Halima Mdee na wenzake wapinga kuhojiwa na Wakili Kibatala, wadai wao ndio Wana haki ya kuihoji CHADEMA

Wakili wa Halima Mdee na wenzake amesema kisheria wateja wake 19 ndio wameishtaki Chadema na kwa sababu hiyo wa

o ndio Wana haki ya kuihoji Chadema Siyo kuhojiwa

Kesi umeahirishwa hadi Ijumaa ijayo na Jaji amewataka akina Halima Mdee na wenzake wasije mahakamani hadi watakapoambiwa baada ya pingamizi kuamuliwa.

Chanzo: ITV

Pia soma - Mdee na Wenzake wawasili mahakamani kwa ajili ya usikilizwaji wa shauri lao
Hivi kuna mtu yeyote jasiri ambaye anakubali kuhojiwa na Kibatala
 
Yaani tukiangalia uchaguzi wa Kenya na siasa za Tanzania inatia huruma!
Ni kweli maana makabila mawili tu makubwa kenya ndio yanaweza kuwapatika wakenya Rais.Tuwaige kabisa wako vizuri
 
Ni kweli maana makabila mawili tu makubwa kenya ndio yanaweza kuwapatika wakenya Rais.Tuwaige kabisa wako vizuri

Unajua kabila la Ruto kama ni kubwa! au una ropoka tu. Ukisingizia mgombea mwenza je kwanini sisi mgombea mwenza lazima atoke zanzibar!

Wametuzidi sana kwenye demokrasia sisi uchaguzi wa 2020 mashirika yaleyale ya waangalizi walisema uchaguzi sio huru lakini kenya mpaka kikwete kakubali kwamba hajawahi kuona uchaguzi wa uwazi vile. Sasa unataka kusema kikwete kadanganya au
 
2025 ndiyo watatoka bungeni.Watakaua washaaandaliwa mazingira ya vua gwanda,vaa gamba la kijani,wanapewa vyeo,wanatulia.
Lakini tutakuwa tumeshawafamu kama tulivyomfahamu yule polisi kuwa ni debe tupu kwa pgo
 
Hiyo kesi ina maslahi na serikali, na kesi yoyote yenye maslahi na serikali hasa ya kisiasa dhidi ya wapinzani, tegemea mizengwe tu huko mahakamani ili kupoteza muda. Kesi ya uchaguzi wa urais hapo Kenya itaendeshwa haraka na uamuzi utatolewa, huku ya kina Mdee ikiendelea kupotezea wetu muda. Anayetegemea maamuzi yaliyo kinyume na matakwa ya serikali kwenye hizi mahakama kibogoyo anapoteza muda wake.
Si kupoteza muda tu. Itapoteza na pesa nyingi za walipa tozo
 
Hiyo kesi ina maslahi na serikali, na kesi yoyote yenye maslahi na serikali hasa ya kisiasa dhidi ya wapinzani, tegemea mizengwe tu huko mahakamani ili kupoteza muda. Kesi ya uchaguzi wa urais hapo Kenya itaendeshwa haraka na uamuzi utatolewa, huku ya kina Mdee ikiendelea kupotezea wetu muda. Anayetegemea maamuzi yaliyo kinyume na matakwa ya serikali kwenye hizi mahakama kibogoyo anapoteza muda wake.
Kuna kitchen cabinet inaendesha hii kesi. Awali hitaji la kuwahoji Halima na wenzake lilikubalika bila pingamizi. Kitchen cabinet baada ya kutafakari ikaona huko ni kubaya na sasa wamekuja na sarakasi hii hii. Bila shaka maandalizi yote yamefanyika kabla ya kuleta sarakasi hii. Unajisi wa mahakama unaendelea.
 
Sioni jipya lolote kwenye hiyo kesi maana hatuna mahakama huru.
 
Back
Top Bottom