Halmashauri zetu na mustakabali wake

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Wapendwa, Salaam aleikum;

Naanza kwa kuhoji: 1. Ni wangapi kati yetu sisi tunaochangia humu tuna shiriki katika masuala yanayohusu Halmashauri na seikali zetu za mitaa huko tunakotoka?

2. Ni wangapi kati yetu tunaofahamu walau kwa kiwango kidogo uendeshaji wa Halmashauri zetu Tanzania?

Hivi karibuni Mhe. Dr. Lyatonga Mrema na Kamati anayoiongoza ya Hesabu za S/Mitaa alitoa maoni ambayo yametustua wengi na kutusikitisha haswa pale alipobainisha mwenendo unaoonyesha kutokuwepo kwa uadilifu na umakini katika utendaji wa taasisi hizi za serikali.

Kwa kuwa kazi za Kamati ni ya usimamizi na ufuatiliaji pengine ingekuwa vema pia kama Mhe Dr. huyo angeeleza pia yale ambayo Halmashauri hizo zimeweza kuyafanikisha na aidha Kamati hii ingepata credit zaidi kama ingefuatilia na kubaini sababu za udhaifu ambao imeutangaza kwa umma.

La msingi hapa ni kwamba picha inayojitokeza inaelekea kuegemea zaidi kwenye kuzinyooshea vidole Halmashauri hizi na kuzibebesha lawama kwa mengi ambayo Wa-Tanzania tunayaona kama ni kunyimwa haki ya kikatiba ya kupata maendeleo kupitia vyombo hivi vilivyowekwa na Katiba.

Nataka niwajuze kwamba Halmashauri hizi, kwa utaratibu wa nchi hii zimepewa dhamana kubwa ya kusimamia upatikanaji wa huduma za umma katika maeneo zinamofanya kazi. Je maoni kama haya ya Mhe Dr. na Kamati yake yanatuonyesha lipi? Kwamba zimeshindwa kutekeleza majukumu zilizopewa?

Historia inatueleza kuwa mafanikio ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii yamepatikana kupitia mfumo imara wa serikali za mitaa katika nchi mbalimbali ulimwenguni- mfano Japan, England, nchi za Scandinavia, na hata Marekani.

Tuna matatizo gani Tanzania katika kupata mfumo imara kwa hili ambalo ndilo linaweza kutukomboa kutokana na mgando tulionao katika maendeleo?

Wasalaam
 
Kwa ujumla halmashauri zetu nyingi ni uozo wa ajabu, huwezi kuamini.Fedha nyingi sana zinazopelekwa kwenye halmashauri hizi zinaishia kwenye mifuko ya watendaji sio miradi, rushwa imekithiri,siasa za ovyo, uelewa mdogo wa wafanyakazi wa halmashauri,madiwani wengi mbumbumbu,halmashauri nyingi hazina vision na wakurugenzi wengi wa halmashauri sio wabunifu na hawana vision. Kweli halmashauri kama zinapata wakurugenzi wazuri wenye vision, madiwani wazuri waliosoma na wenye vision, wenyeviti na mayors wenye elimu na vision, halmashauri zingekuwa ni kitivo cha maendeleo, lakini ni balaa, zimegeuka sehemu ya watu kujineemesha.Nafikiri kuna haja ya kuangalia upya mfumo wa halmashauri zetu, na nafikiri mkurugenzi iwe nafasi ya kupigiwa kura badala ya kuteuliwa kwa kuwa ndio injini ya maendeleo ila wengi wao wapowapo tu hawana vision japo wengi wanaelimu nzuri.
 
wananchi hatupendi kushiriki ktk serikali zetu za mtaa.Jiulize lini ulitembelea ofisi yako ya mtaa/kijiji:frusty:
 
Back
Top Bottom