Tryagain
Member
- Nov 23, 2021
- 66
- 436
Ndugu zangu mara nyingi tumekuwa na sababu nyepesi sana za kiuchumi pale kampuni zetu zinapoanza kufanya vibaya kwenye soko.
Nimeona kuna taarifa zinazosambaa kuhusu wateja milioni 1.3 kuacha kutumia mtandao wa Vodacom na sababu wakasema ni Tozo hii si kweli kwa asilimia 100.
Wakati wa Utendaji wa Bodi ya wakurugenzi Rostam Aziz Vodacom ilitengeneza mapato mengi kutoka na strategy yao ya kuanzia chini kwenye grass root level kupeleka huduma kwa Wananchi.
Voda wameuacha huu muundo wamebakia mijini huduma za M-Pesa katika mikoa ya Morogoro, Tanga, Manyara, Lindi, Mtwara, Mbeya, Ruvuma zinapatikana mijini tu na Wilaya ni tabu kupatikana.
Huku Tigo wanapatikana katika kila kitongoji na kila kijiji achana na huduma ya Mobile Money tu, huduma ya mawasiliano kwa voda ni tabu na pia imekuwa ya gharama sana ukilinganisha na huduma za mawasiliano kama Tigo na Airtel.
Kama ni Tozo zimewaondoa wateja wa Voda, Airtel ingepata wateja wengi zaidi ila Tigo waliona soko mapema wakajikita kuboresha huduma kwa kipindi cha miezi mitano kampuni ya Tigo imeongeza wateja milioni 1.2.
Kama Voda wanasema kuwa ni Tozo zimewaondolea wateja, vipi kuhusu Halotel na TTCL ambazo zimepoteza wateja wengi ndani ya kipindi kifupi.
Wananchi wa Tanzania wanaishi kwenye word of mouth hawa Tigo wameweza sana kuishi nao wana ubunifu ukitazama kwa kipindi cha miezi mitano Voda hana jambo lolote la kibunifu kwa wateja wake.
Idara ya masoko ya Vodacom imefeli pakubwa haina jipya itafute sababu nyingine.
Mbuzi wa kafara hufa huku akilia.