Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 56,395
- 92,720
Hamad Rashid: Nitapambana na Seif hadi kieleweke
Joseph Zablon
MBUNGE wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed amesema anasubiri kwa hamu barua ya kuitwa na Kamati ya Maadili ya chama hicho, akijinasibu kwamba, mtu mzima hatishiwi nyau.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Hamad Rashid alisema anasikia tu katika vyombo vya habari kuhusu suala hilo, lakini binafsi hajaelezwa chochote na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Julius Mtatiro jambo alilosema ni ukiukwaji wa katiba ya chama hicho.
Kilichofanyika ni ukiukwaji mkubwa wa katiba, kwani kimsingi nilipaswa kuitwa katika vikao vya chama na sio kuhukumiwa na kushutumiwa kupitia vyombo vya habari. Nasema na uandike kwa wino mweusi kabisa kuwa, mtu mzima hatishiwa nyau, alisema.
Mbunge huyo aliyekuwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alisema pamoja na kuisubiri barua ya kuitwa katika kikao hicho cha baraza la maadili, atapambana na Maalim Seif kuwania ukatibu mkuu CUF hadi kieleweke.
Kauli ya mbunge huyo, imekuja siku moja baada ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Julius Mtatiro kutoa kauli kwenye mkutano na wanahabari akidai kuwa kuwa kitendo cha Hamad Rashid kufanya mkutano na wanachama wa Tawi la Chechnya, Manzese bila kutoa taarifa ofisi za chama makao makuu ni kwenda kinyume na taratibu za chama.
Mtatiro alisema kuwa katika mkutano huo ambao ulivamiwa na walinzi wa chama hicho wa Blue guard, Hamad Rashid aliungana na wajumbe wengine wa baraza kuu la chama hicho kuendesha mikutano hiyo kinyume na utaratibu wa CUF na kudai kwamba anachofanya Hamad Rashid ni umafia kwa kuwa ukatibu mkuu hautafutwi kwa njia hiyo.
Lakini, jana Hamad Rashid alisema kuwa CUF ina utaratibu wake katika kushughulikia mambo ikiwa ni pamoja na vikao kwa kujibu wa katiba ya chama hicho na siyo kupitia vyombo vya habari.
Alisisitiza kuwa atawania nafasi hiyo na kwamba nia yake hiyo aliieleza katika mkutano wa hadhara na wapiga kura wake katika Jimbo la Wawi aliosema wamemuunga mkono.
Hakuna mjadala ni lazima niwanie nafasi hiyo ya ukatibu mkuu wa chama kwani ni haki yangu ya kikatiba na sifa ninazo za kufanya hivyo, alisema.
Katika hatua nyingine, Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF ambaye pia ni Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa alisema kinachotokea ndani ya chama hicho anakisikia tu katika vyombo vya habari na hajaelezwa kitu gani kinachoendelea.
Sijui chochote, nasikia tu katika vyombo vya habari licha ya kuwa mimi ni mjumbe wa baraza kuu taifa, alisema.Sakata hilo linatokana na vurugu zilisababisha watu kadhaa kujeruhiwa kwa kukatwa mapanga zilizozuka wakati Hamad Rashid alipokwenda kufanya mkutano na wanachama wa Tawi la Chechnya lililopo Manzese jijini Dar es Salaam.