Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,568
Kiongozi wa Hamas, Mousa Abu Marzouk amesema amesema kuwa ilikuwa ni vigumu kuachiliwa mateka wanaowashikiria wakati Israel ikiishambulia Gaza kwa mabomu.
Kiongozi huyo wa Hamas ameyasema hayo wakati wa mahojiano maalumu na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), huku akiahidi kwamba kundi lake litawaacjia mateka hayo.
"Tutawaachilia. Lakini tunahitaji kusitisha mapigano," amesema kiongozi huyo wa juu wa Hamas.
Wakati takribani watu 249 wanashikiliwa kama mateka na wananmgambo wa Hamas, Wizara ya afya inayoongozwa na kundi hilo Imesema kuwa watu 10,000 wameuawa tangu Israel ianze operesheni mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa BBC, hivi majuzi Marzouk alisafiri hadi Moscow kujadili kuhusu watu wanane wenye uraia pacha wa Russia na Israel ambao ni sehemu ya waliotekwa na Hamas.
Aidha, kiongozi huyo amejitenga na madai kuhusu wananmgambo wake kuua raia, akisema kuwa kundi hilo linapambana na walengwa tu.
Kwa mujibu wa BBC, Marzouk ameliambia shilika hilo la habari kwamba wanawake, watoto na raia si sehemu ya mashambulizi ya Hamas, mazungumzo hayo yanamfanya kiongozi wa juu kuzungumza na BBC tangu mauaji ya Oktoba 7, mwaka huu.
Wangeweza tu kuwaachilia mateka, amesema, ikiwa "Waisraeli watasimamisha mapigano ili tuweze kuwakabidhi kwa Msalaba Mwekundu."
Kwa mujibu wa Marzouk, Kiongozi wa kundi la Kijeshi la Hamas la ‘Qassam Brigades,’ Mohamed el-Deif, aliwapa amri askari wake kutoua raia.
"El-Deif aliwaambia wazi wapiganaji wake 'msiue mwanamke, msiue mtoto na msiue mzee'," amesema na kuongeza kuwa; waliua walengwa, ni majeshi au askari pekee waliuawa,’ amesema.
Na alipoulizwa iwapo mrengo wa kisiasa wa Hamas ulijua kuhusu maandalizi ya shambulio hilo, kiongozi huyo amesema kuwa mrengo huo wenye silaha "sio lazima kushauriana na uongozi wa kisiasa. Hakuna haja."
Mrengo wa kisiasa, ulio na makao yake nchini Qatar, mara nyingi hujionyesha kuwa uko mbali na vikosi vya kijeshi huko Gaza, japo mataifa ya ulaya hayaoni tofauti yoyote.