Kulikoni mbona nguvu kubwa sana inatumika promo ya sensa?

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,537
4,517
Salama ndugu?

Najiuliza sana... Mbona ilikuwa ni jambo la kawaida tu kwa serikali kutumia mamlaka yake KUTANGAZA TU KWAMBA TAREHE FULANI KUTAKUWA NA ZOEZI LA SENSA... HIVYO WANANCHI MTAPASWA KUFUATA MAAGIZO YAFUATAYO.

Simple...
Sasa hizi promotion kupita kiasi lengo lake ni kweli kuhamasisha tu watu wahesabiwe? Just watu wahesabiwe tu?

Yaani serikali inataka hesabu ya idadi ya watu wake... Inawahamasisha kwa nguvu kubwa hivi...

Pesa nyingi inatumika kila sekta kuhamasisha sensa... Kuanzia kwenye vyombo vya habari michezo wasanii na miziki na kila nyanja... Ni SENSA SENSA...

Hivi kuna SENSA tu kipindi hiki kama kipaumbele cha nchi au kuna kingine chini ya kapeti hakitakiwi kugundulika na ummaa...?

Nilielewa labda ni ka njia ka upigaji ka pesa za umma...pale ambapo niliona habari kwenye UTV ALASIRI LOUNGE jana. Wakiripoti "CHAMA CHA WALEMAVU WA NGOZI WAIOMBA SERIKALI IWAPE FUNGU LA PESA NA WAO... ILI NA WAO WAWEZE KUSAMBAA WILAYA MBALIMBALI NCHINI KUHAMASISHA WATU WENYE ULEMAVU JUU YA KUJIANDAA KUHESABIWA."

Kuna habari vilevile... Kuna kiongozi sikumbuki ni nani alisema...." OLE WAKE ATAKAYEVURUGA ZOEZI HILI LA SENSA".

Najiuliza hizi gharama nyingi zinazotumika kufanya promo kubwa hivi... Inategemea serikali kuzirudishaje?

HII NGUVU INAYOTUMIKA INATIA SHAKA KWAKWELI...

HII SENSA HUENDA HAINA FAIDA KWA MWANANCHI WA KAWAIDA KAMA INAVYOELEZWA...

NINA SHAKA KUNA KAUPIGAJI KABLA, WAKATI WA SENSA AU BAADA YA SENSA... NINA SHAKA...

Ni wasiwasi wangu tu.

NOTE:
* KUSEMA HAYA SIHAMASISHI WALA SINA LENGO LA KUHAMASISHA WATU WASIKUBALI KUHESABIWA.

* BINAFSI Mimi nipo tayari kuhesabiwa(kwangu mimi hainidhuru kwa lolote nikihesabiwa, na nisipohesabiwa vilevile haininufaishi kitu) .

JIANDAE KUHESABIWA... SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA.
 
Kwa sababu uelewa wa watu bado mdogo, miongoni mwa vitu wanakosea ni kutokurespond Jambo kwa mapema kwa sababu kutokuwa waelewa kwa Jambo dogo linawapa watu wengine ulaji wa kutoa elimu ya sensa
 
Wakinikuta home watanihesabia. Ila sitaacha mishe zangu wanihesabie.
Wewe fanya mambo yako tu. Wanakuhesabu ulipolala usiku wa kuamkia Tarehe 23 August. Hakikisha unalala kwenye nyumba yoyote afu toka uanze mishe.
 
Sensa ina umuhimu mkubwa sana katika Taifa na kwa sisi wenye umri mkubwa tunakumbuka hamasa zake toka siku za nyuma

Idadi ya watu ni muhimu sana katika kupanga maendeleo ya sehemu na taifa kwa ujumla. Bajeti inapangwa kwa idadi ya watu.
 
Ni kweli huenda kuna maradhi yataanza kuibukia hapa nchini endapo tukishajulikana tupo wengi kuliko...
 
Hata mm nimetafakar sana....kwenye kushangilia ubingwa wa klabu yang pendwa niliona lile bus limebandikwa mmabango ya kuhamasisha SENSA nkachoka kabsa
Umri wa mleta mada na wewe yawezekana mnalingana, suala la sensa lina historia ndefu sana mpaka kwenye vitabu vya dini lipo, na huko vijijini wapo wenye uelewa finyu kuhusu kuhesabiwa, wapo wenye imani za ajabu kuhusu kuhesabiwa, sasa serikali isipotoa elimu ya kutosha usishangae wahesabuji wanaenda kwenye nyumba ya mtu wakatolewa baruti au wakakimbia nyumba na kutokomea polini, kwahiyo wakawa wamekwamisha zoezi la sensa, kuna miji mingine lazima kwenda na uongozi wa sehemu husika na wao wakiona huo uongozi wengine wakafikiri wamekuja kukamatwa.
 
Salama ndugu?

Najiuliza sana... Mbona ilikuwa ni jambo la kawaida tu kwa serikali kutumia mamlaka yake KUTANGAZA TU KWAMBA TAREHE FULANI KUTAKUWA NA ZOEZI LA SENSA... HIVYO WANANCHI MTAPASWA KUFUATA MAAGIZO YAFUATAYO.

Simple...
Sasa hizi promotion kupita kiasi lengo lake ni kweli kuhamasisha tu watu wahesabiwe? Just watu wahesabiwe tu?

Yaani serikali inataka hesabu ya idadi ya watu wake... Inawahamasisha kwa nguvu kubwa hivi...

Pesa nyingi inatumika kila sekta kuhamasisha sensa... Kuanzia kwenye vyombo vya habari michezo wasanii na miziki na kila nyanja... Ni SENSA SENSA...

Hivi kuna SENSA tu kipindi hiki kama kipaumbele cha nchi au kuna kingine chini ya kapeti hakitakiwi kugundulika na ummaa...?

Nilielewa labda ni ka njia ka upigaji ka pesa za umma...pale ambapo niliona habari kwenye UTV ALASIRI LOUNGE jana. Wakiripoti "CHAMA CHA WALEMAVU WA NGOZI WAIOMBA SERIKALI IWAPE FUNGU LA PESA NA WAO... ILI NA WAO WAWEZE KUSAMBAA WILAYA MBALIMBALI NCHINI KUHAMASISHA WATU WENYE ULEMAVU JUU YA KUJIANDAA KUHESABIWA."

Kuna habari vilevile... Kuna kiongozi sikumbuki ni nani alisema...." OLE WAKE ATAKAYEVURUGA ZOEZI HILI LA SENSA".

Najiuliza hizi gharama nyingi zinazotumika kufanya promo kubwa hivi... Inategemea serikali kuzirudishaje?

HII NGUVU INAYOTUMIKA INATIA SHAKA KWAKWELI...

HII SENSA HUENDA HAINA FAIDA KWA MWANANCHI WA KAWAIDA KAMA INAVYOELEZWA...

NINA SHAKA KUNA KAUPIGAJI KABLA, WAKATI WA SENSA AU BAADA YA SENSA... NINA SHAKA...

Ni wasiwasi wangu tu.

NOTE:
* KUSEMA HAYA SIHAMASISHI WALA SINA LENGO LA KUHAMASISHA WATU WASIKUBALI KUHESABIWA.

* BINAFSI Mimi nipo tayari kuhesabiwa(kwangu mimi hainidhuru kwa lolote nikihesabiwa, na nisipohesabiwa vilevile haininufaishi kitu) .

JIANDAE KUHESABIWA... SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA.
Watawahesabu magasho yao mimi sihesabiwi tena ntakua bar nakula burudani
 
Back
Top Bottom