Wasalaam wanajamii!
Toka mwaka huu uanze na hasa hasa kuanzia tarehe 19 mwezi januari baada ya kutoka kwa ile barua ilokuwa ikiwaelekeza wakuu wa mikoa kupitia wakurugenzi na maafisa elimu kupungunza walimu wa sanaa na kuwahamishia shule za msingi zilizopo karibu; zoezi lililopangwa kukamilika tarehe 15 mwezi wa pili yaani Alhamisi wiki hii. Walimu walowengi hasa wa masomo ya sanaa wamekuwa tumbo joto na baadhi yao hapa nchini kwenye mikoa mbalimbali wameshapewa barua za uhamisho zikionesha shule ya msingi ya karibu anayohamia.
Mpaka sasa hali imekuwa sintofahamu kwa shule za sekondari za mijini na majiji. Kwani mpaka sasa miji na majiji mengi walimu wa sanaa katika shule mbali mbali hawajapewa bado barua. Na hata hili swala la uhamisho imesakuwa kama zilipendwa! Hakuna kinachoendelea! Ukimya mkubwa umetanda sana.
Ukimya huu unasadikika kuwa maafisa elimu wameshindwa wafanyeje kubalance hii IKAMA maana wamegundua kuwa hata huko shule za msingi walimu wamejaa mno mpaka basi. Walimu shule za msingi katika miji na majiji hapa nchini ni wengi hata kuliko masekondari! The equation can't be balanced!!!
Kinacho wakwamisha wakui wamikoa ; maafisa elimu na wakurugenzi wengi wa sehemu ambapo uhamisho huo haujaanza ni kitu kimoja tu; wanajiuliza, je wawapeleke walimu hao wa sanaa shule za msingi kulikojaa pia ili kubalance IKAMA sekondari?
Je wasolve tatizo la wingi wa walimu sekondari na wapeleke mafuliko ya walimu shule ya msingi? Mpaka hapo kweli hawana cha kufanya. Vikao vinakalika ila no solution!
Wepesi ungejuwa kwao kama barua ile ingewataka kuwahamisha walimu hao wa sanaa walozidi masekondali mahali popote ndani ya wilaya au mkoa bila kujali ukaribu ;hapo mambo yangeenda. Ila mpaka sasa ngoma imedunda!
Mikoa mingi walimu wamejaa sana si shule za msingi na hata sekondari. Kote ngoma ni draw!
Vijijini na sehemu za ndani ndani ndo walimu ni shida wawe wa sanaa wenyewe na hata wa science! Shule nyingi hazina walimu wa Geography na kiingereza. Hata walimu hao wa kiswahili na History ni haba sana huko vijijini.
Serikali ingeondoa kigezo cha kuhamisha walimu wa sanaa kwenda kwenye shule za karibu na ya sekondari wanayohamishwa. Yaani kigezo cha uhamisho wa ndani ya kata kingetenguliwa kwani mpaka sasa ni shule za mjini na majiji chache ambazo wakuu wa mikoa wamefanikisha mpango huu.
Kwa mfano katika manispaa ya Moshi ( kwa wachaga ) kuna shule za sekondari takribani 14 na hizo zote walimu wamejaa mpaka basi. Sasa kuna taarifa ya chini chini kuwa walimu wanaohitajika primary wako 6 tu! Je hao wengine wa sanaa walorundikana masekondari watapelekwa wapi?
My take!
Serikali itenge fungu la uhamisho kwa walimu hao wa sanaa na iwasambaze mahali panapokuwa na uhitaji!
Mijini; Manispaa na Majiji walimu wamejaa kote si primary au sekondari.Basi Serikali iwahamishe walimu wa sanaa katika shule za msingi na sekondari zilizopo vijijini na maeneo ya ndani ndani ndani ya wilaya; mkoa au ikibidi hata nje ya wilaya; mkoa au jiji.