Halima Mdee: Hongo haitazuia mabadiliko 2010!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halima Mdee: Hongo haitazuia mabadiliko 2010!!!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by minda, Sep 28, 2010.

 1. minda

  minda JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  Tuesday, 28 September 2010 04:36  Na Tumaini Makene

  [​IMG]
  MGOMBEA ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bi. Halima Mdee amesema zama za wananchi kufanya mabadiliko ya uongozi zimefika na hazitazuiliwa na mgombea au chama chochote kwa nguvu za hongo.


  Amesema kuwa katika uchaguzi wa mwaka huu Watanzania maskini waliochoshwa na uongozi mbovu usiojali maslahi ya wananchi, watakwenda kupiga kura za kimapinduzi, bila kujali hongo wanazopewa na baadhi ya wagombea wa vyama mbalimbali wanaosaka madaraka.

  Bi. Mdee aliyasema hayo juzi katika mfululizo wa mikutano yake ya kampeni akiomba ridhaa ya wananchi kuwa mbunge wa Jimbo la Kawe, jijini Dar es Salaam.

  Alisema kuwa kama ambavyo imekuwa ikitokea miaka ya nyuma wakati wa uchaguzi, mwaka huu pia wamejitokeza wagombea na vyama vinavyotumia nguvu ya fedha kuwarubuni na kuwanunua wapiga kura, hivyo akawataka wananchi kutorudia makosa ya nyuma.

  "Watanzania uchaguzi wa mwaka huu ni uchaguzi wa aina yake, ni uchaguzi ambao tunapaswa kupeleka salamu kwa watawala wa sasa wa CCM na wengine kuwa maskini wa Tanzania tuliopigika tunaweza kuamua kufanya mabadiliko dhidi ya matajiri wachache.

  "Wanatumia wakati huu kuwahonga wananchi ili wapate kura, wachukue nafasi kujineemesha wenyewe huku wananchi walio wengi wakizidi kuwa maskini. Tunatuma ujumbe mzito, mwaka huu maskini wataamua mustakabali wa nchi dhidi ya matajiri kupitia sanduku la kura.

  "Hatutaki kura za huruma, msipige kura za kutuhurumia, pigeni kura za kimapinduzi. Tunataka mabadiliko ya uongozi, tupate viongozi makini watakaoshirikiana na wananchi kusukuma gurudumu la maendeleo," alisema Bi. Mdee.

  Mgombea huyo ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu katika bunge lililopita kupitia CHADEMA, alisema anasikitishwa na hali ya jimbo hilo kuwa pamoja na kuwa liko mjini lakini liko nyuma katika miundombinu na huduma za jamii.

  Alisema anashangazwa kuwa kuna kata hazina hata zahanati, baadhi ya shule zikiwa katika hali mbaya huku baadhi ya maeneo miundombinu ya barabara ikianza kufanyiwa marekebisho yasiyo na tija wakati huu wa uchaguzi.

  "Jamani Watanzania lazima tuambizane ukweli, nanyi mmechangia kuifikisha nchi hapa ilipo kwa kukubali hongo na kuwapigia kura viongozi wabovu, sasa kama kweli wanawapenda kwa nini wasitumie fedha hizo kuwajengea walau zahanati au shule bora.

  "Nasikia sasa wanapita pita usiku wanawagawia fedha, na pilau mmeshaanza kupikiwa, angalieni sana, kuweni makini, msirudie makosa mliyowahi kufanya. Mnawachagua watu wanaenda kwanza kujilipa vile walivyowahonga, maendeleo hakuna," alisema Bi. Mdee.

  Aliwataka wananchi kujiandaa kwenda kupiga na kulinda kura Oktoba 31, ili kuachana na visingizo vya kura kuibiwa.

  mwisho.

  Source: Majira
   
 2. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Halima Mdee tunamuhitaji mjengoni tafadhali wana Kawe mpatieni kura za kutosha.
   
 3. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu mbona haulizwi alifanya nini alipokuwa mbunge wa kupewa?

  Kuongea kwa madoido na body language ya ishara za mikono hata pale isipotakiwa kama wale watangazaji wa ITV haitoshi kukufanya upate ubunge. :becky:
   
 4. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  keep it up gal.nchi inakuhitaji sana.watu wa kawe mpeni kura jamani huyu dada
   
 5. kibhopile

  kibhopile JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 1,304
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  huwa namkubali ile mbaya,yuko na akili n sexy pia,,,
   
 6. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  You rock mama; sijakusikia siku sasa unanipa wasi wasi Mbatia asije akatuharibia; wote wanatakiwa wafunikwe mbali sana akina mbatia na yule muuza sura; pigana sasa ndio muda sipo huko lakini najua wanakawe wanakuhitaji sana kipindi hiki
   
 7. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  yule yuko juu sana
   
 8. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huenda wewe ni mmoja wa wale jamaa ambao hawafuatilii yanayosemwa bungeni na kikifika kipindi hiki cha uchaguzi waanza kuuliza maswali ya aina hii! Halima ametoa changamoto kubwa bungeni katika kipindi chote tangu ateuliwe. Ni binti mdogo lakini mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza bila hofu wala kubabaika. Kama Halima ataukosa ubunge wa Kawe ni kwa sababu ya mfumo dume uliotawala fikra za watu kama wewe, kudadeki. Wapo wanaume wengi tu huenda na wewe ni mmojawao wanaoongea vibaya mno na sauti zao za kukoroma!

  Halima usife moyo dada umeonyesha ujasiri na uwezo mkubwa kushinda hao wanaume. Keep it up!
   
 9. F

  FM JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 2, 2009
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Tatizo linalomkabili huyu binti ni kutofanya kampeni za kutosha huku Kawe hasa sehemu za Mbezi Beach hajaonekana huko!! Asiwe overconfident, anatakiwa afanye kampeni za door to door asifanye masihalla hiki kibarua ni kizito!!
   
 11. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  tumtendee haki dada Halima... kama ni kutoa hoja zilizoenda shule nadhani alifanikiwa.Ni msemaji mzuri na halina ubishi hili. Kazi ya uwakilishi ni pamoja na kuwasemea wengine hata kama hajajenga zahanati wala kituo cha afya.Kumbuka viti maalum hawana jimbo kama jimbo - jimbo lao ni wananchi wote popote walipo kuendana na ajenda na swala.
   
 12. m

  mbarbaig Senior Member

  #12
  Sep 28, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  kama hujui nakusaidia moja...ila uache wivu....amesaidia kuondoa gratuity kwenye mashirika ya umma..nadhani waweza uliza ppf, gaming board na mashirika mengineyo ambayo yalikuwa yanajilipa gratuity after every end of the contract..sasa ukimaliza contract unapewa perm. ilikuwa inakula hela nyingi sana za walipa kodi...inatosha?
   
 13. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Halima Mdee: Mwanamke Chuma
   
 14. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  crap
   
 15. 1

  1954 JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2010
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 4,286
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  Jamani, huyu mtoto nampenda siku nyingi. How do I get her?
   
 16. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Color print picture yake na ingia nayo bafuni. :becky:
   
 17. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  crap
   
 18. K

  Keil JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Waulize Salum Londa na Yusuf Makamba, watakuambia Halima Mdee ni nani. Waliingia mitini kimya kimya na baadaye Spika Sitta alimaliza hiyo kashfa kwa kuficha aibu ya CCM wanavyolindana. Meya wa Manispaa ya Kinondoni na Katibu Mkuu wa CCM walipeleka malalamiko kwa Spika kwa mbwembwe kwamba Halima Mdee afute kauli kuwa Meya Londa analindwa na CCM kwa kuwa Londa amekuwa akihusika na kuuza viwanja. Mdee aligoma kufuta kauli, na kesi ilipoenda kwenye Kamati ya Bunge (Maadili), nyaraka zilizowasilishwa na Mdee ziliwavua nguo Londa na Makamba na baada ya hapo hawakupeleka tena utetezi wao. Sitta kama kawaida yake akasema Mdee hawezi kuomba radhi wala kufuta kauli na kesi imeisha.

  Mdee amehangaika sana na matatizo ya Ardhi (viwanja) na hasa viwanja vya wazi kwenye maeneo ya jimbo lake la Kawe. Londa alikuwa anauza maeneo ya wazi kama hana akili nzuri, akakumbana na mtaalam wa sheria alimlipua Bungeni, then Londa akaja juu kwamba amezushiwa. Makamba nae akalaani kwamba Mdee anaipakazia CCM kwamba inamlinda Londa. Zilipopelekwa nyaraka (miniti) za vikao vya CCM, ndipo Makamba na Londa walipoingia mitini.

  Bado una unataka kujua mengine? Kama unamchukia kwa kuwa si mwana CCM, ni bora ungekaa kimya.
   
 19. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 669
  Trophy Points: 280
  Mkuu, utetezi wako tosha kabisa bila kuongeza yaliyo kwenye red. Nadhani makala za kutosha zimetolewa na wajuzi kuhusu kazi za mbunge. Ni mafisadi tu ndio wanapenda kujidai kwa kujenga hiki na kile kwa fedha zao. Kazi aliyofanya huyu binti Bungeni kwa nafasi yake ni ya uhakika sana; inatosha kumtambulisha kwa wananchi makini.
   
 20. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #20
  Sep 29, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  I love strong ladies like her. Keep it up Halima, I am really proud of you. Kumbe wamama tunaweza kiukweliukweli!
   
Loading...