Hali ya vyoo Dar es salaam Institute of Technology (D.I.T) ni mbaya.

Dan Geoff P

Member
Jan 16, 2012
85
100
Habari zenu wana jamii, leo nimeona niongelee hali ya vyoo katika chuo chetu hiki ambacho kipo mjini kabisa katika jiji hili kubwa kuliko yote Tanzania,,hakuna shaka ukikutana na mwanachuo yeyote anayesoma katika chuo hiki hatasita kukueleza jinsi hali ya vyoo ilivyo mbaya (chafu) katika chuo hiki,,hali hiyo pia imeambatana na uhaba wa maji katika maeneo husika (vyoo) hivo kupelekea wanafunzi wengi kuugua magonjwa ya mfumo wa mkojo (U.T.I) mara kwa mara. Tatizo hili limekuwa ni sugu chuoni hapo na hivo kupelekea wanachuo kutumia gharama kubwa za matibabu bila kupona kwani kila wanapotibiwa wanarudi kwenye mazingira yale yale ya uchafu na kupelekea kuugua tena baada ya muda mfupi.
Mbaya zaidi hii inapelekea usugu wa wadudu (drug resistance) hivo mgonjwa kutumia dawa kubwa zaidi yenye garama kubwa.
 
Shida ni kuwa mnatarajia viwe safi, bila kutafakari issue ya ustaarabu wa kutumia. Mtu wa kwanza tu anayeingia anachafua.

Usafi wa vyoo unaweza kuwa endelevu tu iwapo kuna uungwana wa matumizi. Kwenye gents urinary, kwa nini tusilenge mahali vema bali tunalowanisha sakafu.

Ni wazi suala la maji ni muhimu, lakini kwa experience yangu ya UDSM, hata maji yakiwepo bado watumiaji hawawajibiki.

It can be done play your part.
 
Kama ni kweli' wanafunzi wote mgomeni, fanyeni maandamano ya amani kuonyesha kuwa hampendezwi na hali hiyo inayo hatarisha maisha na afya zenu. Fanyeni kama watoto wa farao kule misri, kawaida wanakwenda tahrir square, nyie nendeni m'moja. Acha kulalamika tu, chukueni hatua. Afya ndiyo kila kitu, elimu yenu mtaiko hivi hivi, mkifanya mchezo na uchafu.
 
Nilipita UDSM mwanzoni mwa mwaka huu...nilipoingia 'ofisi ndogo' kwenye jengo moja niliona maajabu ya Musa...sasa sijui tatizo ni wingi wa wanafunzi au hakuna maji ya kutosha au hakuna watu walioajiriwa kusafisha vyoo hivyo au wanafunzi wenyewe tu wamekosa ustaarabu!? Inatia kinyaa sana...!
 
Nakumbuka headmaster wangu wa O'level alinieleza kitu ambacho siwezi kukisaau. Namnukuhu; "Ukitaka kujua kuwa elimu imeshuka - angalia tabia za vijana walioko mashuleni na vyuoni"

Tabia za vijana walioko mashuleni na vyuoni ni chafu kupita kiasi; hivyo hata vyoo vyao lazima viwe kama tabia zao.
Chuo cha SAut kwa kuwa kiko chini ya uangalizi wa dini, kidogo tabia za wanafunzi zimeanza kurudi kwenye mstari, lakini chuo kama DIT chini ya serikali ya CCM - wezi wa mali ya umma, kodi wanapeleka nje ya nchi, wanafunzi hawana uangalizi wa kutosha tutegemee nini?

Nilitegemea taarifa hii itolewe na uongozi wa juu wakilalamikia serikali kwa kutojali mazingira ya wanafunzi; sijui mtoa mada ni mwanafunzi au mtumishi.

Poleni sana, mambo yatarekebika tukiwakataa wahujumu uchumi.
 
Ndugu yangu mimi ni mtumishi wa afya katika moja ya hospitali karibu na D.I.T na nimekuwa nikiwatibu mara kwa mara hawa wanafunzi,pamoja na yote hayo nimekuwa nikiwashauri juu ya usafi na kupeleka malalamiko yao mahali husika ili waondokane na tatizo hilo na kwamba wasitegemee mtu wa mbali aje awatatulie matatizo yao.
Nakumbuka headmaster wangu wa O'level alinieleza kitu ambacho siwezi kukisaau. Namnukuhu; "Ukitaka kujua kuwa elimu imeshuka - angalia tabia za vijana walioko mashuleni na vyuoni"

Tabia za vijana walioko mashuleni na vyuoni ni chafu kupita kiasi; hivyo hata vyoo vyao lazima viwe kama tabia zao.
Chuo cha SAut kwa kuwa kiko chini ya uangalizi wa dini, kidogo tabia za wanafunzi zimeanza kurudi kwenye mstari, lakini chuo kama DIT chini ya serikali ya CCM - wezi wa mali ya umma, kodi wanapeleka nje ya nchi, wanafunzi hawana uangalizi wa kutosha tutegemee nini?

Nilitegemea taarifa hii itolewe na uongozi wa juu wakilalamikia serikali kwa kutojali mazingira ya wanafunzi; sijui mtoa mada ni mwanafunzi au mtumishi.

Poleni sana, mambo yatarekebika tukiwakataa wahujumu uchumi.
 
Nilijizuga kuingia choo cha sabasaba, loh.

Utafikiri watu wanafanya research ya kuvumbua bomu la nyuklia!

Halafu nilivyowalalamikia wahudumu wananishangaa mimi, kama nashangaa samaki kuogelea.
 
Huo ni muendelezo wa mifano ya mazingira ambayo yalitakiwa kuwa mfano kwa jamii, lakini badala yake imekua kinyume
chake, kuna siku mwana JF alielezea kilio chake kwa aliyoyakuta kwenye choo katika wodi za wagonjwa!!

Wakati mwengine tunaweza kulaumu, uongozi wa juu, lakini tukubali pia kwamba, uwajibikaji ni tatizo katika secta za ngazi
zote kuanzia juu mpaka chini, hapa nchini kwetu, Tanzania. Tukiweza kufanya yale tuliyo na uwezo nayo kutoka ngazi za chini
huenda tukaweza kumaliza tatizo au kubakiza padogo sasa! Hebu angalia, ingawa matunda ya mti huchomoza juu lakini
mkulima huondoa magugu yaliyopo chini !!
 
Karibuni Arusha Technical College, maji ya kutosha, vyoo visafi na idadi sahihi ya wanafunzi. Ndio chuo bora cha ufundi kilichobaki Tanzania
 
Nimesikia leo taarifa ya habari, nurse kawatoa drip watoto wagonjwa waliolazwa hospitali ya wilaya chato, sababu wazazi wanaowahudumia wagonjwa hao walikataa kusafisha choo. Hospitali ya wilaya, mgonjwa/ mhudumu wa mgonjwa anasafisha choo.

Leo inakuja hadithi ya vyuoni, usijekuta hakuna watu wa kusafisha vyoo hivyo, kama wapo wapo kwenye pay roll tu mishahara inaingia mfukoni mwa mtu.

Siku nyingine daktari analalamika kunguni hospitalim ya wilaya, anauliza anasema wagonjwa ndio wanaleta, badala ya kusema kuwa hao kunguni ni shauri yeye ameshindwa kudhibiti uchafu.

Sisi Watanzania ni wachafu kupindukia, rasi na convoy ya BMW anapita kwenye majalala, Rais na covyo ya Benzi anakatisha kwenye dimbwi la maji taka.

Tunakwenda wapi nchii hii jamani, nchi hii imeoza, inanuka bado kidogo itakufa sio utani.
 
watoto wa pale nuksi,yani chuo kimechanganywa na watoto waliomaliza form four,niliwahi kukaa hostel zao kwa takribani mwezi mzima,walinipga jeans zangu na perfume yangu..dah,..
 
Nimesikia leo taarifa ya habari, nurse kawatoa drip watoto wagonjwa waliolazwa hospitali ya wilaya chato, sababu wazazi wanaowahudumia wagonjwa hao walikataa kusafisha choo. Hospitali ya wilaya, mgonjwa/ mhudumu wa mgonjwa anasafisha choo.

Leo inakuja hadithi ya vyuoni, usijekuta hakuna watu wa kusafisha vyoo hivyo, kama wapo wapo kwenye pay roll tu mishahara inaingia mfukoni mwa mtu.

Siku nyingine daktari analalamika kunguni hospitalim ya wilaya, anauliza anasema wagonjwa ndio wanaleta, badala ya kusema kuwa hao kunguni ni shauri yeye ameshindwa kudhibiti uchafu.

Sisi Watanzania ni wachafu kupindukia, rasi na convoy ya BMW anapita kwenye majalala, Rais na covyo ya Benzi anakatisha kwenye dimbwi la maji taka.

Tunakwenda wapi nchii hii jamani, nchi hii imeoza, inanuka bado kidogo itakufa sio utani.

Mkuu, hata wanaosafisha wakiwepo, watumiaji wanatumiaje?

Haijajengeka culture ya kuwafikiria wengine. Kwa matumizi ya vyoo, mtu ukikuta choo ni kisafi, unapaswa kukiacha kisafi pia.

Kwa nini tuweke vitu sakafuni balala ya kwenye tundu?

Tukiweza kufanya hivyo hata watu wa kufanya usafi sehemu hizo watapatikana na watafurahia kazi zao.
 
Nilipokuwa udsm, nilikuwa nalala block a, hapa barabarani karibu na cafeteria! Nilikuwa nakwenda zangu kwa sista kente kukata gogo, daily na kuoga! Maisha ya vile vyoo yalinishinda kabisaaaaaa, ndio kisa cha kukaa pale mpaka namaliza third year! Lol! Poleni wanafunzi!
 
Kwa nini tuweke vitu sakafuni balala ya kwenye tundu?

It is something i cannot imagine, huyu mtu ana akili timamu kweli, au ni punguani, hayawani, kichaa auuuuuu.

Akianza kazi akienda kazini badala ya kuendesha kushoto mwa barabara, ataendesha kulia mwa barabara na kuona yu sahihi,

Kazini atajenga barabara mbaya ndugu yake atapata ajali akiendesha gari,

Kazini atafanya operesheni ya kichwa badala ya mguu etc etc orodha ni ndefu

Sasa naelewa
 
Shida ni kuwa mnatarajia viwe safi, bila kutafakari issue ya ustaarabu wa kutumia. Mtu wa kwanza tu anayeingia anachafua.

Usafi wa vyoo unaweza kuwa endelevu tu iwapo kuna uungwana wa matumizi. Kwenye gents urinary, kwa nini tusilenge mahali vema bali tunalowanisha sakafu.

Ni wazi suala la maji ni muhimu, lakini kwa experience yangu ya UDSM, hata maji yakiwepo bado watumiaji hawawajibiki.

It can be done play your part.

me like this
 
Back
Top Bottom