Halmashauri ya Jiji la Arusha chini ya CHADEMA yatoa mikopo ya 624mil kwa wanawake na vijana

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Halimashauri ya jiji la Arusha imetoa jumla ya Tshs 624,000,000,00(624mil).Kati ya hizo 425mil kwa ajili ya wanawake na 199,mil kwa ajili ya Vijana.Hii ni awamu ya pili kwa Halmashauri kutoa mikopo kwa ajili ya vikundi mbalimbali.Mara ya kwanza jumla ya 405mil zilitolewa,hivyo jumla ya 1.24bil zimetolewa tangu Halmashauri hii iwe chini ya CHADEMA na hivyo kufanya halmashauri ya jiji la Arusha kuwa Halimashauri ya kwanza nchini tangu uhuru kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake.

Mikopo hii ambayo ni mapato ya ndani ya Halmashauri ambayo ni zaidi ya 1bil kila mwezi,sambamba na hilo Halmashauri imetoa mafunzo maalum kwa ajili ya matumizi bora ya fedha hizo.

Bado Halmashauri itaendelea kutoa mikopo hii kwa wananchi wote wa Jiji la Arusha.Natoa rai kwa wananchi wote kuunda vikundi ili waweze kufaidika na mikopo hii.

Hongera wananchi wa Arusha
Hongera Meya
Hongera madiwani wote
IMG-20170102-WA0035.jpg
IMG-20170102-WA0034.jpg
IMG-20170102-WA0037.jpg
 
Hivi wewe haujaguswa na suala la kupotea kwa BEN maana kila siku uNaleta umbeya humu....Ili hali msaidizi wa Mkuu wako ajulikani alipo...EBU SAIDIENI KUPAZA SAUTI HUYU KIJANA AONEKANE......
 
Halimashauri ya jiji la Arusha imetoa jumla ya Tshs 624,000,000,00(624mil).Kati ya hizo 425mil kwa ajili ya wanawake na 199,mil kwa ajili ya Vijana.Hii ni awamu ya pili kwa Halmashauri kutoa mikopo kwa ajili ya vikundi mbalimbali.Mara ya kwanza jumla ya 405mil zilitolewa,hivyo jumla ya 1.24bil zimetolewa tangu Halmashauri hii iwe chini ya CHADEMA na hivyo kufanya halmashauri ya jiji la Arusha kuwa Halimashauri ya kwanza nchini tangu uhuru kutoa mikopo kwa vikundi vya vijana na wanawake.

Mikopo hii ambayo ni mapato ya ndani ya Halmashauri ambayo ni zaidi ya 1bil kila mwezi,sambamba na hilo Halmashauri imetoa mafunzo maalum kwa ajili ya matumizi bora ya fedha hizo.

Bado Halmashauri itaendelea kutoa mikopo hii kwa wananchi wote wa Jiji la Arusha.Natoa rai kwa wananchi wote kuunda vikundi ili waweze kufaidika na mikopo hii.

Hongera wananchi wa Arusha
Hongera Meya
Hongera madiwani wote

Weka na za mikoa mingine Wacha ushabiki? Vile vile weka takwimu hao waliopata wanazitumia vipi na mechanism ya kuangalia kama hazitolewi kwa upendeleo nk. kama ubunge wa viti maalum nk.
 
Habari inahusu Arusha!! Hiyo mikoa mingine anzishia hoja yake, yaani ni kama mtu kaandika kuhusu uchaguzi wa marekani halafu umwambie aandike na nchi nyingine! Mbona matatizo ya akili yanaongezeka kwa kasi hivi hapa nchini? Au maisha magumu?
 
Sio mikoa mingine tu, weka habari iliyoshiba. Hayo mengine Je?
 
Hebu weka taarifa yako vizuri usiongeze mbwembwe ukawaponza watu bure.

Kawaida ni kwamba asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri hutakiwa kwenda kukopesha vikundi vya kina mama na watoto.

Sasa hebu tutajie mapato ya jiji la Arusha kwa kipindi cha miaka miwili toka chadema iwe madarakani na utuonyeshe asilimia kumi yake ni kiasi gani halafu tulinganishe na hiko kiasi cha mikopo mlichokitoa kama ni sahihi au la....

Kama ni kidogo basi Mtuambie kingine kimeenda wapi.

Kama ni kingi basi mtueleze mmefuta miradi gani?

Pili ni vyema mkatuwekea list ya majina ya vikindi vilivyokopeshwa....isije ikawa ni vikundi vya madiwani!
 
Kutoa sawa, ishu itakuja kwenye urejeshaji wa mikopo hiyo. Mbaya zaidi ukute moja ya wanufaika ni hao hao madiwani kupitia mgongo wa vijana na akina mama.
 
Hebu weka taarifa yako vizuri usiongeze mbwembwe ukawaponza watu bure.

Kawaida ni kwamba asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri hutakiwa kwenda kukopesha vikundi vya kina mama na watoto.

Sasa hebu tutajie mapato ya jiji la Arusha kwa kipindi cha miaka miwili toka chadema iwe madarakani na utuonyeshe asilimia kumi yake ni kiasi gani halafu tulinganishe na hiko kiasi cha mikopo mlichokitoa kama ni sahihi au la....

Kama ni kidogo basi Mtuambie kingine kimeenda wapi.

Kama ni kingi basi mtueleze mmefuta miradi gani?

Pili ni vyema mkatuwekea list ya majina ya vikindi vilivyokopeshwa....isije ikawa ni vikundi vya madiwani!
Mikoa mingine ambayo manispaa/halmashauri zake ziko chini ya ccm wameweza kufanya hayo yaliyofanywa Arusha??
Tupe takwimu za Dodoma,..
Siyo utoe udenda kama kuku mwenye mdondo!!
 
Weka na za mikoa mingine Wacha ushabiki? Vile vile weka takwimu hao waliopata wanazitumia vipi na mechanism ya kuangalia kama hazitolewi kwa upendeleo nk. kama ubunge wa viti maalum nk.
Mbona habari inaeleweka kabisa? Acha wivu kama Mrisho Gambolela
 
Habari inahusu Arusha!! Hiyo mikoa mingine anzishia hoja yake, yaani ni kama mtu kaandika kuhusu uchaguzi wa marekani halafu umwambie aandike na nchi nyingine! Mbona matatizo ya akili yanaongezeka kwa kasi hivi hapa nchini? Au maisha magumu?
Pesa zitapotea hadi makanisani
 
Back
Top Bottom