Hamad Rashid: Nitaunda chama kipya!

Hamad rashid mzee wangu nakuheshimu sana,nakuomba ufute hiyo kali ya mimi na wenzangu tutaanzisha chama "chetu" siipendi,sema tu tutaanzisha chama cha kidemokrasia ya kweli,na pia kama itatokea kweli mkaanzisha hicho chama si lazima wewe uwe mwenyekiti,mfanye uchaguzi huru na wa haki apatikane mwenyekiti,kidogo mjitofautishe na hizi,chadema,cuf,tlp,nccr mageuzi na hata ccm ambako kwenye chaguzi za ndani ukijitokeza kugombea nafasi ya mwenyekiti unaonekana mkorofi au unatumiwa na "adui" kukivuruga chama!!mkifanya hivyo kukawa na uwazi kwenye chaguzi za ndani hata mimi ntajiunga!
 
Nyie cdm adui yako usimwombee mabaya,kimachotokea cuf ni kutaka madaraka na cdm haiko mbali sana na uchaguzi wa mwenyekiti.Itakumbukwa ya kwamba Zitto ndie aliehadiwa kuwa mwenyekiti pindi mbowe atakapomalizi kipindi chake na kwa jinsi mambo yalivyo cdm Zitto na kundi lake hawatakubali nafasi ya uenyekiti iende kwa kundi la dk Slaa na hapo ndio itakuwa ni mgogoro wa kusambaratisha cdm
 
Kweli hamad. Pamoja na uroho wako wa madaraka! Ni kweli cuf imeuwa dhaifu. Maalimu seif kapata alichokuwa analilia basi. Hatari ni kwamba akumbuke kuwa cuf ikifa hata hiyo nafasi atakosa. Ccm ni hatari watawauwa na huo mseto1
 
Ndio yataka vunjika kinamna flani hivi na anaeivunja ndoa yenu ni huyo mume wenu ccm
 
L.A.+Guns+-+Vicious+Circle.jpg
RIP CUF

Hiki chama hovyo kabisa hata kikifa tutashukuru Mungu
 
Huyu mpemba hana lolote.Kiherehere kingi tu.Ni mpenda ukubwa na umaarufu na hana hekima za kuvitafuta bali analazimisha.Mwisho wake ndio huu.Akajiunge na wenzake akina Akwilombe,Hizza.
Halafu kwanini vyama vipewe posho?.Sababu zake sizipendi.Hizi posho ni namna ya kuvidhibiti na kuleta ugomvi miongoni mwao.
 
Naona kama ile 'muvi' ya Jidulamabambasi na Mzee Cheyo kule UDP? CUF kwishen!
 
Hamad Rashid akianzisha chama chake, zile kura za Pemba watazigawana na CUF hivyo hata hiyo serikali ya umoja haitakuwepo tena. Pole sana Sharif.
 
Haya ndo matunda ya sera zao za jino kwa jino na bado watatafunana kama mbwa mwitu hawa hadi wabaki mifupa mitupu!!!!!!:A S embarassed:
 
ukiilani CHADEMA, wewe ndie unapata laana hiyo! HR alijitahidi kuitenga CHADEMA na wananchi wake akalaani na kuisomea Albadir na sasa yote yanamrudia yeye! CUF chukueni hatua haraka sana, fukuzeni mtu huyu arudi CCM ambao watamteua na kumpa uwaziri kwenye serikali ya Tanganyika!
Huyu hafai kuitwa Mpemba tena na wala hastahili kuwa Mtanganyika!!!! Ataendelea kutanga tanga hadi mwisho wa dahari
 
Hamad Rashid akianzisha chama chake, zile kura za Pemba watazigawana na CUF hivyo hata hiyo serikali ya umoja haitakuwepo tena. Pole sana Sharif.

Mkuu ndio kusema watarudi kwenye enzi zile za utemi !
 
siasa za tz ni full kichefuchefu,na huyu Hamad R,inavyoonekana ana kundi lake ndani ya cuf ila halijaamua kujitokeza,mpaka kufikia hatua ya kusema endapo watamtimua basi ataondoka na watu wake,nafikiri nia yake ni kukiua chama na si kujenga tena..lets wait and see
 
Hamad Rashid namkubali unapiga na mfumo mbovu wa CUF wa kuwekeza Zanzibar pekee yake.Anzisha chama kadi namba mbili itakuwa yangu nawapenda watu wasiopenda kuonewa,kunyanyaswa,kudharauliwa kisa eti Maalim makamu wa Rais wa mkoa wa Zanzibar.
 
USHAURI WA BURE HR; Samaki ana nguvu akiwa kwenye maji, ukimtoa nje hana kitu chochote hata kupumua hawezi. Nawe una nguvu kwa kuwa uko CUF ukitoka nje umekwisha. Na pia taifa limekushtukia kuwa una tamaa ya madaraka, hasa pale ulipotaka kwa nguvu uongozi wa kambi ya upinzani halafu baada ya kukosa ukaleta zengwe kuwa mahela ya kiongozi wa kambi rasmi yawe yanakaguliwa, wakati unayatafuna wala hukutuambia kama yapo. Wewe unaonekana una tamaa ya madaraka iliyozidi kifani
 
Hamad Rashid akianzisha chama chake, zile kura za Pemba watazigawana na CUF hivyo hata hiyo serikali ya umoja haitakuwepo tena. Pole sana Sharif.

Huyu HR hata huku Pemba hazungumzwi munamtaja nyinyi huko Tanganyika tu coz wanasiasa wenu huko wote ni Vilaza! Nakuhakikishia kwa 100% na zaidi hata Hamad Rashid aunde chama cha aina gani kwa huku Pemba hapati ata 0.01%, tumeshamjua huyu! Sisi ndio Wapemba wenyewe tunajua kama huku ni CUF na kwenda mbele tu hadi mwisho wa dunia.
 
hizi ndio changamoto za ndoa ya mkeka; mke anapokuwa mkali ili kuilinda ndoa yake isivunjike, ndugu wanakuwa wakali, na kutaka kuingilia mpaka mambo ya ndani! RIP CUF; hii ndiyo malipo ya dhambi ya kuwa CCM-B
 
Back
Top Bottom