Halmashauri ya Jiji la Arusha chini ya CHADEMA yatoa mikopo ya 624mil kwa wanawake na vijana

Hebu weka taarifa yako vizuri usiongeze mbwembwe ukawaponza watu bure.

Kawaida ni kwamba asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri hutakiwa kwenda kukopesha vikundi vya kina mama na watoto.

Sasa hebu tutajie mapato ya jiji la Arusha kwa kipindi cha miaka miwili toka chadema iwe madarakani na utuonyeshe asilimia kumi yake ni kiasi gani halafu tulinganishe na hiko kiasi cha mikopo mlichokitoa kama ni sahihi au la....

Kama ni kidogo basi Mtuambie kingine kimeenda wapi.

Kama ni kingi basi mtueleze mmefuta miradi gani?

Pili ni vyema mkatuwekea list ya majina ya vikindi vilivyokopeshwa....isije ikawa ni vikundi vya madiwani!
Imekuuma sababu CCM alikuwa mnagawana wake wa Mawaziri na watoto wao
 
Ha ha ha ....mbona huongelei takwa la kikanuni kuhusu 10% ya own source ni kwa ajili ya mikopo?
Hebu ulizia Meru,Karatu,Kigoma,Hai kwa mwenyekiti n.k kama hawajatoa hizo fedha.
N.B hata kwa mwenyekiti wako ni lazima watekeleze ilani ya CCM....
Ingawa ninyi mlikuwa na wazo hili hapa chini....
Madiwani wa CHADEMA Arusha sasa katika kashfa ya posho – Raia Mwema

Naona mnajifurahisha.Check za mkopo zimetolewa.na Halmashauri chini ya CDM. Walianza na Kinondoni, Leo Arusha kazi.ya Gambo ni kuweka watu jela,a subiri kuweka watu jela
 
Mbona mnatuchanganya???

huu ni mkopo wa 16/17 au 15/16???
Je hamjatafuta data za kiasi kilichotolewa na CCM katika taarifa za awali za jiji ??

Dont fool us with cheap popularity scams
Umeambiwa 16/17 hiyo 15/16 ni yakwako
 
Wamepewa kina mama wangapi wa kata gani? Pamoja na vijana wa wapi? Na utaratibu wa kupata hiyo mikopo ni vipi kama sivyo usanii tu.
Haya maswali nenda ofisini kwa Mkurugenzi Athumani Kihamia ukaulize usituchoshe Hapa.
 
Wewe inaonekana na Mgambo wako mlikimbilia laana zite za shetani. Sasa hela zitolewe na halmashauri tena useme Mkuu wa mkoa katoa? Ama kweli kwa Arusha ccm mnajikojolea mwambie Gambo atafute hela kama ofisi yake ina fungu halafu awagawie maccm wenzie kisha akutume ulete uhalo wenu hapa. Lakini kama ni hii ya halmashauri Gambo hausiki bali kama ni kuwakabidhi hapo kaitwa tu na halmashauri tena kwa dharau kubwa kumuonyesha ni jinsi gani Chadema kwa Arusha inatekeleza budget yake na ili 2020 kwenye campaign pindi Gambo anagombea ubunge ccm na huku Lema anagombea kupitia chadema pasiwepo usumbufu. Lema atakuwa anasema tumekusanya mapato ya kutosha na kutoa mikopo kwa wajasiriamali. Na shahidi ni Gambo ndiye alikuja kutusaidia kuzitoa kwa wajasiriamali. Na kule Gambo atakuwa anasema nipeni kura na madiwani wa kutosha wa ccm ili tuirudishe Arusha kama zamani hakuna kukusanya mapato wala kutoa mkopo kila mtu atafute mtaji wake ccm haijawaambia muwe masikini.
 
Fedha hizi zinatolewa kwa Mujibu wa Sheria na Riba yake ni asilimia kumi tu Hakuna zaidi lengo sio kufanya biashara Bali kusaidia Wananchi
Ukiisha weka riba maanayake ni biashara. Tofautisha kati ya Msaada na mkopo wenye riba. Huu sio msaada. Ndyo maana waliopewa ni wenyevigezo vya kurudisha pekee
 
Halmashauri ikusanye fedha na kupanga vikundi vya kupewa fedha kisha anaitwa mkuu wa mkoa kugawa katika sherehe hizo basi tayari yeye ndio katoa fedha hizo? Nimepata mantiki ya Lema kutaka kumcharaza makofi pale kwenye kuweka jiwe la msingi la hospitali.
 
Hebu weka taarifa yako vizuri usiongeze mbwembwe ukawaponza watu bure.

Kawaida ni kwamba asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri hutakiwa kwenda kukopesha vikundi vya kina mama na watoto.

Sasa hebu tutajie mapato ya jiji la Arusha kwa kipindi cha miaka miwili toka chadema iwe madarakani na utuonyeshe asilimia kumi yake ni kiasi gani halafu tulinganishe na hiko kiasi cha mikopo mlichokitoa kama ni sahihi au la....

Kama ni kidogo basi Mtuambie kingine kimeenda wapi.

Kama ni kingi basi mtueleze mmefuta miradi gani?

Pili ni vyema mkatuwekea list ya majina ya vikindi vilivyokopeshwa....isije ikawa ni vikundi vya madiwani!
Acha hizo bana kwan zile pikpik zilizogawiwa majina yaliletwa hum?
 
Rc Gambo amekabidhi hundi kwa Vikundi 125 kwa Vikundi vya Wanawake na Vijana

Mikopo hii inatolewa na Halmashauri kwa Mujibu wa Sheria na Utekelezaji wa Ilani lengo ni kuwainua wananwake na Vijana.

Sheria inaelekeza asilimia kumi ya Mapato ya Ndani itolewe Kama Mikopo kwa makundi hayo kwa riba ya asilimia 10 tu.

Hivyo Jiji la Arusha limetoa Tsh Mil 624 kwa kipindi cha Robo ya kwanza na Pili kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.


Utoaji wa Mikopo hiyo Sambamba na Mafunzo yametolewa Leo kwenye Ukumbi wa Arusha Sec na Mgeni Rasmi ambaye ndiye aliyekabidhi Hundi ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo


Hakika sio Jambo Rahis baada ya kuminya Mianya yote ya posho holela walizokuwa wanajilipa. Madiwani wa Jiji fedha za Mikopo zimepatikana

Mkuu huyu Ana kazi sana.

Hivi Gambo katika hali Ya kawaida una hizi
Pesa? Acheni kudanganya watu. Mashindano ya nnini? Tunajua kazi Ya chadema arusha na si wewe unayetumia nguvu kubwa kuonekana kwenye media. Arusha for Chadema Arusha for God bless Jonathan Lema
 
Tatizo wananchi tunaona chadema ndo wameleta pikipiki chadema ndo wameleta mikopo..ccm wamekula hela zetu..chezea machalii wa chuga tutakaza ivyo ivyo mpaka mtujengee uwanja wa bombadier
 
give credit where credit is due,

so long,amewapa unafuu kikundi fulani,

then,ana pongezi zangu za dhati.
 
Back
Top Bottom