Hamasa ya watu kwenye kilimo na ufugaji na jinsi watu wanavyotapeliwa

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,915
HAMASA YA WATU KWENYE KILIMO NA UFUGAJI NA JINSI WATU WANAVYO TAPELIWA.

Katika siku za hivi karibuni watu wamejuwa na mwamko sana wa Ujasiriamali hasa kwenye kilimo.

Watu wamekuwa na hamasa ya kufuga aina mbali mbali za mifugo.
- Kuku
-Ng'ombe,
-Sungura
-Bata na Nguruwe

Watu pia wamekuwa na hamasa ya kulima mazao hasa ya muda mfupi kama Mazao ya nafaka kama mahindi, Mboga mboga na matunda.

UTAPELI SASA

Hapa watu wamekuwa wanatumia mwanya huu kupiga pesa ndefu sana tena mno yaani wanatengeneza pesa isiyo kuwa na jasho.

1. KUTAFUTIA WATU MASHAMBA
Mtu anahamasisha watu wachange pesa awatafutie mashamba pembeni ya mto sijui gani au wanunue shamba la ushirika. Hapa watu huingia kichwa kichwa na kulizwa pesa zao.

2. KULIMIWA KWA NIABA
Yaani unaambiwa wewe tuma.pesa sisi tutalima na kupalilia wewe utakuja kuvuna tu. Hahaaa hapa Watanzania wengi wanapenda sana kusikia kitu kama hiki yaani wanapenda utajiri ila hawapendi kujishughulisha au kuchafuka.
Watu wengi sana wamepigwa kwa staili hii kwamba unalimiwa na wao wanasimamia wewe unaenda kuvuna.

3. KUAGIZIWA SIJUI MBEGU ZA NG'OMBE AU MBUZI au KUKU.
Hapa watu wamekuwa wanashawishiwa watoe pesa kuna mbegu za Ng'ombe zitaagizwa kutoka South Africa au kwingineko.
Kwa sababu tunapenda utajiri ila hatupendi kuumiza akili watu wanapigwa.
Kuagiza Ng'ombe South Africa si swal la kitoto hata siku moja.

4. KUTOA KIINGILIOA CHA KUJIUNGA KWENYE GROUP THEN UTANUFAIKA NA KUUZA BIDHAA ZAKO.

Hapa ni sehemu pia ya kupiga pesa isiyo kuwa na jasho. Watu wamekuwa wanashawishow wajiunge kwenye Group au tasisi sijui gani na watoe pesa za kuwa wanachama na wao watafaidika kwa kuuza mazao yao au product na watauza kwa sababu kuna soko nje na ndani ya nchi.

Hapa watu huambiwa kuna soko hata USA au JAPANI au CHINA.

5. Kushawishiwa kwa kupata vitu kibao kama vile BIMA ZA AFYA, MIKOPO BENKI, Kuunganishwa sijui na nini.

Hapa napo watu wamelizwa sana kwa kuaminishwa wakijuiunga na vikundi fulani watapata Bima na pia watapata mikopo BENKI ZA BIASHARA.

6.KUPITIA PICHA
Watu bila kujiongeza wamekuwa wanapigwa kupitia picha zainazo chukuliwa google na picha zilizo pendeza za Mazao, mifugo hasa Kuku na hapa mtu huambiwa toa pesa au fanya hivi.

7. KUPITIA KWA WATU KUUNDA MAKUNDI YAO SPECIAL YA WHATSAP AU FB
Hii ndo njia mpya, mtu akitaka asishitukiwe anaunda kundi lake la whatsap na yeye anakuwa adimin na hapo yeye atawashawishi watu kwa kila namna ikiwemo kutoa pesa za viingilio na.kadhalika.

Kwenye grouop huchagua watu wa kujiunga hasa wale anao ona ni rahisi kudanganwa na kwa wale anao ona ni wajanja basi hawezi kuwaunga kwenye group.

Hapa watu hulishwa matango pori ya kutosha watu hulishwa sumu za kutosha.
Watu huaminishwa aina fulani pekee ya kitu ndo bora kuliko za wengine.

8. KUPIGIWA FAIDA KUBWA
Hapa wengi wameliwa sana mtu anapigiwa faida yaamilioni ambayo tangu azaliwe hajawahi yashika.
Mtu anapigiwa faida ya milioni 90 kwa mwaka, mtu akisikia milioni 90 anaona umasikini sasa basi.

Watu wamekuwa wanapigiwa faida tu, tena kubwa sana na hakuna hasara.

MWISHO.

Katika Dunia hii hakuna atakeye take risk kwa niaba yako yaani wewe ulalae yeye awe shambani anakulimia au anakufugia na wewe ukavune.Hakuna kitu kama hicho chini ya Jua

Tafuta mafanikio yako mwenyewe kwa juhudi zako mwenyewe kwa akili yako mwenyewe.

Watu ni wavivu wa kusoma na sana watu wanatapeliwa kwa kukosa information.

Tafuta sana informationa soma sana na kamwe hakuna atakaye kudanganya na bila hivyo utadanganywa mno na utalizwa sana.

ACHA MIHEMUKO ANZA KIDOGO KIDOGO, kama lengo ni kuku elfu 10 anza na wawili na sio uambiwe jiunge na roa pesa tukupatie vifaranga 1000.

HAKUNA SHORTCUT YA MAFANIKIO

NB: inawezekana kulimiwa, inawezekana kutafutiwa shamba, Inawezekana kugaziwa Ng'ombe na inawezekana kutafutiwa soko.ILA TAFUTA INFORAMATION KWANZA nakama nilivyo sema watu wanapigwa kwa sababu kuu 1 watu hawana Information na pia watu ni wavivu wa kutafuta information.

BY
CHASHA FARMING.
0767-691071

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nzuri sana hii wabongo tunapenda vitu rahisi na vya haraka haraka, ni kweli you are responsible for your business kwani wewe ndo mwenye uchungu na hiyo ishu yako mwingine ukimiachia atafanya sukuma twende au ili mradi tu. Btw mkubwa nilizikikubali sana zile C zako tatu.
 
Umesemaukweli haswa mkuu, watu siku hizi wamekuwa matapeli na mtu asipokuwa na taarifa za uhakika anatapeliwa kirahisi sana.
 
Mm nimekubaliana na jamaa wanasimamia project zangu za kilimo ila kila week lazima niende shambani kukagua maendeleo, kwa kweli mambo sio mabaya na wanafanya kazi kwa uaminifu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku hizi dar kila siku vikao vya wanununuzi fake wa mazao, wanahamasicha mlime maeka na maeka, mbaya zaidi hawakusaidii kwa lolote lile, watu wanapenda sana kutajirikia kwenye migongo ya watu, mfano mzuri ni projects za sungura watu wamelia balaa
 
Siku hizi dar kila siku vikao vya wanununuzi fake wa mazao, wanahamasicha mlime maeka na maeka, mbaya zaidi hawakusaidii kwa lolote lile, watu wanapenda sana kutajirikia kwenye migongo ya watu, mfano mzuri ni projects za sungura watu wamelia balaa
Sungura imekuaje mkuu maana huku Arusha tunaelezwa soko lake lipo nje hususani SAUZI?
 
Watu wameingizwa kwenye miradi ya kufuga sungura kwa kutoa hela nyingi,lakini ukweli wa mambo ni kwamba hakuna soko la sungura watanzania asilimia kubwa hawana utamaduni wa kuitafva nyama ya sungura kama kitoweo sijawahi ma mgahawa au banda la chips nyama ya sungura ikiuzwa,mtoa uzi nakushukuru kwa kutupa hekima ya kutotapeliwa bigup sana.
 
Hizi ndo threads mbashara, uzi huu nimeupa 5 stars. Ni must kwa kila mjasiriamali wa sekta hii kuupitia. Hilo suala la kupigiwa faida kubwa, limetawala sana. Mtu anakupigia hesabu hzo, anakuaminisha kabisa baada ya miaka miwili atakuwa Mo. Kwa mwelewa ukiamwambia ukweli, unaonekana kama vile umemwonea wivu mnaishia kujenga uhasama.
 
Back
Top Bottom