Hamad Rashid na kauli tata!!

Maswali yangu ni haya;
  1. Kwa nini kama CUF imepasuka anaing'ang'ania hadi mahakamani?
  2. Ikumbukwe kuwa Mtatiro anasema hata kama mahakama itamrudisha maamuzi yao POLITICALLY yako palepale, je HR anaweza kufanya kazi bila ushirikiano na wenzakle endapo atarudishwa?
  3. Kwa nini kama yeye ni jasiri na ana support ya watu kama anavyodai asiachane na hiyo kesi akaendelea na taratibu nyingine za kufungua chama chake na kuleta tumaini jipya analosema wananchi wanahitaji?
Jimbo likiwa wazi, uchaguzi unatakiwa ufanyike ndani ya siku 90. Si rahisi Mh. Hamadi kuanzisha chama kikapata usajili ndani ya siku 90 ili agombee tena Ubunge. The same happened to Mpendazoe, he failed completely to register his party
 
Wadau jana nilimsikiliza HR akiongea na waandishi wa habari mara baada ya shauri lake kusikilizwa na mahakama! Katika maelezo yake alidai kuwa ana imani kubwa na mahakama na ana imani kuwa itatenda haki. Kimsingi ukimuangalia HR ni kwamba anaung'ang'ania uanachama wa CUF kwa udi na uvumba na ndio kisa cha kwenda mahakamani!

Lakini kinachonishangaza ni kwamba katika maelezo yake aliendelea kusema kwamba CUF IMEPASUKA na wananchi wasubiri tumaini jipya. Akatoa mfano akimnukuu Mwalimu Nyerere kuwa alipata kusema kuwa kioo kikiingia vumbi kifute na kikipasuka kiondoe kwa hiyo alimaanisha kwamba CUF imepasuka na inapaswa kuondolewa. Hapa mimi nilifikiri anazungumzia wazo lake la kuanzisha Chama.

Maswali yangu ni haya;
  1. Kwa nini kama CUF imepasuka anaing'ang'ania hadi mahakamani?
  2. Ikumbukwe kuwa Mtatiro anasema hata kama mahakama itamrudisha maamuzi yao POLITICALLY yako palepale, je HR anaweza kufanya kazi bila ushirikiano na wenzakle endapo atarudishwa?
  3. Kwa nini kama yeye ni jasiri na ana support ya watu kama anavyodai asiachane na hiyo kesi akaendelea na taratibu nyingine za kufungua chama chake na kuleta tumaini jipya analosema wananchi wanahitaji?
Nawasilisha
Sioni kosa la HR, nadhani anajua analolifanya sisi tusubiri.
 
Kimsingi Hamad Rashid ana mgogoro mkubwa na Maalim Seif, Maalim Seif ni andiko la kimungu ndani CUF Zanzibar na wa Zanzibar 90% waliopo bara. Ana makosa yake kama Hamad lakini ni ya kimtego zaidi, wanasema hata ile kuingizwa kwake kizuizini na akina Seif eti ilikuwa ni janja ya CCM kutafuta nini mpango wa Seif and team, wanasema alienda kwa kutumwa na CCM kuwasihi vijana wale wa kiPemba waliokimbilia shimoni Mombasa, wanasema hata kuteuliwa kwake kuwa Mbunge na mzee Mkapa hakukuwa na baraka za CUF bali CCM kama asante kwa kazi nzuri. Hii ndio sumu wanayolishwa Wapemba na CUF Seif; wanasema Jussa ndio aliyetoa siri eti posho wanazolipwa bungeni ni nyingi sana kuliko ilivyoripotiwa na Hamad akiwa mkuu wa Upinzani, kwah hiyo Hamad si mchangiaji wa chama zaidi ya tumbo lake, wanasema ameoa mbara na anatumia kofia ya chama ktk biashara zake binafsi.

Fitna ya namna hii inaposukwa na usalama wako ni nini? Kimsingi huyu mzee kosa lake ni ku join hand na wenzake juu SUZ na kuuleta ushirika huo kule Bungeni, alipaswa asiruhusu malumbano na CDM na akaishi ktk low profile, tuhuma na majungu haya amejengewa kabla ya uchaguzi mkuu lakini pia CUF walikuja na agenda ya mabadiliko ktk watendaji wake mpaka Bungeni ilitosha kwa mzee Hamad ku opt ktk low profile ili agenda hii ya kujibu mapigo ya sasa inoge uzuri. Sasa ni kama yatima ktk vita ya kweli kabisa ila ana tatizo moja, nani amuunge mkono wakati hakuna win - win situation !!! Hamad kule Pemba hana nguvu maana hata kura za maoni alishindwa na Seif akampigia kifua kugombea, nani atakayemuunga mkono hapo?


Ukimuunga mkono mzee Hamad inataka ukomavu wa hali ya juu ktk siasa na subira ya matunda ya kazi hiyo ya kujipambanua iive na kuzaa matunda.

Amewashangaa CUF kwa kumnyima yeye muda wa kuandaa utetezi wakati wao wamelialia mbele ya jaji juu ya hilohilo....akasema huu ni ushahidi mmojwapo unaothibitisha chama hiki kukosa muelekeo.
 
Kwa mtazamo wangu, Hamad Rashid ana haki ya kupinga mahakamani kufukuzwa kwake kwenye chama. Akirejeshewa uanachama ndipo anaweza kuamua kujiondoa kwenye CUF, na hiyo itamjengea heshima zaidi kuliko kufukuzwa. Tuhuma zilizosababisha kufukuzwa kwake hazina uzito kivile. Naona zaidi ni uhuni tu uliofanywa na Maalim Seif na wafuasi wake. Viongozi wetu wajifunze kuwa wavumilivu wanapokosolewa. Kwa hili namuunga mkono Hamad Rashid, japokuwa huwa sikubaliani na baadhi ya misimamo yake kwenye masuala mengine.

Mkuu hapo umenena, huyu jamaa "Hamadi" sio, Ila anachokipigania Kafu na mahakamani ni haki yake, na hata kuanzisha Chama pia.
 
Mimi nafikiri HR yuko sawa kabisa na ni kweli kwamba anangangania kuwa mwanachama wa CUF kwa sasa yeyey anachokitafuta ni kurudi bungeni, kumbuka yeye si mjinga na pia kumbuka yeye si mgeni kwenye siasa za kibongo kwa hiyo anajua vema wapi pa kupita, na kauli kwamba CUF pana matatizo ameirudia kuonyesha uimara wake kwamba hatishiki mimi nafikiri jamaa ni shujaa pia kwani amekuwa muwazi sana kwenye hili jambo na natumai atafanikiwa kwani ni moja ya wabunge ninao wakubali sana kwenye bunge letu achilia mbali masuala ya vyama.
 
Mimi ningeshauri thread hii tuwaachie wenyewe wapemba wenye Cuf yao, Watanganyika hapa hatuusiki ni sawa na kushabikia siasa za Congo.
 
kutoka kirahisi kwenye chama ulichowekeza nguvu yako,si jambo rahisi kama mtu anavyoweza kudhani....
Na hata kuanzisha chama si mchakato mdogo,na hasa kipindi hiki ambapo watu hawaangalii,chama,bali mgombea wanayemwamini...
Mara nyingi wanasiasa hufikiria kuacha siasa,au kuhamia chama pinzani chenye nguvu,au kurudi CCM na kutulia,mfano Dr.M.R.M.Lamwai.
 
Anaweweseka tu.

Kumbuka CUF siku zote wakivunja basi hawajengi tena pale.awaulize akina Mapalala au Bi Naila jidawi watamjuza hilo.
sawa ila SEIF ni tatizo kwa nini kawafukuza James and Jidawi ambao wanatofautiana na yeye?
 
Acha vita wapigane wenyewe kama zawadi yao na laana yao cuf ya kuisaliti CDM na wanamageuzi wote pale igunga kwenye uchaguzi ili unabii utimie na kila kilichoandikwa mioyoni mwa wazalendo kithibitike. BRAVO CHADEMA.
 
utasikia karudi CCM
HAWAELEWEKI HAWA
namwona sawa na mrema kazi kuharibu vyama.
 
Anaweweseka tu.

Kumbuka CUF siku zote wakivunja basi hawajengi tena pale.awaulize akina Mapalala au Bi Naila jidawi watamjuza hilo.
Anachotaka Hamad ni kuhakikisha kwamba anawakomoa akina Seif. Anataka kuhakikisha kwamba CUF inaingia kaburini wakati inajifungua mtoto wa CCM, ambae ni chama chake. Mmemwaga mboga, yeye anamwaga Ugali! Nyambaf!!!!
 
Anaweweseka tu.

Kumbuka CUF siku zote wakivunja basi hawajengi tena pale.awaulize akina Mapalala au Bi Naila jidawi watamjuza hilo.
Ivi Bi Naila alirudi CCM vile au? sijamsikia siku nyingi kweli huyu mama
 
Wanasiasa aina ya HR ni "vigeu geu"
Dhambi aliyowafanyia CHADEMA kutaka nafasi ya kuwa "Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani" Bungeni INAMTAFUNA. Na haitamuacha mpaka immalize kisiasa! Bwana zake Sisi Em wamemkimbia hana pa kushika!
 
namshauri Hamad arudi Wawi jimboni kwake akasome upepo siyo kushinda maelezo na waandishi! Au ni kweli hakubariki kule?
 
Anapigania kuendelea na ubunge na wala si uanachama wa CUF kama wengi mnavyodhani.
 
Back
Top Bottom