Halotel hongereni sana, ila Tigo, Vodacom na Airtel mnazingua, jichunguzeni

lindunduru

JF-Expert Member
Aug 2, 2015
392
551
Habari ya jumapili ndugu zangu wana jamvi, na hongereni kwa sikuku ya kubebika, endelea kudeka kama unadekezwa

Narudi kwenye hoja ni hivi mimi nina hizo line zote tajwa hapo juu, huwa napenda kuunga kifurushi cha mwezi mzima,, Changamoto ya hiyo mitandao mingine isipokuwa halotel iko hapa

Kifurushi unachochagua wanasema ni cha mitandao yote, ila ukishaunga unga unakuta wanakwambia dakika 500.

Mitandao yote halafu zilizobaki kama 600 ni kuelekea mtandao husika, maswali yangu:
1) Kwanini mnaudanganya umma kuwa ni mitandao yote wakati siyo hivyo?
2) Mzazi wangu aliko kuna halotel tu,na mke wangu aliko kuna tigo tu, sasa nikiunga kifurushi cha mitandao yote airtel kwa ajili ya kuongea hasa na vipenzi wangu hao,kwake nini mnipe masharti wakati wakati ni uzembe wenu kutopeleka mitandao yenu kule?

Mnazingua sana, kuanzia leo naanza kuwashawishi watu kama mitandao yote tumieni halotel ndo wakweli.

Happy valentines ndugu zangu.
 
Hao halotel ndo wahun kupita...hakuna tofaut ya mitandao hapa bongo.wote ni ndugu
 
Halotel ndio best kila kitu...laini nyingine kwangu zimesalia pambo tu kupokelea simu...
 
Nawashukuru sana watu wa mitandao kwa kutuunganisha na ndugu, jamaa na marafiki kwa urahisi kiasi hiki; enzi zileeee simu za mkorogo sijui ama barua unangoja miezi sita hadi 12 wasort na kutuma posta. Hii ilikuwa hatari na nusu. Tatizo la Watanzania ni kutotunza kumbukumbu ya matukio. Niongeze volume, au!???
 
Nawashukuru sana watu wa mitandao kwa kutuunganisha na ndugu, jamaa na marafiki kwa urahisi kiasi hiki; enzi zileeee simu za mkorogo sijui ama barua unangoja miezi sita hadi 12 wasort na kutuma posta. Hii ilikuwa hatari na nusu. Tatizo la Watanzania ni kutotunza kumbukumbu ya matukio. Niongeze volume, au!???
Mkuu huwezi kupingana na mabadiliko ya dunia.

Kila kizazi kinaishi katika nyakati zake za heri na karaha.

Haya ni mabadiliko ya technolojia duniani.

Tambua pia hii ni biashara yenye faida kubwa na mzunguko mzuri wa fedha kwa siku.

Sioni haja ya kuyashukuru makampuni haya wakati ni wewe ndo umeajibika kumiliki simu.
 
Mkuu huwezi kupingana na mabadiliko ya dunia...
Simu unayomiliki umeitengeneza wewe!? Imagine wangeweka iwe ya periodic servicing kama Bastola na Bunduki, na kwamba haiwezi kuwa private device. Fikiria kidogo sawa!? Tatizo mnawahi sana kuvizoea vitu vya jirani!!!
 
NIMEKOMA kuisifia mitandao ya simu! Juzi tu hapa nilifungua uzi kuwasifia Airtel na kifurushi chao cha "New Smartphone Offer"

Tafadhali msiniulize kulikoni kwa sababu SITAWAJIBU kutokana na uchungu nilionao! Hapa eti bado nahisi kama kulikuwa na something wrong na hivyo nataka kujaribu tena ili nione ikiwa yale yaliyonitokea mara 3 ndo yako vile au ilikuwa ni makosa tu ya kiufundi! Siamini!

Yote kwa yote, ni busara sana mtu kutopoteza muda wako kuisifia hii mitandao ya simu kabla hicho unachokisifia hujaki-experience kwa muda wa kutosha!
 
Halotel wapo vizuri sana ndugu kuanzia vifurushi vya dakika,sms hadi data.Hawana longo longo kamwe had kufikia sasa.
Labda huko kwenu lakini kwa wengine, Halotel nao hawana tofauti na wengine manake wasingekuwa na longo longo wasingeshusha night bundle kutoka 10GB to 4GB!

Hawa wote ni wale wale tu manake siku naona hata speed yake kwa maeneo ninayoishi imepungua sana! Yaani kwangu hivi sasa linapokuja suala la speed, Voda, Airtel, na TTCL imekuwa ndo best kuliko Halotel hadi nikaamua kuachana nao!!
 
Simu unayomiliki umeitengeneza wewe!??? Imagine wangeweka iwe ya periodic servicing kama Bastola na Bunduki, na kwamba haiwezi kuwa private device. Fikiria kidogo sawa!??? Tatizo mnawahi sana kuvizoea vitu vya jirani!!!
Kwani bila pesa ningemiliki simu.
Kila mtu product ili aweze kuuza.
Ninachokimiliki ni changu,
Hivyo bila purchasing power siwezi kumiliki chochote
 
Back
Top Bottom