Hamis Kigwangalla amjibu Bashe kuhusu CCM kujifunza kwa Zambia

Naam wewe acha kuimba kwaya hapa na kupiga vinanda kama Dr wako wa Vinanda Padri Slaa,hata hiyo CHADEMA nayo ijifunze,Mh Satta amewajumuisha Mawaziri toka nje ya chama chake nyie CHAMA CHA MADEM,hata kwenye serikali kivuli mnapigana vikumbo ninyi kwa ninyi,acha kuzijumuisha kambi zengine za upinzani,na muda si mrefu km mlivyokuwa mnaota kwa Padri Slaa bado na mkakaribia kufa kwa aibu na huyo Padri akaugua ukichaa naona kila kitambo anapayuka tu.

Haujaeleweka kabisa sijui ulitaka kusemaje?hebu kajipange tena ili watu waje wakuelewe unachomaanisha.
 
Huyu Kigwa hajitambui,
Hakumbuki hata alichokiongea jana yake. Nakumbuka aliitisha maandamano ya kupinga uwekezaji wa mgodi flani hivi huko Nzega. Alipokuja bungeni Chadema waalipoiponda hotuba ya budget ya Nishati na madini yeye akaibuka na kuwaponda chadema kwamba wanapinga bure hali ya kwamba madini yanasaidia sana pato la taifa. Nakumbuka Lissu ama Mbowe wakamkumbusha yale maandamano yake, wakaamuliza alikuwa analalamikia nini? Akawa hana la kusema. Then akaibuka na speech yake juu ya ardhi yote imeuzwa, na mambo meengi!
Hakumbuki hata huo ubunge wenyewe ni wakupewa. Mwisho wa dhurma ni aibu.
Dhurma ya ccm ndio inayoleta aibu yao leo hii!
 
Maoni ya Bashe
Bashe aipasha CCM
MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Hussein Bashe, ameonya kuwa iwapo CCM hakitajadili matatizo ya wananchi sasa, kitarajie kupoteza dola mwaka 2015, kama ilivyotokea kwa chama tawala Zambia

Majibu ya Hamisi Kigwangalla
"CCM itashinda 2015 bila kufuata ushauri wa Hussein Bashe wala watu wa aina yake. Hiki ni chama cha siasa na kina mifumo ya kufuata katika utendaji wa kazi zake kama kuna kada anataka kutoa ushauri kwa chama afuate mfumo uliopo vinginevyo tutajua anatafuta umaarufu wake binafsi kama alivyofanya ndugu yangu Hussein Bashe. Kwanza sioni kama ana 'moral authority' yakutoa ushauri alioutoa na chama kikafuata, maana yeye mwenyewe ana kundi lake tayari...sema bahati mbaya sana ni kwamba kwa sasa kundi lake limebanwa mbavu na chama na wao sasa wanapaparika hawajui itakuwaje kama kweli maazimio yaliyopitishwa na NEC yatafanyiwa kazi! Mimi nashindwa kuelewa ilikuwaje wenzetu hawa wakazubaa kwenye vikao halali (ambavyo wao ni wanachama) mpaka yakapitishwa maazimio mazito namna hii kwa kweli! Hivi ni kweli CC na NEC nzima hazina 'watu wao?

Maoni yangu:
Mh Kigwa naona Bashe anamnyima usingizi sana, kila maoni anayotoa Bashe lazima yeye ayajibu kwa kumpinga, Kigwa chapa kazi wananchi hawatakuhukumu kwa kumjibu Bashe bali kwa jinsi ulivyowatumikia wana Nzega. Hata hivyo wewe sio msemaji wa CCM wa ngazi yoyote ile, hivi viherehere vya nini?

Kigwa hasomi nyakati ama na kiburi..................................................nadhani yeye ndo anatafuta umaarufu
 
imefikia sasa chama cha magamba they dont trust each pengine kwa personal interest ila wanashindwa kufahamu nn hasa kero za watanzania au pengine wanajua but wanakuwa vichwa ngumu.
tanzanians, we must fight to overcome any trouble no matter how bigger it is but only when we come together!
peopleeeeeee.......!
 
Bashe na Kigwa ni Simba na Yanga za Igunga walisoma wote Primary school na Kigwa akapata chance ya kwenda Sec kwa kutumia jina la mtu mwingine wanajuna hawa wote ni mavuvuzela 2015 CDM wanachukua jimbo wao wanapiga kelele tu
 
We Dr Kigwa tunajua kilichokutoa Wizara ya Afya ndiyo maana ukajificha ndani ya CCM. Jaribu leo kusema ukweli ndani au nje ya ccm utaona jinsi utakavyofuatiliwa yale RDT za Malaria feki uliyoingiza nchini na ukala pesa. Ndiyo maana uliamua kwenda kujificha humo ccm. Mwezako Bashe amsema ukweli unaendana na wakati. Sasa si wakati wa kupiga propaganda kwa vijana.
 
Dr. HK Kigwangalla [MP] on Igunga: Media zimetuonea sana! CCM tutatumia wingi wetu bungeni kuubana Uhuru wa Media, hauna maana!

Huyu jamaa amedhihirisha kuwa IQ yake kwenye siasa na haki za binadamu haijakaa vizuri. Uwingi wa CCM bungeni haimaanishi kuwa wana dhamana hata ya kuamua kuwa watanzania tuwe Ng'ombe na tukawa. Amuulize Mapuri amwambie kuwa Media ni nini hasa?, na je ukitangaza vita na media mshindi anakuwa nani?. Hii ni vita ya wazi kwa Media ambayo CCM imeitangaza kupitia kwa Kigwangalla.
 
huyo mwenye jina la kununua atajibu sana hoja za watu wenye mitazamo chanya. Yeye yupoyupo tu hana cha msingi cha kuongelea na kikawaingia akilini watu.
 
Hbr zenu wana jf, me na hoja moja kuhusu huyu dr kigwangala, dr huna msaada wowote kwenye jimbo letu la nzega, kwanza umekua unapingana na hoja nzuri tena zenye mantini nzur na nchi yetu kisa zimekua zinatolewa na wapinzani, huna maana yoyote, nakwambia kaa ujipange uweke na hela za kuanzisha biashara cause 2015 huchomoki, bora tumrudishe BASHE wetu kipenzi cha wengi.
 
Mwanzoni hamkujua?
Kuweni wapole, kwakuwa unapoamua kitu uwe tayari kuyapokea matokeo ya maamuzi yako.
 
Usilolijua ni kama ucku wa giza ndg yangu, huyu jamaa kabakia kuvaa mi pete yake ya silver hana maana yoyote, kwanza 2015 ccm haitachomoka hata kwa mitutu ya bunduki, hili jimbo bora tuwape cdm wenye miono ya mbali.
 
Hbr zenu wana jf, me na hoja moja kuhusu huyu dr kigwangala, dr huna msaada wowote kwenye jimbo letu la nzega, kwanza umekua unapingana na hoja nzuri tena zenye mantini nzur na nchi yetu kisa zimekua zinatolewa na wapinzani, huna maana yoyote, nakwambia kaa ujipange uweke na hela za kuanzisha biashara cause 2015 huchomoki, bora tumrudishe BASHE wetu kipenzi cha wengi.
nihakikishie kweli kama wewe ni mwana nzega.
Unapajua vipi Mwanzoli ?
baada ya kunijibu hilo swali ndio ntaendelea na wewe.
 
Hamna mpya nyie watu wa NZEGA, hata mkiwekewa jiwe na CCM mtachagua, inabidi muwe wapole tu!!!
 
Sijawahi elewa Hamis Kigwangala ni mwanasiasa mwenye msimamo wa aina gani ndani ya CCM. Huwa simwelewi,maana haeleweki. Anafanya siasa za majungu na unafiki. Heri ya Bashe ameweka msimamo wake wazi ni wapi anasimamia. Inaonyesha kugaragazwa vibaya katika kura za mchujo za CCM kumemwacha Kigwangala na uwoga na kutojiamini.
 
Nampenda Bashe ana msimamo na ni mtu wa wazi anasema kinachomkera hakai nacho,pia naona huko mbeleni atakuwa mwanasiasa mzuri sana,tatizo chama alichomo kinamuona kama gamba, hivyo hatapewa nafasi ya kutanuka kisiasa labda afanye maamuzi magumu ya kukiama chama. Huyo Kigwa sio mwanasiasa saizi ya Bashe, hamuwezi kabisa na kama anataka kujimaliza kisiasa aendeleze bifu na Bashe.

Ushauri kwa Bashe:

Usijibizane na Kingwa, mpuuzie ulinde heshima yako.
 
Ahsante sana Kaka kwa tusi lako...
Kwenye CCM kuna ma conservatives hawa ni wale wasiopenda mabadiliko. Wao tayari ni spent force wanajolondia status quo zao.

Pia kuna reformist hawa ndio vijana wa kileo type ya akina Bashe, Nape etc ambao ni wakereketwa wa kweli wanaokiona kitisho kinachokikabili chama chao hivyo wanataka mabadiliko ya kweli.

Kundi jingine kubwa ni CCM maslahi, hawa wako kimaslahi zaidi wengine kwa lengo la kulinda himaya zao, wengine ni ma oportunists na ma gold digger humo humo. Hawa utawatambia kwa kimbelembele na kujipendekeza kwingi lakini hawana lolote na wala hawakitakii mema chama chao. Kina Mhe. Bagaile ni mmoja wa kundi hili akiamini CCM itatawala milele!. Hawa ni kuwapa pole tuu na kuisubiri siku ya siku!. Wanaofikiri kwa kutumia ....sio wabunge CCM wa Dar peke yao, na wengine wengi tuu wapo na Mhe. Bagaile ni mmoja wao!.
 
Back
Top Bottom