Makala Jr
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,395
- 1,110
Zimebaki siku chache sana kabla ya zoezi la sensa kuanzia usiku wa tarehe 25-26,August 2012. Kwa utafiti mdogo niliufanya Dar es salaam wiki iliyopita...elimu ya uraia ilikuwa bado inahitajika sana.Katika kuwahoji watu kuna uelewa mdogo sana. Kuna watu wameaminishwa kwamba SENSA ni mpango wa freemasons wa kujua idadi ya watu ili wajipange vizuri namna ya kuitawala dunia. Pia kuna wananchi wabishi sana...kuna watu wanadai sensa ya nini kama hawaletewi maendeleo kwa miaka yote waliyowahi kuhesabiwa? Inasikitisha kuona hamasa za kampeni za kisiasa zinakuwa na nguvu kuliko zoezi hili la kitaifa.Kumekuwa na malalamiko ya awali kwamba baadhi ya wale waliochaguliwa kuendesha sensa hawana uwezo wa kutosha kwani rushwa ilitumika. Kuna ujinga ulioenezwa ili kukwamisha sensa ikiwemo misimamo ya kidini,imani potofu na vitisho vya kugomea sensa.Saizi nipo Mbeya mjini kuna matumaini ya zoezi kufanikiwa.Je hapo ulipo hamasa kwa wananchi ikoje?