Halima Mdee akwaa kisiki mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Halima Mdee akwaa kisiki mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Oct 29, 2011.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee, lililokuwa likitaka hati ya madai katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka 2010 iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya (NCCR-Mageuzi), James Mbatia, ifanyiwe marekebisho kwa maelezo kuwa haina msingi wa kisheria.

  Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji John Utamwa ambaye baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili alifikia uamuzi wa kukubaliana na hoja za wakili wa mlalamikaji, Mohamedi Tibanyendela, aliyetaka pingamizi hilo litupwe na mahakama.

  Jaji Utamwa alisema kwa mujibu wa hati ya madai, mlalamikaji ameeleza malalamiko yake yote kwa mapana dhidi ya mdaiwa na maelezo hayo yanajitosheleza kumfanya mdaiwa kujibu tuhuma hizo zilizoelekezwa kwake.

  "Hivyo mahakama hii haikubaliani na pingamizi la mdaiwa anayetetewa na Wakili Edson Mbogoro anayetaka hati ya madai ifanyiwe marekebisho kwa vile hawezi kujibu baadhi ya tuhuma alizotuhumiwa nazo kwasababu zinamkera, kumtia kichefuchefu…..

  Kwa hiyo mahakama hii leo inasema tuhuma hizo hazikeri wala kutia kichefuchefu hivyo ina muamuru mdaiwa kuzijibu na inatupilia mbali pingamizi la mdaiwa," alisema Jaji Utamwa.

  Jaji Utamwa aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba mosi mwaka huu, ambapo kesi hiyo itakuja kwa ajili ya kutajwa na kuangalia muda wa jinsi ya kuendelea nayo, kwani Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 2010 inataka kesi za uchaguzi zimalizike ndani ya mwaka mmoja
  tangu zilipofunguliwa. Kesi hiyo ilifunguliwa Novemba mwaka 2010.

  Uamuzi huo unatokana na pingamizi lililowasilishwa na wakili wa Mdee, Mbogoro la kuiomba mahakama hiyo imwamuru mlalamikaji aifanyie marekebisho hati yake ya madai na kuyaondoa baadhi ya madai ambayo Novemba 25 mwaka 2010 Mbatia alifungua kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa jimbo hilo ambayo yalimtangaza Halima Mdee (CHADEMA) kuwa mshindi.

  Mbatia anadai kuwa katika mikutano ya kampeni, Mdee alimwita yeye kuwa ni fataki anayefanya mapenzi na watoto wa shule, kibaraka wa CCM na kila wiki analipwa sh milioni 80 na chama hicho, hivyo kuwataka wapiga kura wa Jimbo la Kawe wasimchague Mbatia.

  SOURCE. TANZANIA DAIMA
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  hivi Mbatia alijua lini hizi tuhuma za kashfa zimemwathiri katika uchaguzi? alipaswa kupeleka malalamiko yake kwa nec kabla ya uchaguzi na wala siyo baada ya kushindwa.......................................halafu katika kampeni hizo ni tuhuma.................hata kama kweli zilisemwa........................zilimwathiri vipi asichaguliwe.....................kwa nini hakuzijibu?
   
 3. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  sheria bwana, Hapa naona Mdee ana kesi ya kujibu kwa kueleza ni kivipi anatembea na watoto wa shule, anahogwa hizo pesa

  Kusema tu malalamiko mengine yanamletea kichefuchefu ni hoja nyepesi kwenye maswali magumu na sababu ya kupoteza muda-
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kwani kupanda nao gari sio kutembea nao??? i would vote for kutembea as kutembea na sio kufanya mapenzi.... na milioni themanini ndio issue
   
 5. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,068
  Likes Received: 7,539
  Trophy Points: 280
  I think before we shift the problem, is also well to wonder that " Wasn't Halima( The Respondent) aware that these kind of accusations/statements would affect her in the future?
  About how did those statements affect the complainant and if they had any impact on his failure, thats just a game of chance, and we have a lesson to learn out of that.
   
 6. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kuna hatari Halima Mdee, mbunge wa jimbo langu kupoteza kiti chake..

  Naona siku hizi kaamua kuwa mwanamitindo
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mbatia si aliitwaga shoga na mrema huyu...
   
 8. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,068
  Likes Received: 7,539
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 598"]
  [TR]
  [TD]
   
 9. NGOGO CHINAVACH

  NGOGO CHINAVACH Verified User

  #9
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 797
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  Kwani wagombea walikuwa wa CHADEMA na MBATIA?CCM,CUF hawakuwa na wagombea?je alitajwa kwa jina?kwanini alikaa kimya mpaka aliposhindwa?
   
 10. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Pamoja na mambo ya hapa na pale nadhani kikubwa kinachomsumbua huyu James (Yakobo) ni kushindwa na mwanamke tu!
   
 11. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  si waliwahi kusema mbatia ni shoga
  au anatembea na wanafunzi wa kiume
   
 12. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Na atashinda tena kwa kishindo kuliko mwaka jana
   
 13. z

  zamlock JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  kama wanataka kuona game ya uchaguzi jinsi tulivyo ichukia ccm halima mdee ashindwe hyo kesi alafu waitishe uchaguzi ndipo ccm watakapo ona game inavyo chezwa
   
 14. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  CCM wanataka kujiaibisha kwa kutaka re-match na cdm sasa hivi. Halafu kwa kutojua wanagusa majimbo ambayo wanajua wazi hawatapata hata kura alufu. Kama unaakili huwezi kutaka ReKmatch na Mdee au Lema. Hivi wanajua kuwa wanachi bado hawajasahau uchaguzi wa mwaka jana na wengi wanawashwa wanatamani itokee tena nafasi ya kuchagua maana watamalizia hasira zao kwa magamba. Hawajajifunza pale Igunga maana cdm haikuwa hata na jina pale lakini ulimi uliwachomoka.

  CCM wangekuwa na akili wangeachana kabisa na mambo ya kura sasa hivi maana watu wanahasira nao wanaweza wakapata hata zero. Pia wanashindwa kuelewa kuwa kwa kufanya hivyo wanawapa cdm muda wakuongea na wananchi tena.

  Acha wajaribu maana mchwa huwa unajaribu hata kwenye jiwe.


  ?
   
 15. P

  Popooo Member

  #15
  Oct 29, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Mbatia kushindwa na Mdee, inampa shida. Magamba wanataka tumia turufu hiyo kupunguzi idadi ya wa bunge wa CDM.
  Ole wenu magamba hizo kura zenu chache mlizo chakachua 2010 zita ishia ndani.
   
 16. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Of cuurse! Yes.
   
 17. l

  leomx2006 New Member

  #17
  Oct 29, 2011
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hana jipya huyo mbatia. CCMc huyo
   
Loading...