Ameshangaa kuona amri ya mahakama ikivunjwa na kikao kilichokuwa na Makamu wa Rais pamoja na watu wengine ambao ni wanasheria. Mnamo saa tatu na nusu mahakama jijini Dar iliamuru kusimamishwa kwa kikao hicho, lakini maofisa makao makuu ya CUF Dar wakakataa kupokea barua kutoka kwa karani wa mahakama. Mwanasheria wake (Hamad) akaamua kumtumia Hamad amri ya mahakama kwa njia ya e-mail huko Zanzibar kilipokuwa kikifanyika kikao cha Baraza Kuu, na Hamad akaiprint na kumpatia Katibu Mkuu (Maalim Seif), lakini either Seif hakuitoa/kutangaza kwenye kikao au alitangaza ikapuuzwa kikao kikaendelea. Kabla ya watuhumiwa wote 14 kumalizika kuhojiwa, maamuzi ya yakatolewa chap chap dhidi ya watuhumiwa wachache (nadhani wanne) ili walau ijulikane Hamad amefukuzwa, halafu ndio wengine waliobaki wakaendelea kuhojiwa !!
Hayo ni matamshi ya Hamad alipokuwa akiongea kwa simu LIVE pale mlimani TV asubuhi hii