Halmashauri zinakufa, Wabunge mko wapi

Halmashauri zinakufa, Wabunge mko wapi

Mpaka watu wakishindwa kulipwa mishahara sirikalini ndio buku7 watatia akili.
 
Nchi ilishafilisika soon tunakuwa category 1 na Zimbabwe toka Juma ponda Mali aseme matajiri wataishi kama mashetani nimemdharau sana
Kauli za makondacta wa daladala
 
Kinachoendelea katika halmashauri zetu ni kitu cha hatari kabisa.Ukata wa hali ya juu,ukata wa kukwamisha kwa kiwango kikubwa utoaji wa huduma kwa wananchi.

Wadau kwa wale wasio na taarifa ni kwamba halmashauri zipo kwenye hali ngumu sana ya kukosa ruzuku ya kujiendesha na ruzuku za miradi ya maendeleo.Ukata huu umefanya baadhi ya halmashauri zisizo na mapato ya ndani ya kutosha kushindwa kutoa huduma kwa wananchi.Imefikia wakati idara inakosa hata rim papers za kuandika taarifa.

Halmashauri hazikopesheki tena kwa wazabuni,wazabuni wanashinda halmashauri kudai pesa zao.Halmashauri zinaua mitaji ya wafanyabiashara

Watumishi wamekataa tamaa wamepauka hawajui kesho yao,stahiki zao hawajui hatma kutwa kuhakikiwa mara vyeti vya vyuo,mara umri mara ndoa na kadi za benki. Gharama za maisha zimepanda mishahara haijapanda. Wanaishi kwa hofu ya kutumbuliwa.

Madiwani wanakaa vikao hawana mradi wa kujadili fesha hazijaletwa,fedha zinaletwa kwa matukio tu,na sio kwa mujibu wa bajeti. Wakurugenzi wanaogopa wamejaa uwoga wa kutumbuliwa,hawana ujasiri wa kukumbushia ruzuku.
Wabunge wetu mnafanya kazi gani?nyinyi ndio mawakala wetu kwa mawaziri na rais, mbona mko kimya?

Nyie wabunge vipi,mlishindwa kuzuia serikali kuu kupokonya vyanzo vya mapato ya ndani na bado mmekaa kimya tu.Hii sio dalili ya nchi kufilisika?
Kuna post inaendana na hii niliweka humu ikisema"wabunge walio wengi hawasikiki kuhamasisha maendeleo,nini kimewasibu". Kama alivyosema spika majuzi" bunge letu lina takriban 75% wabunge vijana,na wengi ndo mara ya kwanza kuwa wawakilishi. Hali kadhalika kada nyingi za watawala ni watu wapya kwenye utumishi! Nafikiri kuna umuhimu wa kurudisha semina elekezi kuwapa hali halisi ya kazi na nini wanapaswa kufanya jamii isonge mbele.
 
Wanatakiwa wawe wabunifu watafute vyanzo vipya vya mapato kulingana na mazingira waliopo ila chondechonde Serikali Kuu msije mkavichukua vyanzo hivi vipya watakavyovibuni hata kama vitakuwa vinaleta mapato makubwa kama ilivyokuwa kwa Kodi ya Majengo (Property Tax).
 
Jamani Mbona kwenye Post Kama Hizi Siwaoni Akina
Wakudadavuwa,Motochin
Lizabon,Yehodaya,Stroke, Jinga Lao,

Au Hawana Hoja?

Tunakokwenda ni Kubaya Kuliko Tunakotoka Hali ni Ngumu Halmashauri zina Madeni Sana.
 
Kama hamkusanyi kodi punguzeni wafanyakazi, eti rim hizo form mbona tunatoa photocopy wenyewe? Mumepewa ada za leseni kodi za majengo, bado naruzuku mpate? Hapana kabisa. Majaliwa halmashauri itakayoshindwa kujiendesha ifute.

Tunahitaji kujenga reli mpya tuokoe barabara zetu, tunahitaji kujenga viwanda vijana wapate ajira, mwingine anataka apelekewe ruzuku apate hela ya supu na kuhudumia nyumba ndogo. Eti ukata? Kuna mwezi hukulipwa mshahara?
 
Ipo haja ya kupunguza idadi ya halmashauri, mkoloni aliendesha nchi kwa mikoa minane na wilaya chini ya ishirini tena kwa kutumia 109 na moris, leo kuna barabara za lami na mavx simu za rununu, tupunguze wilaya tuokoe pesa.

Kongo wana km 1000 tu za lami nchi kubwa mara nne ya tanzania, sisi tuna elfu 28, bado mtu haoni kazi iliyofanyika pumbaf.
 
Kuna post inaendana na hii niliweka humu ikisema"wabunge walio wengi hawasikiki kuhamasisha maendeleo,nini kimewasibu". Kama alivyosema spika majuzi" bunge letu lina takriban 75% wabunge vijana,na wengi ndo mara ya kwanza kuwa wawakilishi. Hali kadhalika kada nyingi za watawala ni watu wapya kwenye utumishi! Nafikiri kuna umuhimu wa kurudisha semina elekezi kuwapa hali halisi ya kazi na nini wanapaswa kufanya jamii isonge mbele.
Ulisoma kabla hujapost ulichoandika? Umri wa mBUNGE unahusiana nini na Serikali Kuu kupeleka Pesa za Maendeleo kwenye Harmashauri
 
1. Halmashauri hazikopesheki tena kwa wazabuni, wazabuni wanashinda halmashauri kudai pesa zao.
2. Halmashauri zinaua mitaji ya wafanyabiashara
3. Watumishi wamekataa tamaa wamepauka hawajui kesho yao,
4. (Watumishi) stahiki zao hawajui hatma kutwa kuhakikiwa mara vyeti vya vyuo,mara umri mara ndoa na kadi za benki.
5. Gharama za maisha zimepanda mishahara haijapanda. Wanaishi kwa hofu ya kutumbuliwa.

Reading 1, 2, 3, 4, 5, 6 ........
 
Huwa nawashangaa sana watu ambao wakiambiwa reality jinsi mamb yalivyo hasa yanayohusu hela wao wanabisha na kukejeli kwa misemo ya "fanyeni kazi",nachukia sana hii tabia ya watu kujitoa ufahamu na kuweka maslahi ya chama na tumbo mbele..ni muda sasa wewe unaebisha kutafakari kama kweli unachokifanya kina tija kwa wale watanzania wanaoishi mikoa mingine na hata usiowajua..usiongee kwa kufikiri kuwa tanzania ni lile enwi mnaloishi na hivyo huakisi nchi nzima...panua fikra zako na kuwafikiria wengine then ndo utajua utumbo ambao kila siku unakesha kuitetea humu!!!!!
 
Back
Top Bottom