Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,224
- 166,265
Binadamu ni wa ajabu kweli, alipo rudi toka India alikuja na maneno ya kutia moyo sana kuwa amebadili tabia. Kumbe pale alikuwa bado anakumbukumbu ya hospitali,sasa kasahau na kiburi juu. Mdee alistahili kumwita vile
Mbunge Halima Mdee kaomba radhi kwa kauli aliyomtolea Spika Ndugai bungeni kwenye uchaguzi wa EALA.
Huo ni mtego mkubwa sana kwa Ndugai kwani kama tabia alizoonyesha kwenye uchaguzi hataziacha matusi yale atatukanwa tena na wabunge wengine.
Ni wakati sasa naye kujiangalia jee anatenda haki au anafanya mambo yanayo stahili kuitwa tena "fala'?
Spika na naibu wake hata na wenyeviti wa Bunge wanapaswa kutenda kwa kufuata kanuni na kuondoa upendeleo ili kujiepusha na lugha za kuwadhalilisha.
Rais wetu walala hoi..
Nakubaliana na wewe bujibuji, ingawa siungi mkono hiyo k, k. Kwakuwa Sijui maanayake.Tabia za Ndugai ni za ki K, K tu.
Kupiga wenzie fimbo kisogoni
Kuipendelea CCM
Kukandamiza demokrasia etc
Hata lowasa naye kasema alishinda, sasa sijui kati ya wewe na yeye nani mkweli.
Mkuu mimi mpare!Wasukuma bana...kienglish hamjui hata kiswahili jamani....mnatia aibu sana
Mimi binafsi sishabikii matusi lakini pia siungi mkono vitendo vya viongozi wa Bunge vyakuwadhalilisha Watanzania asa wawakilishi wetu,kumbuka Bunge sio chombo cha ccm nimali ya Watanzania.Hongera Halima kwakuomba radhi ila tunamtaka na Ndugai awatake radhi wapinzani.
Mimi si mpenzi sana wa Halima Mdee, na huwa simshabikii sana maana mara nyingi yuko kisiasa zaidi kuliko kimaendeleo.
Huku Kawe ni mbunge wangu lakini HAKUNA mradi ulioanza kwa ushawishi wake, na hii ni awamu yake ya pili.
Kitendo cha Halima Mdee kuombavradhi kwa lugha isiyostahiki bungeni imenipa moyo.
Mtoto kaanza kukua kiakili!
Anaweza kuona kama ni suala dogo, lakini kitendo kinarudisha imani ya usikivu.
Sasa hata akienda wizara ya ujenzi su Halmashauri kuomba na kufuatilia mradi wa barabara atasikilizwa.
Hongera Halima.
Tabia za Ndugai ni za ki K, K tu.
Kupiga wenzie fimbo kisogoni
Kuipendelea CCM
Kukandamiza demokrasia etc
Msamaha wa Mdee hauna masharti bali sisi tunamuonya Ndugai kuwa tusi lile lilitokana na tabia yake aliyoonyesha na kuwa naye atumie nafasi hii kujirudi asije tukanwa tena na Mbunge mwingine.Hiki ndio nini tena? msamaha wenye masharti?