Kwa ufupi bongo star seach haina majaji, pamoja na kuwepo wote kulipaswa kuwe na mtaalamu wa mziki ambae hajaji tu kwa sikio bali kwa utaalamu. Master J ni producer sawa lakini si mtaalamu wa muziki.
Kuna makosa mengi ya kiufundi wanafanya, na majaji wanayajua ila wanashindwa kuyaeleza kitaalam. Rejea show ya wiki iliopita december 3 kama sikosei. Kuna mshiriki aliimba, J dee aka sense kuna tatizo sehemu flani, akaishia kusema una sauti lakin kuna kitu sijui nini labda Master J anisaidie.
Master J akaishia blah blah, Dully nae aka comment nashindwa kuelewa sijui mikia[emoji3][emoji3][emoji1787], na hili neno mikia ndio linaniua zaidi, ya pigo kuwa kamili ndio mikia. [emoji1787][emoji1787] sasa kama jaji anashindwa jua tatizo hasa la muimbaji kisauti ana jaji nini?
Kuna mshiriki anaitwa fatuma katika show hiyohiyo ya jumapili, alianza na ufunguo wa chini wimbo wa Nandy, na akawa anaenda off key kila akitaka kupanda. Ila majaji wanaishia tu kusema bado kuna tatizo sehemu.
All in all mwalimu wao wa sauti anapaswa kuongeza juhudi maana karibu waimbaji wote wanakosa voice control, hasa wanapotaka kuhit high notes. Tatizo hili hadi yule muimba na gitaa mwenye vocal nzuri.