kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee ametaka Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wazo na askari wake waondolewe hapo na kupelekwa watu wengine kwa madai kwamba wanalinda wahalifu na vigogo wanaomiliki mashamba makubwa katika eneo hilo na kusahau jukumu lao la kuwalinda wananchi na mali zao.
Mdee alitoa kauli hiyo juzi jioni baada ya kupokea malalamiko ya wananchi wa Kata ya Wazo waliobomolewa nyumba zao na watu wanaodaiwa kuwa mabaunsa waliokodishwa kutoka Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Alisema kituo hicho kilichangia kutokea kwa mauaji wanaodaiwa kufikia 11 baada ya kutokea mapigano kati ya wananchi na mabaunsa hao katika tukio lililotokea Aprili 7, mwaka huu.
Wakitoa malalamiko yao kwa Mbunge huyo, wananchi hao walisema siku ya tukio walitoa taarifa kwenye kituo cha Wazo lakini walijibiwa kwamba wao waende wauane na mtu atakayebakia ndiye aende kutoa taarifa kwao.
Kutokana na majibu hayo wananchi walikata tamaa na kuamua kukaa kimya na mabaunsa hao walipoanza kuvunja ndipo walipoanza kuwafukuza kwa marungu, mikuki, mapanga, mashoka na zana zingine za jadi ambapo watu 11 hadi sasa wamedaiwa kupoteza maisha.
Mbunge huyo juzi alizitembelea familia nane zilizobomolewa nyumba zao ambapo alisema mgogoro wa ardhi katika jimbo lake unachangiwa na vigogo wakubwa wa Serikali ambao wanamiliki mashamba makubwa lakini hawataki kuyaendeleza.
Kutokana na matatizo yaliyowapata wananchi kwa kuvunjiwa, Mdee aliahidi kuzisaidia familia hizo ingawa alisema yeye pekee hataweza kumaliza matatizo ya msingi yanayowakumba wakazi hao.
Alisema kama uchunguzi wa kina hautafanyika kwa lengo la kutatua migogoro ya ardhi katika jimbo lake kunaweza kujitokeza maafa makubwa kuliko haya ya sasa yaliyotokea.
Wakati huo huo aliliomba jeshi la Polisi kumuachia mwenyekiti wa mtaa wa Mivumoni, Deodatus Kamugisha aliyekamatwa na kufunguliwa jalada la mauaji.
Alisema Kamugisha hahusiki kwa kitu chochote na wala mtaa yalipotokea mauji hayo sio eneo lake na kwamba yeye angekuwa mtu wa kwanza kupongezwa kwani ndiye alikuwa wa kwanza kutoa taarifa kituo cha Kawe kwamba kuna mabaunsa wamevamia wananchi wa Nakasakwa na wanataka kuvunja nyumba.
Aliongeza kuwa kitu cha kushangaza polisi waliamua kumkamata yeye na kumfungulia jalada la mauaji kitu ambacho kinashangaza watu wanaojua mgogoro wa eneo hilo na jinsi mauji hayo yalivyotokea. Mwenyekiti huyo kwa sasa anashikiliwa na polisi katika kituo cha Mabatini Kijitonyama tangu alipokamatwa juzi asubunhi akiwa nyumbani kwake.
Wakati huo huo, Beatrice Shayo anaripoti kuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela amesema kuwa katika tukio hilo bado wanaendelea na upelelezi wao ili kubaini watu wengine waliohusika katika mauaji hayo.
Kenyela alisema mpaka sasa wanawashikilia watuhumiwa 10 na kwamba idadi hiyo itaongezeka kuwa kubwa wakati wowote.
Tunaendelea na msako wetu na lazima tuwakamate wale wote waliohusika katika sakata zima ikiwemo waliosababisha mauaji na wale madalali wote na kwamba idadi ya watuhumiwa itaongezeka kuwa kubwa kutokana na tukio hilo , alisema Kamanda Kenyela.
Kamanda Kenyella alisema majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Mwananyamala kwa sasa wamebaki watatu na wengine tayari wameruhusiwa.