Hamduni
Senior Member
- Apr 25, 2020
- 170
- 117
MIKUTANO YA HADHARA NI FURSA KWA VIJANA WA CCM KUTENGENEZA AJENDA
Na Victoria Charles Mwanziva: Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa
Demokrasia ni mchakato ambao hutoa mwangaza wa namna ya uendeshaji wa mambo katika nchi kuendana na matakwa ya Wananchi kisiasa, kiuchumi, kijamii na kwa kufuata Mila na Desturi za nchi husika, pamoja na ushirikishwaji wa wananchi. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonyesha nia na dhamira yake ya kuihuisha Demokrasia yetu katika njia ya Maridhiano. Sisi vijana wa Chama cha Mapinduzi inatupasa kuunga mkono juhudi hizi kwa ukamilifu mkubwa.
Nichukua fursa hii Kuwapongeza sana Rais wa Jamahuri ya Muungano Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuwahudumia watanzania na Utekelezaji Mkubwa wa Ilani ya Uchaguzi 2020-2025. Lakini Pia Kipekee niwapongeze sana Mwenyekiti wa Jumuiya yetu ya Umoja wa Vijana wa CCM Komradi Mohamed Kawaida, Makamu Mwenyekiti Komradi Rehema Omari na Katibu Mkuu wetu Komradi Kenani Kihongosi kwa namna wanavyochapa kazi na kuendelea kuwa Daraja kwa vijana na kutusemea changamoto zetu vijana kwenye mamlaka mbalimbali.
Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi ipo katika hatua mbalimbali za kutanua wigo wa ushirikishwaji wa wananchi kwa kuzingatia mazingira yetu, huku tukiongozwa na moyo wa maridhiano yaliyoasisiwa na Rais Dkt. Samia yanayotujengea usawa, mshikamano na umoja kama Taifa huru lililojengwa katika misingi ya Demokrasia. Rais Dkt Samia hivi Karibuni katika kutekeleza Adhma ya Maridhiano aliyoyaanzisha ili kuvipa vyama vya siasa kutimiza haki zao za kikatiba ameruhusu mikutano ya hadhara. Chama cha Mapinduzi ni miongoni mwao vyama hivyo vya siasa ambavyo vimeruhusiwa kufanya mikutano ya hadhara jambo ambalo ni la kawaida kwa CCM.
Dhamira ya Rais Samia ni kujenga Tanzania katika misingi ya Demokrasia usawa na kuheshimu haki za binadamu akiamini huu ndio msingi wa utawala bora, Rais Samia wakati anazungumza na wanasheria katika Jukwaa la Wanasheria wa Jumuiya ya Afrika mashariki alisema: "Sisi hapa Tanzania tumeamua kuizingatia misingi ya haki na nataka niwahakikishie kwamba tutajitahidi kuijenga Tanzania yenye Haki, Demokrasia, Usawa na Mafanikio. Na ndio maana katika kipindi hiki tumekuja na idea ya zile 4R's, Nataka nisisitize kwamba kutenda haki na kuheshimu utawala bora ni misingi ambayo Serikali yoyote inayotokana na watu haina budi kuifuata bila shinikizo lolote kutoka nje. Kama Serikali ni ya watu haina budi Serikali hiyo kufuata misingi hiyo.”
Mikutano hiyo ya hadhara ni fursa kwetu Vijana wa Chama cha Mapinduzi kwenda Majukwaani kujenga hoja zenye mashiko kwa wananchi na kuwaeleza nini Serikali yao inafanya chini ya Rais Dkt. Samia, twendeni tukatengeneze ajenda Jenzi tusisubiri kujibu hoja au ajenda za Wapinzani wetu.
Dunia kwa sasa imepiga hatua kubwa sana katika masuala ya teknolojia, matumizi ya mitandao ya kijamii imekua kwa kiasi kikubwa sana, katika ulingo wa siasa na uendeshaji wa serikali na upashaji wa habari huwezi kuikwepa mitandao ya kijamii. Wananchi wa kileo wengi wao wana uelewa mkubwa wa nini kinachofanyika katika nchi yao, Vijana wengi ni wasomi na wana ujuzi wa matumizi ya mitandao ya kijamii.
Twendeni kwenye mikutano ya hadhara tukijua kabisa hatuendi kuzungumza na watanzania wa miaka 10-20 iliyopita, tujue kabisa tunaenda kuzungumza na kundi lenye Taarifa ambazo zinaweza kuwa sahihi au sio sahihi. Hatuwezi kama Vijana wa CCM kwenda kupambana majukwaani na vyama ambavyo havina Ilani, sisi mtaji wetu ni Ilani ya uchaguzi 2020-2025 tuisoma na tutafute taarifa sahihi za utekelezaji wake ili tupate hoja zenye mashiko na zenye ushawishi kwa wapiga kura wetu.
Chama cha Mapinduzi kimeandaa vizuri vijana na kinaendelea kuandaa vijana wake katika siasa za hoja na ushindani katika demokrasia ya kweli. CCM ni Chama chenye mfumo mzuri wa kupika vijana wenye uwezo wa kujenga hoja na kuyajua mambo mengi yanaenyoendelea katika Taifa lao kwa undani, Chama cha Mapinduzi kinaamini Vijana ndio askari wa kukilinda Chama na Serikali yake ndani na nje.
Vijana lazima tusiwa watu wa kufukia Mashimo yanayochimbwa na Wapinzani bali tuwe wachimbaji na wao washindwe kuyafukia lazima tuwe wasemaji wa Kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia katika Taifa letu. Ukubwa wa Chama cha Mapinduzi sio wa kujibu hoja za wapinzani bali ni kutenda, kuitekeleza Ilani yake, kuwahudumia wananchi wake, Jukumu la kuzungumza kukisemea Chama na Rais wetu kwa wananchi ni jukumu letu vijana wa CCM.
CCM Ipo kila mahali katika nchi hii CCM ni kubwa, CCM ni Taasisi iliyo imara yenye nguvu, ushawishi na ushupavu wa kiuongozi inayojitosheleza kila idara, mizizi ya CCM Ni mirefu mikubwa na iliyokwenda mbali sana, ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hakuna mahali hutaikuta CCM, CCM inaongoza kwa Kuwa na wanachama wengi katika nchi hii.
Tunao mtaji wa kutosha wa hoja kwani Serikali ya CCM chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mambo mengi awamu kwa awamu na hatua kwa hatua, Kila eneo matakwa na mahitaji ya wananchi yanafanyiwa kazi na machache ambayo hayajafanyiwa kazi basi yapo kwenye mchakato wa kufanyiwa kazi kwani serikali ya Rais Samia ni Serikali Sikivu sana. Huu ni Mtaji tosha wa Vijana Kwenda kujipambanua na kuzungumza yote yaliyofanyika, yanayofanyika na yanayotajariwa kufanyika, hii itakua ni njia nzuri ya kuwapa wananchi Taarifa sahihi na kufuta upotoshaji unaweza kwenda kupelekwa kwao na wanasisasa.
Ushauri wangu kwa Vijana wenzangu wa CCM Mtaji huu wa ukubwa na uwepo wa CCM kila kona ya nchi hii Utekelezaji wa Ilani Uliotukuka usitufanye tubweteke tutafuteni Taarifa sahihi tusome Ilani na Utekelezaji wake, tujue Serikali yetu imetekeza nini inatekeleza nini na nini bado lakini pia tujitahidi sana kukijua Chama Katiba yake na Kanuni zake hii itatusaidia sana Kwenda kujenga hoja tunapoenda kuzungumza na wananchi wa leo wenye uelewa mkubwa wa mambo mengi yanayoendelea katika Taifa letu kwenye mikutano ya hadhara.