Halmashauri ya Jiji la Arusha chini ya CHADEMA yatoa mikopo ya 624mil kwa wanawake na vijana

Mbona mnatuchanganya???

huu ni mkopo wa 16/17 au 15/16???
Je hamjatafuta data za kiasi kilichotolewa na CCM katika taarifa za awali za jiji ??

Dont fool us with cheap popularity scams
Kawaulize dodoma huko habar za ccm
 
Kuna sehemu hii taarifa ikitanabaisha kuwa Mkuu wa mkoa Mrisho gambo ndiye katoa hii mikopo kumbe walikuwa washaigeuza hii taarifa duh !!
 
Dr:Wilbrod Slaa
Propaganda haziwafikishi mbali. Msemakweli ni Mpenzi wa Mungu.

1) Nimekuwa Mbunge Miaka 15. Ninafahamu msingi 10% ya Mapato ya Halmashauri kutolewa kwa Mikopo kwa Wanawake na Vijana. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa haihusiki kwa lolote. Mkuu wa Mkoa hupewa katika Bajet ya Mkoa Tshs 10 Million kusaidia Miradi ya Wananchi pale anapokuwa Ziara mbalimbali. Mamilioni yanayosemwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa ni uwongo na upotoshaji uliokithiri.

2) Fedha za Mikopo kwa Makundi ya Wanawake na Bijana ni Rebolving Fund, ambayo inasimamiwa na Halmashauri husika. Mchakato, tangu kuchambua, kuwapa elimu, kuwafuatilia hadi fedha kurudishwa ni kazi ya Halmashauri husika kupitia idara husika ya Halmashauri. Mkuu wa Mkoa hahusiki. Ni uwehunkuingiza siasa mahali pasipostahili kwa kuwa matokeo yake ni kufanya hizo fedha zisiweze kurudishwa. Nimekutana sana na matukio ya aina hiyo wakati nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa. Aidha Halmashsuri ambazo nazo zilikuwa hazitengi fedha hizo asilimia 10% Watendaji wake tulikuwa tukiwapiga wao wenyewe Faini. Hivyo Mrisho Gambo asiwapotoshe Watanzania. Vita vyake na Lema isije ikaathiri utendaji kazi wa mifumo ya Serikali iliyowekwa siku nyingi. Mpango huo wa kuxitaka Halmashauri kutenga fedha ulianza Wakati Kingunge Ngombale Mwiru akiwa Waziri wa TAMISEMI. Propaganda anazofanya Mridho Gambo ni za kitoto sana, nsomba radhi lakini bahati mbaya katika nchi hii ninajua mengi, na hakuna wa kunidanganya. Hivyo, mbuyu uitwe tu mbuyu. Huu mchezo anaofanya Mrisho Gumbo ndio unaozidi kupandisha watu hasira kama alivyotaka kufanya wakati wa Kituo cha Afya cha Mama na Mtoto.

3) Meya, sikutetei iwa kuwa ni Halmashauri ya Chadema. Ninasimamia ukweli. Wananchi wa Arusha sio wote wa Chadema. Hata wasio Chadema wanahaki na fedha hizo kwa kuwa wote walipiga kura na hivyo wote wana haki ya kunufaika na kura zao. Meya, chapa kaxi bila ubaguzi wa aina yeyote. Simamia ukweli, simama penye haki, Mungu. Atavatiki, lakini usikubali laana ya ubaguzi kwa kuwa unashindana na huyo ambaye hajui mipaka yake ya kazi.
4) Fedha 10% za Halmashauri zinaongezewa pia fedha kutoka Hazina kupitia kinachoitwa " Fidia ya Vyanzo vya usumbufu". Hizo ndizo nadhani Mrisho Mgambo anaziita fedha za TAMISEMI. Wizara ya Tamisemi kama mdimamizi wa Serikali za Mitaa, ni daraja tu, lakini fedha za Fidia zinaidhinishwa na Bunge la JMT kwa lengo la kuxirudishia Halmashauri fedha kutoka vyanzo ambavyo 2002 vilichukuliwa na Serikali Kuu. Ninavyoelewa hakuna utaratibu mwingine uliofanyika. Hivyo hizo fefha ni kodi ya Watanzana wote na Mrisho Gambo hana haki ya kuzifanyia Propaganda.

Manispa ya Arusha tembeeni kifua mbele kutimiza ahadi yenu, na ninaziomba mamla zote za Halmashauri zitimise ahadi zao ili Watanzania wote bila kujali itikadi zao wanufaike. Mungu Ibariki Tanzania. Mungu wabariki Wanyofu wa moyo wanaotekeleza majukumu yao kwa kadiri ya mapenzi yako na siyo matakwa binafsi ya mtu mmoja mmoja.Arusha mnanibariki sana
 
mwenzenu mlisho gambe katanagaza nakakwamba yy ndio alitafuta hzo pesa kwa juhudi zake msibaaaa
 
Rc Gambo amekabidhi hundi kwa Vikundi 125 kwa Vikundi vya Wanawake na Vijana

Mikopo hii inatolewa na Halmashauri kwa Mujibu wa Sheria na Utekelezaji wa Ilani lengo ni kuwainua wananwake na Vijana.

Sheria inaelekeza asilimia kumi ya Mapato ya Ndani itolewe Kama Mikopo kwa makundi hayo kwa riba ya asilimia 10 tu.

Hivyo Jiji la Arusha limetoa Tsh Mil 624 kwa kipindi cha Robo ya kwanza na Pili kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.


Utoaji wa Mikopo hiyo Sambamba na Mafunzo yametolewa Leo kwenye Ukumbi wa Arusha Sec na Mgeni Rasmi ambaye ndiye aliyekabidhi Hundi ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo


Hakika sio Jambo Rahis baada ya kuminya Mianya yote ya posho holela walizokuwa wanajilipa. Madiwani wa Jiji fedha za Mikopo zimepatikana

UPU.MBA.VU at its Best Level! Nyote mnafanana! Mbona hajaenda kukabidhi Meru? Yeye si mkuu wa Mkoa? Au ni WA WILAYA? Ku force umaarufu Ni Upuu.zi WA mwisho! Kuwa na kijana mjinga hivi ni hasara. Arusha hawadanganyiki!!!!!! Yeye SII sehemu ya Halmashauri, Ni kama kapewa lifti kaanza kupiga na honi! Hana Mamlaka na fedha za Halmashauri!Period!
 
Hivi wewe haujaguswa na suala la kupotea kwa BEN maana kila siku uNaleta umbeya humu....Ili hali msaidizi wa Mkuu wako ajulikani alipo...EBU SAIDIENI KUPAZA SAUTI HUYU KIJANA AONEKANE......
Huna cha cha ku comment kaa kimya au nenda au nenda huko fb
 
Haya ndio mambo sasa tunayotaka kuyasikia.....

Hongera sana Meya wa Arusha na madiwani wote ...............

Mashindano yawe ya Maendeleo

Chadema mna fedha zipi??....mna ilani ipi inayotekelezwa??hebu acheni sanaa zenu kuwahadaa wananchi
 
Halimashauri ya jiji la Arusha imetoa jumla ya Tshs 624,000,000,00(624mil).Kati ya hizo 425mil kwa ajili ya wanawake na 199,mil kwa ajili ya Vijana.Hii ni awamu ya pili kwa Halmashauri kutoa mikopo kwa ajili ya vikundi mbalimbali.Mara ya kwanza jumla ya 405mil zilitolewa,hivyo jumla ya 1.24bil zimetolewa tangu Halmashauri hii iwe chini ya CHADEMA na hivyo kufanya halmashauri ya jiji la Arusha kuwa Halimashauri ya kwanza nchini tangu uhuru kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake.

Mikopo hii ambayo ni mapato ya ndani ya Halmashauri ambayo ni zaidi ya 1bil kila mwezi,sambamba na hilo Halmashauri imetoa mafunzo maalum kwa ajili ya matumizi bora ya fedha hizo.

Bado Halmashauri itaendelea kutoa mikopo hii kwa wananchi wote wa Jiji la Arusha.Natoa rai kwa wananchi wote kuunda vikundi ili waweze kufaidika na mikopo hii.

Hongera wananchi wa Arusha
Hongera Meya
Hongera madiwani wote
View attachment 453392 View attachment 453393 View attachment 453394
Mbona hii misaada haifikii walengwa husika nasikia tu bilioni .milioni na shida ziko pale pale
 
So technically hiyo mikopo ni kwaajiri ya wanawake.... Maana kama umetenga 400+milion kwaajiri ya wanawake halafu useme 199milion ni kwaajiri ya vijana, je katika hao vijana wanawake hawezi kuwa vijana.....?!

Ha ha ha ha ha aiseeee so now tumefikia hapa.... So technically hata ofisi za serikali zimeanza kupractice "Male economic incarceration"?!

Dah tunasafari ndefu sana..... Jinamizi la black Americans linaanza kuja Africa.....
 
Back
Top Bottom