A
Anonymous
Guest
Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe hailipi madeni kwa sisi ambao tumefanya zabuni nao, na ukifuatilia malipo unajibiwa vibaya. Pia wamejipa majukumu ya TRA kwa kuzuia malipo endapo unadaiwa TRA, jambo ambalo ni kinyume na sheria pamoja na taratibu.
Tunaziomba mamlaka za juu kuchukua hatua kwani mitaji yetu inayumba sana. Kwa sasa hata zabuni za ujenzi tunaogopa kuchukua maana tumeshaathirika sana, kiasi kwamba unaingia kwenye kazi ukiwa tayari unajua unakwenda kuzima mtaji wako.
Zaidi ya milioni 20 nimezungushwa huku na kule kama kifaranga asiye na mama, huku nikitumia gharama kubwa kufuatilia malipo yangu.