Halima Mdee: Kuna dhamira ya kutaka kumfunga Sugu

Halima Mdee: Kuna dhamira ya kutaka kumfunga Sugu

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,450
Reaction score
32,290
Mbunge wa jimbo la Kawe (CHADEMA) Mhe. Halima Mdee amefunguka na kumuomba Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma kufuatilia mwenendo wa kesi za kisiasa nchini na kudai kuwa baadhi ya mahakimu wamekuwa wakipindisha mambo kwa sababu za kisiasa.




halima%20mdee.jpg

Halima Mdee amesema hayo wakati akiongea na www.eatv.tv na kusema kuwaa Jaji Mkuu anaposema wanasiasa wasiingilie Mahakama hivyo na yeye anapaswa kusimama na kuhakikisha kuwa Mahakimu wakitenda haki na kukemea wale ambao kwa makusudi wamekuwa wakipindisha haki za watu.

"Ni zaidi ya wiki sasa Mhe. Sugu yupo ndani lakini amenyimwa dhamana kwa kosa ambalo linadhaminika kisheria na kiutaratibu kwa muhibu wa sheria zetu kama kosa linadhaminika ni wajibu wa polisi kutoa dhamana na polisi wakikushikilia ndani ya zile saa 48 wakikupeleka mahakamani ni jukumu la Mahakama kufanya hivyo sasa suala la Sugu limeenda Mahakamani ambapo huo ndiyo muhimili pekee ambao tunautegemea . Sasa unapokwenda Mahakamani sehemu pekee ambayo unaitegemea kupata haki halafu unaona hiyo haki haipatikani kwa makusudi kabisa hivyo Jaji Mkuu na yeye anapaswa kuyatambua haya na kuwakemea baadhi ya Mahakimu ambao wanafanya vitu kama hivi" alisema Mdee

Mbali na hilo Halima Mdee amedai kuwa kuna tetesi za kutaka kumfunga Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi “Sugu' kama ambavyo alifungwa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali
 
Tumia akili kidogo wajinga wengi ni mtaji wa ccm hili sio jukwaa la mahusiano.
Sasa kama ni ujinga kihere here gani kilichokufanya kudandia!Nyie ni mtaji wa CDM endeleeni kutumika,Hizo mahakama anazozisemea huyu zikiwapa haki nyinyi zinakuwa zinatenda haki ila zikitenda haki kwa upande wa serikali mahakama zinaingiliwa lini mtaachaga tabia za kindumilakuwili!
 
Mbunge ambaye anaoneka wazi kuwa hawezi kununuliwa akiingia kwenye 18 asipewe dhamana na akanyee ndoo.
Na hakimu atakayempa dhamana ajue hana kazi!!!.
 
Sasa kama ni ujinga kihere here gani kilichokufanya kudandia!Makarai ni mtaji wa CDM endeleeni kutumika kama kondom,Hizo mahakama anazozisemea huyu mume wa naniliu zikiwapa haki nyinyi zinakuwa zinatenda haki ila zikitenda haki kwa upande wa serikali mahakama zinaingiliwa lini mtaachaga tabia za kindumilakuwili!

Nisingependa kujikita zaidi kwenye lugha za makondom na makarai lugha za mkapa na yule dogo za kuwalaghai wafuasi wa ccm


Kesi ya msukuma alipoenda kuleta fujo mgodini na kuhamasisha raia kuzuia shughuli za uzalishaji kule ipo?
 
Yaani akiachwa huru hii tabia ya wabunge kujiona wako juu ya Sheria haitakoma, halima mdee tulia dawa iwaingie hii Nchi kwa sasa iko huru sio zama za kikwete matusi ya wanasiasa hayakuwa sehemu ya kosa.

Kwa usawa wa Magu Sheria lazima ifanye kazi, kwa hiyo acha pupa na kuingilia muhimili wa Mahakama wacha ufanye kazi yake .
 
Back
Top Bottom