Hamad Chande: Mkoa wa Kagera unachangia 2.6% ya Pato la Taifa

Hamad Chande: Mkoa wa Kagera unachangia 2.6% ya Pato la Taifa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,327
Reaction score
15,817
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 47 leo Juni 13, 2023.


​


Naibu wa Waziri wa Fedha, Hamad Chande amesema “Kwa mujibu wa taarifa ya National Accounts for Tanzania Mainland iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu hadi kufikia Mwaka 2021 Mkoa wa Kagera ulichangia 2.6% ya Pato la Taifa ukilinganisha na 2.5% kwa Mwaka 2020

Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge Anatropia Theonest aliyehoji Mkoa wa Kagera unachagia kiasi kwenye pato la Taifa?


Muswada wa Sheria ya marekebisho ya Sheria mbalimbali
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt. Eliezer Feleshi amewasilisha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2023 Bungeni Jijini Dodoma ikiwemo Sheria ya Mazishi ya Viongozi wa Kitaifa, Sura ya 419 ambapo pamoja na mambo mengine marekebisho haya yanakusudia kutoa mamlaka kwa Rais kutangaza tarehe ya maziko ya Rais aliyefariki akiwa madarakani kuwa ni siku ya mapumziko.

“Sehemu ya Tano ya Muswada inapendekeza marekebisho kwenye Sheria ya Mazishi ya Viongozi wa Kitaifa, Sura ya 419 ambapo kifungu cha 6 kinapendekezwa kufutwa na kuandikwa upya kwa lengo la kuboresha masharti kuhusu mamlaka ya Rais kutoa tangazo la kifo cha Kiongozi wa Kitaifa au Kiongozi mahsusi aliye madarakani”

“Marekebisho hayo pia yanampa mamlaka Kiongozi mahsusi aliye madarakani kutoa tangazo la kifo cha Kiongozi mahsusi mstaafu, vilevile marekebisho haya yanakusudia kutoa mamlaka kwa Rais kutangaza tarehe ya maziko ya Rais aliyefariki akiwa madarakani kuwa ni siku ya mapumziko”

“Lengo la mapendekezo haya ni kuweka bayana na kutofautisha mamlaka zinazopaswa kutoa matangazo ya vifo vya Viongozi wa kitaifa na Viongozi mahsusi, vifungu vya 9 na 10 vinapendekezwa kurekebishwa ili kutoa Mamlaka kwa Kiongozi mahsusi aliye madarakani kutoa tangazo la kifo cha Kiongozi mahsusi mstaafu, lengo ni kutambua utaratibu unaotumika sasa ambapo pamoja na kwamba Sheria imemtaja Rais kama mamlaka ya kutoa tangazo la kifo cha Kiongozi mahsusi mstaafu, matangazo ya aina hiyo kwa kawaida yamekuwa yakitolewa na Viongozi mahsusi walio madarakani”
 
Worthless pieces of [I couldn’t find the shit emoji]….
 
Back
Top Bottom