SI KWELI PreGE2025 Halima Mdee: Gwajima si Mtakatifu,2020 alibariki uhuni Kawe

SI KWELI PreGE2025 Halima Mdee: Gwajima si Mtakatifu,2020 alibariki uhuni Kawe

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Halima James Mdee (@halimamdee)
“Gwajima hapaswi kuonekana mtakatifu. Kwenye uchaguzi wa Kawe 2020 alibariki uhuni, ameawatukana viongozi na waumini wa Kanisa Katoliki hadharani, akawavunjia heshima Waislamu pia. Huyu ni mtu wa kutafuta umaarufu, si mkweli. Apuuzwe.”
Halima Vs Gwaji Aug 16.jpg
Halima Vs Gwaji 2 Aug 16.jpg
 
Tunachokijua
Halima Mdee amewahi kuwa mbunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia jimbo la Kawe na baadaye kuwa mbunge wa viti maalum kuanzia 2020-2025.

Askofu Josephat Gwajima ni Askofu mkuu wa makanisa ya ufufuo na uzima Tanzania, ambaye pia amewkuwa mbunge wa jimbo la Kawe kuanzia mwaka 2020-2025 pia ni mkjumbe wa halamshauri kuu wa kamati ya CCM.

Madai

Agosti 16, 2025 imeibuka taarifa ikiwa imeambatanishwa na baadhi ya grafiki za vyombo vya habari ikiwemo Jambo TV na Millard Ayo ikieleza kuwa Halima Mdee amesema kuwa Askofu Gwajima si mtakatifu na mwaka 2020 alibariki uhuni Kawe.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.

Kupitia utafutaji wa maneno muhimu imebainika kuwa ujumbe unaonekana kuchapishwa na Halima Mdee kupitia ukurasa wake wa X akielza kuwa Gwajima hapaswi kuonekana mtakatifu ni wa kugushi kwani haujachapishwa na Halima kupitia ukurasa wake rasmi wa X.

Hadi wakati ripoti hii inaandaliwa Agosti 16, 2025 taarifa iliyokuwa ikionekana ya mwisho kuchapishwa na Mdee kupitia ukurasa wake wa X ulikuwa ni wa Juni 25, 2025 ambapo taarifa hiyo ilikuwa ni matokeo ya Yanga dhidi ya Simba kwenye Derby ya Kariakoo. Tazama hapa.

Aidha ufuatiliaji kwa njia ya mtandao, JamiiCheck imebaini kuwa grafiki hizo hazijachapishwa na Millard Ayo wala Jambo TV na badala yake ni za kughushi. Grafiki hizo pia zimetumia mpangilio tofauti ukilinganisha na grafiki halisi.

Similar Discussions

Back
Top Bottom