Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,038
- 2,199
Maono yangu miaka mi5 ijayo:halmashauri zilizoleta mabadiliko na kutwaliwa na chadema zijiandae kufunga mkanda kwani iwapo CCM itashika dola basi ni wazi itatumia mbinu zote chafu ili kuonyesha upinzani ni dhaifu.ni wazi kuwa CCM imepata pigo kupoteza majimbo yenye ushawishi ktk kila hali especially uchumi na siasa ktk Tanzania na EAC kwa ujumla.kwa CCM ,kuachia majimbo haya yafanikiwe ni sawa na kusign death certificate kabla ya 2015.tutegemee kuona msaada kutoka central goverment ukipungua,msuguano kati ya pande hizi mbili kuwa mkubwa.mfano wa haya nisemayo upo;ni hivi karibuni nchini uganda wameamua kurudisha mamlaka za majiji chini ya serikali kuu.kulikua na msuguano mkali kati pande hizi mbili kwa sababu KCC(KAMPALA CITY COUNCIL) iko chini ya upinzani.hivyo maoni yangu kwa wananchi na viongozi wa sehemu husika wawe tayari kwa challenge hii inayokuja,watahitaji 'kufunga mkanda' kupambana ,kuwa majasiri zaidi,wavumilivu na wabunifu ili kujiletea maendeleo yao wakiwa huru dhidi ya makucha ya mafedhuli na mafisadi."mapambano ya kuikomboa Tanganyika(zanzibar ni nchi huru) ndio yameanza.umahiri waliounyesha na watakaonyesha kwa kipindi kijacho cha 5yrs utakuwa ni chachu ya mabadiliko kwa taifa hili.VIVA! ARUSHA ,MBEYA MWANZA.....mapambano yaendelee mpaka kieleweke.naomba kuwasilisha!