wakongwe kwenye mahusiano hayo ila tu walikuwa hawajaamua kuweka mambo hadharani kwasababu haamini sana katika mahusiano ya mitandaoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom