Hali yazidi kuwa tete escrow, hapatoshi Dodoma

Hali yazidi kuwa tete escrow, hapatoshi Dodoma

kwani kamati ya Zito ndiyo iliyoandika Riport ya CAG? Kamati si itazingatia yaliochunguzwa na CAG na Takokuru sasa hao wabunge wataonewaje. acheni kupotosha kwa hongo za singasinga

You are missing the point Bro rudi usome vizuri.

''Hatupaswi kuwaadhibu watu kwa sababu tu tunawachukia, au kwa sababu tunachuki na tofauti nao binafsi ama za kisiasa, sisi kama bunge ni lazima tufanye kazi zetu kwa kudhibiti hisia zetu, wanachokifanya kina Zitto, David Kafulila na Deo, ni chuki binafsi na si uzalendo kama wanavyotaka iwe, kama ni wazalendo wasingefanya kama haya wanayofanya''. alisema mbunge huyo.


Alisema mbunge huyo, wabunge hao baada ya kuona ripoti ya CAG haiwatii hatiani serikali na wanaowachukia wao, wanalazimisha kusema kuwa kuna hasara ya bilioni 321. Waache kuwafanya wabunge watoto wadogo kwa kuwa kila kitu tunakijua.
 
mtasema mengi sana lakini mwisho wa siku lazima kila jiwe lipinduliwe. wezi wote lazima waende wakanydee debe segerea.

hako kamchezo k@kup!nduliwa kamekuingia damuni mkuu! teh teh teh teh! Wezi wamehukumiwa na mahakama ya ufipa au?
 
Hivi ni kweli mnapewa pesa kuleta uzushi na uongo namna hii au kuna kitu kmingine cha ziada mnachofanyiwa katika miili yangu ambapo msipoandika uongo kuwaficha hao watu wanaowafanyia hicho hao watu watakataa kuendelea kuwafanyia hivyo amani na faraja yenu ya moyoni itapotea kwani hamuwezi kuishi bila kufanyiwa hivyo? Zitto ametoka hadharani mara kadhaa, mbele ya bunge, mbele ya kamera. Hata mara ya mwisho aliuposisitiza hivyo tena mbele ya kamera kuwa watu wote wahojhiwe kwa uwazi na aliyeshauri isifanyike hivyo ni Job Ndugai tena mbele ya kamera. Uasho wa namna gani huo usiovumilika hata kuja kudanganya jambo ambalo ni bayana kabisa mbele za watu? Leo Deo na Zitto ndio wabaya? Duu bora mchumiatumbo kuliko muwashwa.........Ashakum si matusi muda mwingine lugha za staha zina mwisho wake

Mkuu nnamashaka na wewe, siyo mzima wewe!

Baada ya kupokea ripoti hiyo, Zitto akihojiwa na waandishi wa habari, alisema wa kwanza kuhojiwa na kamati yake atakuwa ni CAG.Zitto alisema kwamba na kwamba kamati itafanya kazi iliyokabidhiwa na Ofisi ya Spika kwa siri.

Alisema watafanya kazi hiyo kwa siri kwa kuwa ndani ya suala hilo kuna mambo ya mahakama, hivyo wanaepuka kuingia katika malalamiko hapo baadaye ya mtu kuonewa na kwamba, watahakikisha wanatenda haki.

Hayo ni maneno ya Ndugai au ya Zitto? kwahiyo Zitto mara hii kasikiliza ushauri wa Ndugai? yaani unatokwa na matusi minikajua unahoja yenye kunikamata kweli kumbe zwazwa tu :boink:
 
Hali ni tulivu na shwari msizuzuje na kelele za mbwa subirininmwenye mbwa aseme
 
Habari hii ni kipuuzi haina mashiko chadema tumegundua mnajaribu kukchafua zitto lkn hamtaweza.
 
Naona Michoro ya wazi katika kuzima hii ishu.......
 
mimi akili zangu ni za kawaida na zimenisaidia kujua upeo wa watu wengine, kumbe tatizo hapo ni UMAARUFU! mwanakamati yupo tayari aseme uongo eti kwa kuwa kuna mwanakamati anatajwa sana na vyombo vya habari kuliko yeye! NASIKITIKA KUNA WATANZANIA WANAOMBA KABISA HIYO PESA IENDE KWA MUHINDI KULIKO TANESCO AU SERIKALI (PENGINE ZINGETUMIKA KULIPIA DAWA MSD) ETI KWA SABABU MTU FULANI ATAPATA UMAARUFU KISIASA!
 
mimi binafsi mpaka sasa nimechochwa maana siasa ni kama wehu fulani until now wananchi tunashindwa kuelewa mkweli ni nani? kila mtu anakula kwa urefu Wa kamba yake full stop
 
You are missing the point Bro rudi usome vizuri.

‘’Hatupaswi kuwaadhibu watu kwa sababu tu tunawachukia, au kwa sababu tunachuki na tofauti nao binafsi ama za kisiasa, sisi kama bunge ni lazima tufanye kazi zetu kwa kudhibiti hisia zetu, wanachokifanya kina Zitto, David Kafulila na Deo, ni chuki binafsi na si uzalendo kama wanavyotaka iwe, kama ni wazalendo wasingefanya kama haya wanayofanya’’. alisema mbunge huyo.


Alisema mbunge huyo, wabunge hao baada ya kuona ripoti ya CAG haiwatii hatiani serikali na wanaowachukia wao, wanalazimisha kusema kuwa kuna hasara ya bilioni 321. Waache kuwafanya wabunge watoto wadogo kwa kuwa kila kitu tunakijua.

Chuki binafsi ya nani na nani? Huna point huna hoja kaa kimya.
 
ccm
chadema
wanasiasa
cuf
vyombo vya habari

lao moja hawa wanasiasa wanatutesa sisi wanachi wa kawaida
 
hili ni suala la kitaifa, acha kuingiza usiasa wako wa kikumer hapa. wezi wote waliotajwa lazima washughulikiwe kwa ufasaha.

Ufipa kuna chuo cha matusi enheee. Naona ndio moja ya sifa za kuwa Bavicha.
 
Hizi bado ni aina ya tricks zinazotumiwa na washenzi kwa kuwalaghai waandishi wa habari baadhi ambao nao ni makanjanja tusubirini mambo yanaenda kwa hatua ikifika hatua ya kujua kama kuna rushwa ilitembeas ndani ya kamati tutajua tu lakini kwa sasa tuachieni kwanza nyie waandishi makanjanja hatua hii inahitaji utulivu sio fulani alipata hiki huyu alikosa ndio maana analalama mlikuwa wapi kusema mapema mambo yamefika hapa ndio mnataka kuanza kutuchanganya acheni hizo bhana hiyo riport lazima bati la bunge liezuke kama kuna wabunge watajiokeza kuwakingia kifua wezi
 
Mkuu nnamashaka na wewe, siyo mzima wewe!

Baada ya kupokea ripoti hiyo, Zitto akihojiwa na waandishi wa habari, alisema wa kwanza kuhojiwa na kamati yake atakuwa ni CAG.Zitto alisema kwamba na kwamba kamati itafanya kazi iliyokabidhiwa na Ofisi ya Spika kwa siri.

Alisema watafanya kazi hiyo kwa siri kwa kuwa ndani ya suala hilo kuna mambo ya mahakama, hivyo wanaepuka kuingia katika malalamiko hapo baadaye ya mtu kuonewa na kwamba, watahakikisha wanatenda haki.

Hayo ni maneno ya Ndugai au ya Zitto? kwahiyo Zitto mara hii kasikiliza ushauri wa Ndugai? yaani unatokwa na matusi minikajua unahoja yenye kunikamata kweli kumbe zwazwa tu :boink:

Masikini wee! Ilikuwa hivi, Zitto akiwa ndani ya baada ya spika kusema ripoti ya CAG inatosha na baadhi ya wabunge wakitaka iletwe pia na ripoti ya PCCB, Zitto akapewa nafasi kama mwenyekiti wa PAC, live mbele ya kamera akasema kamati yake ina utaratibu wa kuwahoji watu hadharani kwa uwazi hivyo angependa nao wahojiwe hadharani. Hii ilikuwa mara ya pili, mara ya kwanza ni pale alipotuhumiwa kuomba hela PAP kwa mazishi ya mamaake, akasema angependa wahusika wahojiwe hadharani ili kutoa minong'ono na mashaka. Siku Zitto akikabidhiwa hiyo ripoti Job Ndugai akaiambia kamati kuna ushauri wa kutofanya Zitto alichopendekeza kwani suala lipo mahakamani. Kamati ikaridhia na ushauri wa Spika. Sasa wewe endelea kudandia treni kwa mbele
 
Mkuu nnamashaka na wewe, siyo mzima wewe!

Baada ya kupokea ripoti hiyo, Zitto akihojiwa na waandishi wa habari, alisema wa kwanza kuhojiwa na kamati yake atakuwa ni CAG.Zitto alisema kwamba na kwamba kamati itafanya kazi iliyokabidhiwa na Ofisi ya Spika kwa siri.

Alisema watafanya kazi hiyo kwa siri kwa kuwa ndani ya suala hilo kuna mambo ya mahakama, hivyo wanaepuka kuingia katika malalamiko hapo baadaye ya mtu kuonewa na kwamba, watahakikisha wanatenda haki.

Hayo ni maneno ya Ndugai au ya Zitto? kwahiyo Zitto mara hii kasikiliza ushauri wa Ndugai? yaani unatokwa na matusi minikajua unahoja yenye kunikamata kweli kumbe zwazwa tu :boink:

Haya we muwashaji mwenye pepo la uongo mwenye uzima wa kutegemea watu wakusukume kutumia vionjo vyako soma hiyo mwananchi. Mwenzako nilifuatilia kwa siku kadhaa kila hatua.

Katika makabidhiano ya ripoti yaliyoshuhudiwa na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na wajumbe wengine watatu wa PAC, Ndugai alisema; "Naielekeza kamati yako ifanye uchambuzi na kutoa maoni na mapendekezo katika kila hadidu rejea.


"Katika kufanya uchambuzi kamati ijikite zaidi katika kufanya uchambuzi wa CAG na Takukuru."

Ndugai alisema katika uchunguzi wake, CAG aliwahoji wote waliohusika na jambo hilo na kisha kuwasilisha taarifa yake kwa Takukuru kwa hatua zaidi.

"Kamati ifanye kazi kwa kuzingatia kanuni ya tatu na nne kwa kuzingatia nyongeza ya saba ya kanuni za Kudumu za Bunge za mwaka 2014 na kifungu cha tisa kifungu kidogo cha kwanza na cha 31 vya Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge, Sura ya 299," alisema.

Alisema ni matumaini yake kwamba baada ya kumaliza kazi ya kutoa maoni na mapendekezo, taarifa iwasilishwe kwake (Ndugai) ili ajiridhishe kabla ya kuwasilisha bungeni.

"Nimemwelekeza Katibu wa Bunge, asimamie na awape ushirikiano unaotakiwa ili kazi yenu iweze kuwa ya ufanisi na yenye kiwango," alisema.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah aliikabidhi PAC watendaji wanne ambao wataisaidia kufanya kazi hiyo.

Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Zitto alisema kamati yake itazingatia maagizo ya Ndugai kutokana na masuala ya kimahakama yaliyomo ndani ya ripoti hiyo.

"Kwa hiyo PAC haitakuwa na utaratibu wa kawaida ambao tunafanya tunapowaita watu wakati wa kuhoji mahesabu yao. Nimeshtuka kidogo maana Bunge limeipa nguvu sana PAC katika jambo hili kwa kuwaelekeza kutumia sheria namba tatu. Sisi tutaitumia nguvu hiyo kutenda haki katika jambo hili zima, haki kwa Watanzania na watu ambao wametajwa kuhusika katika jambo zima."


Zitto alisema ripoti hiyo inaonyesha jinsi taasisi za kiuwajibikaji zinavyofanya kazi, mambo ambayo huwezi kuyaona katika nchi nyingine.



 
‘’Ni kweli kila mtu atavuna alichopanda, kama wanataka kutugeuza wabunge wote ni ‘Rubber stamp’ tuhalalishe hukumu inayotokana na hasira zao za kunyimwa mgao, basi wamegonga mwamba’’.
Alisema mmoja wa wabunge hao anayetokea chama kimoja cha upinzani akijibu kauli ya Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe aliyenukuliwa na gazeti moja hivi karibuni.

Hivi karibuni Filikunjombe, alisema katika gazeti hilo, kwamba kila mtu atavuna alichopanda katika sakata hilo, baada ya kupokea ripoti ya CAG kutoka kwa Naibu Spika, Job Ndugai.


Ripoti nyeupe, Zitto kapiga mpunga, anashindwa namna ya kuchomoka ndio maana kaanza kusema watahoji wahusika nyuma ya pazia sababu anajua hakuna mtuhumiwa kama alivyokuwa akijitamba.

Hata mtoto wa kike ana aibu kidogo...grow up!
 
Mimi naona, hata hiyo habari yenyewe inutata. kama unasema ripoti haina kitu, inakuwaje basi IPTL wanataka kuwapa rushwa PAC?
Hawa waandishi wengine wa habari ziro kabisa,
.
 
Akizungumza kwa kujiamini, mbunge mwingine ambaye pia ameomba ahifadhiwe jina lake kwa sasa anasema ''Hata Kamati yenyewe ya PAC imegawanyika vipande vipande, wakubwa wao wamevuta mzigo wa kutosha na wenzao wanawaburuza, halafu kazi nzima ya kamati inapelekeshwa kutoa sifa kwa watu wawili tu ambao ni Zitto na Filikunjombe, huu ni upuuzi''.


Mbunge huyo alisema sisi sote ni wanasiasa, unafikiri nani atakuwa tayari kufanya kazi, halafu sifa ziwaendee watu wawili tu kwamba wao ndio wanaakili sana na wana uchungu sana na nchi.
''Hebu jiulize kamati ina wajumbe zaidi ya 20 lakini kila kitu zitto na deo wanajiweka kimbelembele, sasa na safari hii wanapoumbuliwa kwa madili yao ya rushwa wakae kimbelembele hivyo hivyo''. Alisema mbunge huyo.
 
Back
Top Bottom