Dan Geoff P
Member
- Jan 16, 2012
- 85
- 100
Habari zenu wana jamii, leo nimeona niongelee hali ya vyoo katika chuo chetu hiki ambacho kipo mjini kabisa katika jiji hili kubwa kuliko yote Tanzania,,hakuna shaka ukikutana na mwanachuo yeyote anayesoma katika chuo hiki hatasita kukueleza jinsi hali ya vyoo ilivyo mbaya (chafu) katika chuo hiki,,hali hiyo pia imeambatana na uhaba wa maji katika maeneo husika (vyoo) hivo kupelekea wanafunzi wengi kuugua magonjwa ya mfumo wa mkojo (U.T.I) mara kwa mara. Tatizo hili limekuwa ni sugu chuoni hapo na hivo kupelekea wanachuo kutumia gharama kubwa za matibabu bila kupona kwani kila wanapotibiwa wanarudi kwenye mazingira yale yale ya uchafu na kupelekea kuugua tena baada ya muda mfupi.
Mbaya zaidi hii inapelekea usugu wa wadudu (drug resistance) hivo mgonjwa kutumia dawa kubwa zaidi yenye garama kubwa.
Mbaya zaidi hii inapelekea usugu wa wadudu (drug resistance) hivo mgonjwa kutumia dawa kubwa zaidi yenye garama kubwa.