Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamad Rashid: Nitaunda chama kipya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Dec 16, 2011.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,227
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  • Maalim Seif kunena leo Ikulu Zanzibar

  KIONGOZI mashuhuri wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, amesema ataunda chama kipya na kikubwa cha siasa ikiwa atafukuzwa uanachama kwa kufuata taratibu na kanuni za Chama cha CUF.

  Hamad alisema chama atakachounda mara baada ya kutoka CUF kitasheheni viongozi wengine walioko ndani ya chama hicho ambao hawakubaliani na uongozi wa sasa ambao umekifanya chama hicho kilichokuwa na nguvu kubwa kuwa dhaifu.

  Hamad alibainisha hayo jana alipozungumza kwenye kipindi cha ‘Pambazuka’ kinachorushwa hewani na kituo cha televesheni cha Channel 10 na kuongeza kuwa haogopi kufukuzwa ndani ya CUF kama alivyotishiwa na baadhi ya viongozi wenzake wanaopingana, lakini akaonya kuwa hatua hizo zifuate kanuni na taratibu za chama.

  Mbunge huyo wa Jimbo la Wawi alisema ikiwa viongozi hao watakiuka kanuni za chama za kumfukuza atawafikisha mahakamani kupinga kufukuzwa kwake, lakini iwapo ataridhika na taratibu zitakazotumika atashawishika kuunda chama kingine akishirikiana na viongozi wenzake.“Wakinifukuza sina mpango wa kuhamia chama chochote cha siasa, kwani mimi si malaya wa kisiasa. Nitawashawishi wenzangu tuanzishe chama chetu,” alisema.

  Pamoja na hayo, alisema hata wakimfukuza chama hicho kitaendelea kuwa dhaifu kwa kuwa hivi sasa viongozi hawakiendeshi chama kama taasisi.“Nimefanya juhudi kubwa za kuimarisha chama Tanzania Bara, lakini pia kwa mujibu wa katiba kila mwanachama anapaswa kuimarisha chama katika eneo analoishi na mimi naishi Kinondoni, hivyo nilikuwa sahihi kuitisha mkutano ule, lakini cha kushangaza wakawaleta Blue Guards na kuwapiganisha na wanachama,” alisema.

  Akizungumzia chanzo cha mzozo huo, Hamad alisema unatokana na kutangaza nia ya kutaka kuwania nafasi ya ukatibu mkuu na baadhi ya wanachama kuhoji masuala ya msingi ndani ya chama ambao anadaiwa kuwapandikiza.“Katika mkutano halali wa Baraza Kuu, Rakesh, Doyo Hassan na Yassin Mrotwa walihoji matumizi ya fedha za chama sh milioni 500 zipo wapi. Wakadai eti nimewapandikiza,” alisema.

  Alisema alihoji matumizi ya sh milioni 307 katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, lakini mpaka sasa hajapatiwa majibu jinsi fedha hizo zilivyotumika.“Watu wanapohoji matumizi hayo, wanaambiwa ni kundi langu, lakini katika uchaguzi huo, Mtatiro anasema walitumia sh milioni 49 kukodi ndege mara tatu. Atuambie chenji yetu iko wapi?“Wanatumia rasilimali za chama kuchafua jina langu bila kunishirikisha.

  Hivi kutangaza nia ya kuwania nafasi ya ukatibu mkuu imekuwa nongwa? Mbona Maalim Seif ametangaza nia hiyo katika mkutano wa baraza kuu?” alihoji.Alisema kuwa baadhi ya viongozi wanamtuhumu kuhongwa sh milioni 700 na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumshawishi Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) kugombea urais kwa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao na yeye awe mgombea mwenza na pia wanamtuhumu kukipa nguvu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).“Madai yote haya yanayoelekezwa kwangu hayana ushahidi wowote.

  Mtatiro ananiita muasi, amepata wapi mamlaka hiyo? Ina maana ameshanihukumu bila ya kunisikiliza? Mbona hatuendi na kaulimbiu ya chama ‘Haki sawa kwa wote?’ “Mimi sina ukorofi, lakini wao wanatumia vikao kunichafua, sipewi nafasi nikizungumza kwenye vyombo vya habari naonekana mkorofi, sasa wanataka nifanyeje?” aliuliza mbunge huyo.Alionesha kushangazwa kwake na kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ambayo alisema ndani ya CUF haipo, labda kama imeundwa hivi karibuni.

  Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad leo anakutana na waandishi wa habari Ikulu, Zanzibar. Hata hivyo haijajulikana nini atakiongea, ingawa kuna madai kuwa atazungumzia sakata hilo la mgogoro baina yake na Hamad Rashid.Katika siku za hivi karibuni kumezuka mzozo kati ya mbunge huyo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, uliosababisha kuzuka kwa mapigano makali na watu kadhaa kujeruhiwa baina ya wanachama wanaowaunga mkono.::Tanzania Daima::

  UP DATE 22:51
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 31,175
  Likes Received: 5,464
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD] Hamad Rashid: Nitaunda chama kipya
  • Maalim Seif kunena leo Ikulu Zanzibar

  na Tamali Vullu


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] KIONGOZI mashuhuri wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, amesema ataunda chama kipya na kikubwa cha siasa ikiwa atafukuzwa uanachama kwa kufuata taratibu na kanuni za Chama cha CUF.
  Hamad alisema chama atakachounda mara baada ya kutoka CUF kitasheheni viongozi wengine walioko ndani ya chama hicho ambao hawakubaliani na uongozi wa sasa ambao umekifanya chama hicho kilichokuwa na nguvu kubwa kuwa dhaifu.
  Hamad alibainisha hayo jana alipozungumza kwenye kipindi cha ‘Pambazuka’ kinachorushwa hewani na kituo cha televesheni cha Channel 10 na kuongeza kuwa haogopi kufukuzwa ndani ya CUF kama alivyotishiwa na baadhi ya viongozi wenzake wanaopingana, lakini akaonya kuwa hatua hizo zifuate kanuni na taratibu za chama.
  Mbunge huyo wa Jimbo la Wawi alisema ikiwa viongozi hao watakiuka kanuni za chama za kumfukuza atawafikisha mahakamani kupinga kufukuzwa kwake, lakini iwapo ataridhika na taratibu zitakazotumika atashawishika kuunda chama kingine akishirikiana na viongozi wenzake.
  “Wakinifukuza sina mpango wa kuhamia chama chochote cha siasa, kwani mimi si malaya wa kisiasa. Nitawashawishi wenzangu tuanzishe chama chetu,” alisema.
  Pamoja na hayo, alisema hata wakimfukuza chama hicho kitaendelea kuwa dhaifu kwa kuwa hivi sasa viongozi hawakiendeshi chama kama taasisi.
  “Nimefanya juhudi kubwa za kuimarisha chama Tanzania Bara, lakini pia kwa mujibu wa katiba kila mwanachama anapaswa kuimarisha chama katika eneo analoishi na mimi naishi Kinondoni, hivyo nilikuwa sahihi kuitisha mkutano ule, lakini cha kushangaza wakawaleta Blue Guards na kuwapiganisha na wanachama,” alisema.
  Akizungumzia chanzo cha mzozo huo, Hamad alisema unatokana na kutangaza nia ya kutaka kuwania nafasi ya ukatibu mkuu na baadhi ya wanachama kuhoji masuala ya msingi ndani ya chama ambao anadaiwa kuwapandikiza.
  “Katika mkutano halali wa Baraza Kuu, Rakesh, Doyo Hassan na Yassin Mrotwa walihoji matumizi ya fedha za chama sh milioni 500 zipo wapi. Wakadai eti nimewapandikiza,” alisema.
  Alisema alihoji matumizi ya sh milioni 307 katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, lakini mpaka sasa hajapatiwa majibu jinsi fedha hizo zilivyotumika.
  “Watu wanapohoji matumizi hayo, wanaambiwa ni kundi langu, lakini katika uchaguzi huo, Mtatiro anasema walitumia sh milioni 49 kukodi ndege mara tatu. Atuambie chenji yetu iko wapi?
  “Wanatumia rasilimali za chama kuchafua jina langu bila kunishirikisha. Hivi kutangaza nia ya kuwania nafasi ya ukatibu mkuu imekuwa nongwa? Mbona Maalim Seif ametangaza nia hiyo katika mkutano wa baraza kuu?” alihoji.
  Alisema kuwa baadhi ya viongozi wanamtuhumu kuhongwa sh milioni 700 na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumshawishi Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) kugombea urais kwa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao na yeye awe mgombea mwenza na pia wanamtuhumu kukipa nguvu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
  “Madai yote haya yanayoelekezwa kwangu hayana ushahidi wowote. Mtatiro ananiita muasi, amepata wapi mamlaka hiyo? Ina maana ameshanihukumu bila ya kunisikiliza? Mbona hatuendi na kaulimbiu ya chama ‘Haki sawa kwa wote?’
  “Mimi sina ukorofi, lakini wao wanatumia vikao kunichafua, sipewi nafasi nikizungumza kwenye vyombo vya habari naonekana mkorofi, sasa wanataka nifanyeje?” aliuliza mbunge huyo.
  Alionesha kushangazwa kwake na kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ambayo alisema ndani ya CUF haipo, labda kama imeundwa hivi karibuni.
  Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad leo anakutana na waandishi wa habari Ikulu, Zanzibar. Hata hivyo haijajulikana nini atakiongea, ingawa kuna madai kuwa atazungumzia sakata hilo la mgogoro baina yake na Hamad Rashid.
  Katika siku za hivi karibuni kumezuka mzozo kati ya mbunge huyo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, uliosababisha kuzuka kwa mapigano makali na watu kadhaa kujeruhiwa baina ya wanachama wanaowaunga mkono.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,017
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  [​IMG]RIP CUF
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 22,496
  Likes Received: 14,125
  Trophy Points: 280
  Hamad Rashid is running away like headless chicken.
   
 5. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,099
  Likes Received: 4,202
  Trophy Points: 280
  Muanzisha hii lazima utakuwa unatumia Laptop kutoka kwa Hu Jintao...thread ina matege!
   
 6. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 1,761
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Hamad Rashid aliibuliwa na Mkapa kwa kupewa ubunge wa upendeleo ('viti maalumu 10 vya rais'), umakini wake ukafanya wabunge wa upinzani wamteua kuwa kiongozi wa upinzani bungeni, siasa hubadilika, leo kaukosa ukuu wa upinzani bungeni (hata baada ya kuja na dhana ya minority group na kina Kafulila) ndo tunaona rangi yake halisi ya TAMAA na KUPENDA MAMLAKA anahangaika kuhasimisha CUF, Kama anadhani anaweza kuidhoofisha CUF basi aanzishe hicho chama ('utabiri wa Mayage atautimiza') tuuone mwisho wa mwanzo wake
   
 7. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,901
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Kumbe amejua atafukuzwa, nilizani anapigana kuijenga CUF kumbe alikuwa na lengo lake, watu wengine amejuaje chama atakachounda kitakuwa kikubwa.
   
 8. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 11,704
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Who will trust you this time you mean the business?
  I bet you, in Africa now, there are so many confused people all around. Almost in all spheres.And the painful thing is the guys have the ability still yet to convince people to become followers.
   
 9. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,901
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Jamani naombeni msaada anasema endapo ataridhika na taratibu za kufukuzwa, sasa kama ataridhika kwa nini tena aunde chama kingine akiache kinachofuta taratibu? just thinking aloud.
   
 10. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 792
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hana lolote huyu anatapatapa kwa kukosa madaraka baada ya kukosa kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni
   
 11. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,721
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kila chenye mwanzo hakiosi mwisho...
   
 12. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 1,761
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 160
  Unakumbuka 'umaarufu' alioupata 'naibu waziri mkuu' wa kipindi cha Mwinyi! HR kapata umaarufu ndani ya cuf na sasa angependa kuwa kama A.L. Mrema
   
 13. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 931
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Goodbye CUF!
   
 14. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 2,991
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hawezi kuwacha mwenyewe kwa sasa anaogopa kukosa 'ze posho'
   
 15. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,225
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Hamad sasa ni wakati wa kuunda chama na kukiita wachuja nafaka! Sipati picha kitakavyowika...
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Dec 16, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,788
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mie nashangilia kweli ninavyomuona Hamad akiweweseka........... aliwashambulia sana CHADEMA kwa sifa zote ambazo ndizo anazozitekeleza kwa sasa!!

  Ni mnafiki, mzandiki, choyo, kigeugeu, mwongo, mbinafsi you name it

  kweli siku hizi baya hulipwa hapahapa duniani
   
 17. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #17
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,227
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mtatiro kajibu
   
 18. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,227
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  namkubali huyu jamaa. Ni mpiganaji. Go hamad!
   
 19. Jakubumba

  Jakubumba JF-Expert Member

  #19
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 1,627
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Siasa bwana ni mchezo mchafu, hata wewe mtatiro wala sikuamini maana unapambana upande wako.
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Dec 17, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,177
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Duh! HR nilifikiri ulikuwa una point, kumbe hata wakifuata taratibu lazima utaondoka kuunda chama??

  Sasa si ungeunda tu chama chako bila kuharibu CUF

  What a stupidity?? kwani lazima unyee kambi kwanza au ulikuwa kwenye mission from very beginning
   
Loading...