Hamida Kaniacha. Vijana Jijengeni Kimaisha Aisee

Hamida Kaniacha. Vijana Jijengeni Kimaisha Aisee

Hamida ni nani wakuu na kafanya nini? Siwezi kuiangalia hiyo video!
Kila kona naona jina "HAMIDA"
Msaada wa maelezo tafadhali!
 
Sasa, kama hayo yote anaruhusiwa kumfanyia mkewe tu, hao warembo atawafaidi lini?

Wakati hana, atafute ili awafaidi

Akishakuwa nazo, azitumie kwa mkewe tu.

Mkuu, acha kupangia watu maisha. Una confuse.
Warembo unawafaidi sana tu. Lakini sio lazima ujitoe mhanga kifedha au kiakili ndio uwafaidi.
 
Mbona nimesikiliza jana kipnd cha mina ally amplifire,alikua anamhoji mjomba wa huyo kijana akawa anasema yeye ni mganga wa kienyeji anauwezo kutengeneza majini na ndyo alikua amemtengeneza huyo jini, hamida hakua msichana wa kawaida bali ni jini lilimwingilia huyo kijana,na lilimwingilia kijana kwa kua alikua anamdhihaki mjomba wake pindi linapokua lipo ndani ya mjomba wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uongo mtupu katika hilo. Asante lakini kwa post yako
 
Usitufundishe maisha, hayo yote tunajua
Ile video ya 'Hamida Kaniacha' inahuzunisha. Sijui kama hio video ni genuine (ina ukweli wote) au sio, lakini jambo la ukweli vijana wanachanganyikiwa sana wapenzi wao warembo wakiwaacha.

Vijana wenzangu niwashauri msijikite sana katika mapenzi. Pambaneni kujinasua kimaisha na kimaendeleo. Warembo wa siku hizi wanatafuta maslahi na ukiwa haumpi anakuacha aende kwa atakayempa starehe, pesa nk. Kama umejikita sana kwake, ndio mambo ya Hamida kaniacha hayo yatakuhusu. Unachangayikiwa na unaweza tumia hata madawa ya ajabu nk. Warembo wapo tu. Ukishatoka kimaisha, hawatakuzingua tena.

Kujikita sana kimapenzi ni pamoja na
1. Kutumia hela yako sana kumpatia demu starehe ambaye sio mke wako. Hiyo hela iwekeze ikuletee maendeleo yako wewe binafsi.

2. Kununua vitu vya gharama kwa demu wako kama smartphone nk. Kama si mke wako, apambane kutafuta smartphone yake.

3. Kusomesha demu ambaye sio mke wako.

4. Kuingia gharama kubwa ili demu akupende kama kukodi nyumba ya gharama, kununua nguo za gharama na zisizo za lazima. Hio hela iwekeze ujengee nyumba yako au uanzishe biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapenzi mabaya mapenzi mabaya, Banana Zoro wimbo Zoba
 
Back
Top Bottom