Hali yazidi kuwa tete escrow, hapatoshi Dodoma

Hali yazidi kuwa tete escrow, hapatoshi Dodoma

vip mkuu na wewe leo timu zitto?????
duu kweli noma siasa za bongooo

Suala hapa siyo TEAM ZITTO hapa ni pesa zetu walizopiga wazirejeshe wasituletee siasa zao.Hivi iankuaje mtu akatae kupokea fungu,asimamie haki halafu awe mbaya?Hainiingii akilini MBUNGE kuwa na chuki sababu kuna wachache watavuna sifa ya kuwa wzalendo,kwa nini na wao wasipiganie haki ili wavune hiyo sifa/

UPUMBAVU mwingine hata mtu akivaa nguo bado anaonekana yupo uchi.Ndiyo wale wabunge wanoatuletea wakujua kusoma na kuandika.
 
Hivi ni kweli mnapewa pesa kuleta uzushi na uongo namna hii au kuna kitu kmingine cha ziada mnachofanyiwa katika miili yangu ambapo msipoandika uongo kuwaficha hao watu wanaowafanyia hicho hao watu watakataa kuendelea kuwafanyia hivyo amani na faraja yenu ya moyoni itapotea kwani hamuwezi kuishi bila kufanyiwa hivyo? Zitto ametoka hadharani mara kadhaa, mbele ya bunge, mbele ya kamera. Hata mara ya mwisho aliuposisitiza hivyo tena mbele ya kamera kuwa watu wote wahojhiwe kwa uwazi na aliyeshauri isifanyike hivyo ni Job Ndugai tena mbele ya kamera. Uasho wa namna gani huo usiovumilika hata kuja kudanganya jambo ambalo ni bayana kabisa mbele za watu? Leo Deo na Zitto ndio wabaya? Duu bora mchumiatumbo kuliko muwashwa.........Ashakum si matusi muda mwingine lugha za staha zina mwisho wake

Masikini wee! Ilikuwa hivi, Zitto akiwa ndani ya baada ya spika kusema ripoti ya CAG inatosha na baadhi ya wabunge wakitaka iletwe pia na ripoti ya PCCB, Zitto akapewa nafasi kama mwenyekiti wa PAC, live mbele ya kamera akasema kamati yake ina utaratibu wa kuwahoji watu hadharani kwa uwazi hivyo angependa nao wahojiwe hadharani. Hii ilikuwa mara ya pili, mara ya kwanza ni pale alipotuhumiwa kuomba hela PAP kwa mazishi ya mamaake, akasema angependa wahusika wahojiwe hadharani ili kutoa minong'ono na mashaka. Siku Zitto akikabidhiwa hiyo ripoti Job Ndugai akaiambia kamati kuna ushauri wa kutofanya Zitto alichopendekeza kwani suala lipo mahakamani. Kamati ikaridhia na ushauri wa Spika. Sasa wewe endelea kudandia treni kwa mbele

Haya we muwashaji mwenye pepo la uongo mwenye uzima wa kutegemea watu wakusukume kutumia vionjo vyako soma hiyo mwananchi. Mwenzako nilifuatilia kwa siku kadhaa kila hatua.

Katika makabidhiano ya ripoti yaliyoshuhudiwa na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na wajumbe wengine watatu wa PAC, Ndugai alisema; “Naielekeza kamati yako ifanye uchambuzi na kutoa maoni na mapendekezo katika kila hadidu rejea.


“Katika kufanya uchambuzi kamati ijikite zaidi katika kufanya uchambuzi wa CAG na Takukuru.”

Ndugai alisema katika uchunguzi wake, CAG aliwahoji wote waliohusika na jambo hilo na kisha kuwasilisha taarifa yake kwa Takukuru kwa hatua zaidi.

“Kamati ifanye kazi kwa kuzingatia kanuni ya tatu na nne kwa kuzingatia nyongeza ya saba ya kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka 2014 na kifungu cha tisa kifungu kidogo cha kwanza na cha 31 vya Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge, Sura ya 299,” alisema.


Alisema ni matumaini yake kwamba baada ya kumaliza kazi ya kutoa maoni na mapendekezo, taarifa iwasilishwe kwake (Ndugai) ili ajiridhishe kabla ya kuwasilisha bungeni.

“Nimemwelekeza Katibu wa Bunge, asimamie na awape ushirikiano unaotakiwa ili kazi yenu iweze kuwa ya ufanisi na yenye kiwango,” alisema.


Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah aliikabidhi PAC watendaji wanne ambao wataisaidia kufanya kazi hiyo.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Zitto alisema kamati yake itazingatia maagizo ya Ndugai kutokana na masuala ya kimahakama yaliyomo ndani ya ripoti hiyo.

“Kwa hiyo PAC haitakuwa na utaratibu wa kawaida ambao tunafanya tunapowaita watu wakati wa kuhoji mahesabu yao. Nimeshtuka kidogo maana Bunge limeipa nguvu sana PAC katika jambo hili kwa kuwaelekeza kutumia sheria namba tatu. Sisi tutaitumia nguvu hiyo kutenda haki katika jambo hili zima, haki kwa Watanzania na watu ambao wametajwa kuhusika katika jambo zima.”


Zitto alisema ripoti hiyo inaonyesha jinsi taasisi za kiuwajibikaji zinavyofanya kazi, mambo ambayo huwezi kuyaona katika nchi nyingine.




Mzee umefauru chuo cha matusi! Hongera sana. Ni wazi umepanic kamanda. Endelea kutukana lakini, labda inakupa faraja.


Baada ya kupokea ripoti hiyo, Zitto akihojiwa na waandishi wa habari, alisema wa kwanza kuhojiwa na kamati yake atakuwa ni CAG.Zitto alisema kwamba na kwamba kamati itafanya kazi iliyokabidhiwa na Ofisi ya Spika kwa siri.

Alisema watafanya kazi hiyo kwa siri kwa kuwa ndani ya suala hilo kuna mambo ya mahakama, hivyo wanaepuka kuingia katika malalamiko hapo baadaye ya mtu kuonewa na kwamba, watahakikisha wanatenda haki.

Chanzo: Nipashe.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/759870-zitto-watuhumiwa-escrow-kuhojiwa-kwa-siri.html
 
‘’Ni kweli kila mtu atavuna alichopanda, kama wanataka kutugeuza wabunge wote ni ‘Rubber stamp’ tuhalalishe hukumu inayotokana na hasira zao za kunyimwa mgao, basi wamegonga mwamba’’.
Alisema mmoja wa wabunge hao anayetokea chama kimoja cha upinzani akijibu kauli ya Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe aliyenukuliwa na gazeti moja hivi karibuni.


Hivi karibuni Filikunjombe, alisema katika gazeti hilo, kwamba kila mtu atavuna alichopanda katika sakata hilo, baada ya kupokea ripoti ya CAG kutoka kwa Naibu Spika, Job Ndugai.


Ripoti nyeupe, Zitto kapiga mpunga, anashindwa namna ya kuchomoka ndio maana kaanza kusema watahoji wahusika nyuma ya pazia sababu anajua hakuna mtuhumiwa kama alivyokuwa akijitamba.

Nchi hii bado sana kwenye mabadiliko ya kweli kama hii ndio aina ya vijana tulio na kwa kuweka ushabiki wa chama mbele..
 
Tuesday, 18 November 2014

RIPOTI IPTL KULIGAWA BUNGE :- KAMATI YA ZITTO KABWE YATUHUMIWA KWA RUSHWA. WAKILI MSANDO NA MALIMA WALITUMIWA NA KAMATI KUOMBA RUSHWA.




wakili Albert Msando kulia anayedaiwa kutumika kuchukua RUSHWA IPTL kwa niaba ya kamati ya PAC akiwa Zitto Kabwe ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya PAC




IKIWA ni siku chache tu baada ya kutolewa kwa taarifa za kukabidhiwa kwa ripoti ya ukaguzi wa akaunti ya ESCROW, uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), kwa spika na kamati ya mahesabu ya serikali PAC, mengi yameibuka.


Hali hiyo inatokana na kuwepo kwa mgawanyiko wa wabunge kuhusu na jambo hilo huku kila upande ukiwa na mtazamo wake tofauti juu ya jambo hilo, ambalo wabunge wengi wanaamini linapikwa na halizungumzwi ukweli.


Taarifa kutoka Dodoma zinasema kwamba wabunge wengi wameshitushwa na kuvuja kwa taarifa kuwa kamati ya PAC imelivalia njuga suala hilo, baada ya kushindwana kuafikiana mgao wa malipo kutoka kwa wamiliki wa kampuni ya IPTL/PAP ili kulizuia kulimaliza katika Kamati lisifike bungeni mapema mwaka huu.


Taarifa hizo zinasema kamati ya PAC iliwatumia mwanasheria aliyefahamika kwa jina la Albert Msando ambaye ni msaidizi wa kisheria wa Zitto Kabwe na Beatus Malima kujadili juu ya malipo watakayolipwa PAC ili kuidhibiti ripoti hiyo na namna ambavyo PAC ingetoa hukumu ya awali.




Deo Filikunjombe ambaye ni makamu mwenyekiti wa kamati ya PAC.






Vithibitisho ambavyo baadhi ya waandishi wameonyeshwa na baadhi ya wabunge hao, vinaonyesha mijadala iliyokuwa ikiendelea bungeni kuwa mingi ni ya kupikwa na ya kimkakati inayotokana na hasira za kutokupatiwa malipo waliyoomba PAP na hivyo kulitaka bunge lipigie mhuri kitu ambacho ni mgogoro unaotawali na maslahi binafsi.


Haijafahamika mara moja kwamba ni kiasi gani kimeombwa na kamati ya PAC kwa PAP ili walifunge jambo hilo, mlakini baadhi ya wabunge hao wamesema wapo tayari kuweka wazi kila kitu ili kila mtu avune alichopanda.


‘’Ni kweli kila mtu atavuna alichopanda, kama wanataka kutugeuza wabunge wote ni ‘Rubber stamp’ tuhalalishe hukumu inayotokana na hasira zao za kunyimwa mgao, basi wamegonga mwamba’’.
Alisema mmoja wa wabunge hao anayetokea chama kimoja cha upinzani akijibu kauli ya Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe aliyenukuliwa na gazeti moja hivi karibuni.


Hivi karibuni Filikunjombe, alisema katika gazeti hilo, kwamba kila mtu atavuna alichopanda katika sakata hilo, baada ya kupokea ripoti ya CAG kutoka kwa Naibu Spika, Job Ndugai.




Baadhi ya wanahabari walipotembelea mitambo ya IPTL inayolalamikiwa hivi karibuni




Akizungumza kwa kujiamini, mbunge mwingine ambaye pia ameomba ahifadhiwe jina lake kwa sasa anasema ’’Hata Kamati yenyewe ya PAC imegawanyika vipande vipande, wakubwa wao wamevuta mzigo wa kutosha na wenzao wanawaburuza, halafu kazi nzima ya kamati inapelekeshwa kutoa sifa kwa watu wawili tu ambao ni Zitto na Filikunjombe, huu ni upuuzi’’.


Mbunge huyo alisema sisi sote ni wanasiasa, unafikiri nani atakuwa tayari kufanya kazi, halafu sifa ziwaendee watu wawili tu kwamba wao ndio wanaakili sana na wana uchungu sana na nchi.
‘’Hebu jiulize kamati ina wajumbe zaidi ya 20 lakini kila kitu zitto na deo wanajiweka kimbelembele, sasa na safari hii wanapoumbuliwa kwa madili yao ya rushwa wakae kimbelembele hivyo hivyo’’. Alisema mbunge huyo.


Hata hivyo, taarifa kutoka kwenye ripoti iliyovuja ya CAG haionyeshi kwamba kuna tatizo kwenye ukaguzi walioufanya wa akaunti ya ESCROW, badala yake umeibua madai mapya ambayo sio msingi wa uchunguzi walioagizwa kufanya.


Itakakumbukwa kwamba akaunti ya ESCROW ilifunguliwa rasmi Julai, 5 2006, wakati ripoti ya CAG inaonyesha mapungufu ya kuanzia Januar 2002 mpaka Desemba 2006 huku ripoti yenyewe ilipaswa kujikita kati ya 2006 mpaka 2013 ilipofungwa.


‘’Hatupaswi kuwaadhibu watu kwa sababu tu tunawachukia, au kwa sababu tunachuki na tofauti nao binafsi ama za kisiasa, sisi kama bunge ni lazima tufanye kazi zetu kwa kudhibiti hisia zetu, wanachokifanya kina Zitto, David Kafulila na Deo, ni chuki binafsi na si uzalendo kama wanavyotaka iwe, kama ni wazalendo wasingefanya kama haya wanayofanya’’. alisema mbunge huyo.


Alisema mbunge huyo, wabunge hao baada ya kuona ripoti ya CAG haiwatii hatiani serikali na wanaowachukia wao, wanalazimisha kusema kuwa kuna hasara ya bilioni 321. Waache kuwafanya wabunge watoto wadogo kwa kuwa kila kitu tunakijua.






Wakati hayo yakiendelea, jana asubuhi Mbunge wa Mtera-CCM, Livingstone Lusinde aliiomba mwongozo kwa Naibu Spika, Job Ndugai kuhusiana na kubana kwa ratiba katika suala la akaunti ya ESCROW huku jambo hilo likiwa na hamasa kubwa kwa watanzania.
“Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Kamati ya Uongozi ya Bunge iongeze siku au muda katika kujadili suala hili, kwa kuwa ni jambo kubwa linalohitaji kujadiliwa zaidi, tuna mengi tunayoyajua, makando kando ya wanaotuhumiwa na wanaotuhumu pia, kwa kuwa waswahili wana msemo mmoja ukimuona anayelia sana ujue ndio mchawi mwenyewe,’’alisema.


Alisema wabunge wanaolia sana kuhusiana na jambo hilo, wenyewe wana makando makando katika suala hilo kutokana na kuhusika kwa namna moja au nyingine katika sakata hilo, ambalo anaamini kujadiliwa kwa muda mrefu zaidi ndio jambo litakaloweka haki kwa kila mtu.
Hivyo, aliiomba Bunge iongeze siku zaidi kujaidli suala hilo, ambapo Naibu Spika Ndugai alisema atawasiliana na Kamati ya Uongozi ya bunge kuhusiana na mwongozo huo wa Lusinde ili ufanyiwe kazi kwa kuwa jambo hilo lina umuhimu mkubwa kwa taifa.







attachment.php

attachment.php

Wanataka kutuondoa kwenye hoja,waweke documents mezani,tunaojua kuhisi tutaifahamu kweli yote.
 
Pesa za singasinga zimeanza kufanya kazi,ni kama kuna genge la majizi yamepewa ujira yashinde na kukesha yakitetea wahujumu uchumi humu ndani.

Saa nane,na wote wenye nia njema na taifa ,tusiwape muda wa kupumua hawa majizi.

Wapo kimkakati tena kwa kushirikiana na baadhi ya wanahabari wa magazeti .

Tunapaswa kuwatia moyo wajumbe wa kamati ili wajue kuwa nyuma yao kuna sauti kubwa ya wanyonge inawategemea,najua watatumia kila hila kuwaziba mdomo,lkn binafsi sinahofu ma uwezo na uzalendo wa viongozi wa PAC hususan Zitto Kabwe na Filikunjombe,hii ni kamati iliyojipambanua kuwapigania wananchi.

Tumepigana sana kwa umoja wetu kuwalazimisha aki na Lukuvi wailete ripoti.

Leo wanakuja watu waliotuibia kutukatisha tamaa ili tuwaachie huru wakati tayari tumeshakamata mwizi wetu.

This is a point of no return,no retreat no surrender,

"IPTL BRING BACK OUR MONEY"
 
Hizi zote ni porojo tu. Mbona hayo hayakusemwa kabla report ya CAG haijakabidhiwa. Watanzania wanajua mtu mwenye kiasi cha pesa kama hiki kilichoibiwa lazima atatumia pesa kuyumbisha ukweli. Ataweza hata kuingiza pesa hata kati ya mawaziri au wabunge. Muhimu tuwaache PAC wafanye kazi yao. Msafi atang'aa na mchafu tutamuona tu. Propaganda hizi sio mpya.
 
Na bado mtahangaika lakini werema na Muhongo wanamkimbi tumbili,kifungo ni halali yao.
 
Hakuna kuonea huruma Wezi,Wachukuliwe hatua,tumechoka kufanywa Matutusa
 
Pac imeingia mdudu na anayeiharibu ni zitto,filikunjombe hana uchu ka zitto

Ina maana yule KM aliyesema zzk na kafulila ni washe.nzi alishajua kulikuwa na kuombana rushwa? I hope Filikunjombe hatanunulika kirahisi vile.
 
Na bado mtahangaika lakini werema na Muhongo wanamkimbi tumbili,kifungo ni halali yao.
 
mimi akili zangu ni za kawaida na zimenisaidia kujua upeo wa watu wengine, kumbe tatizo hapo ni UMAARUFU! mwanakamati yupo tayari aseme uongo eti kwa kuwa kuna mwanakamati anatajwa sana na vyombo vya habari kuliko yeye! NASIKITIKA KUNA WATANZANIA WANAOMBA KABISA HIYO PESA IENDE KWA MUHINDI KULIKO TANESCO AU SERIKALI (PENGINE ZINGETUMIKA KULIPIA DAWA MSD) ETI KWA SABABU MTU FULANI ATAPATA UMAARUFU KISIASA!

Umeongea kweli kabisa,walio wengi humu wanaongea siasa na kutetea kundi fulani la watu,tuna kazi kabwa sana!
 
‘’Ni kweli kila mtu atavuna alichopanda, kama wanataka kutugeuza wabunge wote ni ‘Rubber stamp’ tuhalalishe hukumu inayotokana na hasira zao za kunyimwa mgao, basi wamegonga mwamba’’.
Alisema mmoja wa wabunge hao anayetokea chama kimoja cha upinzani akijibu kauli ya Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe aliyenukuliwa na gazeti moja hivi karibuni.


Hivi karibuni Filikunjombe, alisema katika gazeti hilo, kwamba kila mtu atavuna alichopanda katika sakata hilo, baada ya kupokea ripoti ya CAG kutoka kwa Naibu Spika, Job Ndugai.


Ripoti nyeupe, Zitto kapiga mpunga, anashindwa namna ya kuchomoka ndio maana kaanza kusema watahoji wahusika nyuma ya pazia sababu anajua hakuna mtuhumiwa kama alivyokuwa akijitamba.

Kipi ndio kipi kwako wewe? Umekuwa mstari wa mbele kulikana tukio zima sasa unatueleza nini?
Ningekuwa zwazwa mimi ningefunga domo langu!
 
Kipi ndio kipi kwako wewe? Umekuwa mstari wa mbele kulikana tukio zima sasa unatueleza nini?
Ningekuwa zwazwa mimi ningefunga domo langu!

No relax mkuu, usipanic! tusubiri ripoti ndio itasema ukweli siyo hizi kelele za wanasiasa.
 
Saa nane,na wote wenye nia njema na taifa ,tusiwape muda wa kupumua hawa majizi.

Tumepigana sana kwa umoja wetu kuwalazimisha aki na Lukuvi wailete ripoti.

Leo wanakuja watu waliotuibia kutukatisha tamaa ili tuwaachie huru wakati tayari tumeshakamata mwizi wetu.

This is a point of no return,no retreat no surrender,

"IPTL BRING BACK OUR MONEY"

Acha lugha za kwenye majukwaa wewe, wezi wamehukumiwa na mahakama gani? Umepigana nini wewe? Kwahiyo kama ripoti haijakamilika ulitaka ipelekwe bungeni hivyohivyo? Kama Lukuvi alichelewesha ripoti, unaimani nayo gani hiyo ripoti?
 
Back
Top Bottom