Hali ya usikivu mdogo inavyonikosesha ajira/fursa

Pole kaka yangu....
Me nataka kujua ni tatizo la kuzaliwa au limekuja ukubwani??
 
Gharama sana ndiyo kiasi gani?

Inawezekana zikawa gharama Tanzania lakini wengine wakawa na njia rahisi ya kuzipata nje.

Fuatilia utupe mrejesho. Zinahitajika za aina gani, za specification gani.
Ngoja nifatilie mkuu tutajuzana
 
Habari zenu wana jamvi natumaini wote ni wazima.

Bila kupoteza muda Niende kwenye mada kuu...Ni wazi kabisa kwamba Mimi nasumbuliwa na changamoto ya usikivu (tinnitus) "hali ya kusikia sauti mfano wa honi au kengele ndani ya sikio hali inayopolekea sauti kuingiliana na kushindiwa kuelewa kilichoongelewa na mtu anaekuongelesha kwa wakati huo hadi arudie tena na uconcetrate kwake kwa kuupuuzia sauti za ndani ya sikio".

Changamoto hii inaniepeleka Mimi kukosa Ajira sehem mbali mbali nikiomba kazi nikifika hatua ya usaili wa mahojiano nimekuwa nikiingia na presha kubwa mno hali inayopolekea kufeli interview wakishajua kama Nina shida hiyo wakati mwingine huwa naanza kwa kuwaeleza shida yangu ili wanifanye kama mtu mwenye uhitaji maalumu ili hata nisipoelewa swali waweze kurudia nilielewe lakini bado ni changamoto

Mwaka 2021 nilibahatika kupata kazi kiwanda kimoja kama DATA CLERK lakini mwaka huu nikakataliwa kurejea kazini licha ya kwamba tatizo langu linafahamika ofisi ya waajiri na OSHA lakini daktari mkuu wa kiwanda amenigomea kurudi kazini kusaini mkataba maana kazi ni ya msimu na kila mwaka mnaporejea lazima mfanye vipimo ndo muungie kazini miaka yote hiyo nimekuwa nikipita hatua zote na kupelekea kupangiwa eneo zuri kulingana na hali yangu.

Ni Rasmi sasa nimekuwa baba wa nyumbani sina pa kwenda kila kona ni majaribu nafsi yangu inaumia nikiamka asubuh nikiona wenzangu waliokuwa wananipitia kwenda kazi sasa wanakwenda peke yao Mimi nikiwa nimebaki nyumbani.

Ndugu zangu nirejee tena kwenu kwa mtu yoyote humu mahala popote mwenye connection ya kazi aina yoyote ile basi tusaidieane asihofie hali yangu kwa kuwa sio ya kutisha ni tinnitus tu ndo inayonitesa binafsi Nina Diploma ya ukutubi na uhifadhi wa nyataka (Ordinary Diploma in Library, records and information studies) Nina uzoefu mzuri na wa muda mrefu mbali na kazi kuhusu fani yangu nimehudumu kama Quality Control QC, office attendant, warehouse attendant, Leaf Account Clerk and Greenleaf Data Clerk katika viwanda tofauti tofauti(TTPL,21st century textile LTD,Allionce one international) tangu 2015.

Mbali na hapo kazi yoyote ile halali nafanya naomba msaada wenu wapendwa..Asanteeni na Mungu awabariki

Mwinuka Frank D.

Morogoro
Chamwino-Shule street
House no 060
Simu:0654204670
0744204670
Email.Frankdmwinuka@gmail.com
Pole sana!
Tinnitus haina tiba kamili ila ukienda Muhimbili kumuona ENT Specialist anweza kukufanyia tathmini kamili na kukushauri kutumia electronic device to supress noice..
Kilichokutokea ni sehemu ya sikio inayochuja sauti na kupeleka kwenye ubongo kwa ajili ya utambuzi.
Vifaa vya kusaidia kuchuja sauti vipo.
All the best na Mungu akupe wepesi.
 
Gharama sana ndiyo kiasi gani?

Inawezekana zikawa gharama Tanzania lakini wengine wakawa na njia rahisi ya kuzipata nje.

Fuatilia utupe mrejesho. Zinahitajika za aina gani, za specification gani.
Navojua kwa hearing aids nzuri za kumfaa pamoja na kumpunguzia kelele za tinnitus gharama zake ni si chini ya dola 5000/=.
 
Pole sana!
Tinnitus haina tiba kamili ila ukienda Muhimbili kumuona ENT Specialist anweza kukufanyia tathmini kamili na kukushauri kutumia electronic device to supress noice..
Kilichokutokea ni sehemu ya sikio inayochuja sauti na kupeleka kwenye ubongo kwa ajili ya utambuzi.
Vifaa vya kusaidia kuchuja sauti vipo.
All the best na Mungu akupe wepesi.
Ngoja tufatilie mkuu
 
Pole sana ndugu mm ni social worker najisikia vibaya mtu kubaguliwa kwa namna yyte ile. Nakushauri uende kwa afisa ustawi sehemu ulipo akuandikie barua ili unapoenda kwenye interview uingie nayo.
Upata kibarua ukumbuke kununua zile equipments za kuinua sauti sizijui zinaitwaje
Samahan ndugu naweza pata nafasi ya kuja DM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wana jamvi natumaini wote ni wazima.

Bila kupoteza muda Niende kwenye mada kuu...Ni wazi kabisa kwamba Mimi nasumbuliwa na changamoto ya usikivu (tinnitus) "hali ya kusikia sauti mfano wa honi au kengele ndani ya sikio hali inayopolekea sauti kuingiliana na kushindiwa kuelewa kilichoongelewa na mtu anaekuongelesha kwa wakati huo hadi arudie tena na uconcetrate kwake kwa kuupuuzia sauti za ndani ya sikio".

Changamoto hii inaniepeleka Mimi kukosa Ajira sehem mbali mbali nikiomba kazi nikifika hatua ya usaili wa mahojiano nimekuwa nikiingia na presha kubwa mno hali inayopolekea kufeli interview wakishajua kama Nina shida hiyo wakati mwingine huwa naanza kwa kuwaeleza shida yangu ili wanifanye kama mtu mwenye uhitaji maalumu ili hata nisipoelewa swali waweze kurudia nilielewe lakini bado ni changamoto

Mwaka 2021 nilibahatika kupata kazi kiwanda kimoja kama DATA CLERK lakini mwaka huu nikakataliwa kurejea kazini licha ya kwamba tatizo langu linafahamika ofisi ya waajiri na OSHA lakini daktari mkuu wa kiwanda amenigomea kurudi kazini kusaini mkataba maana kazi ni ya msimu na kila mwaka mnaporejea lazima mfanye vipimo ndo muungie kazini miaka yote hiyo nimekuwa nikipita hatua zote na kupelekea kupangiwa eneo zuri kulingana na hali yangu.

Ni Rasmi sasa nimekuwa baba wa nyumbani sina pa kwenda kila kona ni majaribu nafsi yangu inaumia nikiamka asubuh nikiona wenzangu waliokuwa wananipitia kwenda kazi sasa wanakwenda peke yao Mimi nikiwa nimebaki nyumbani.

Ndugu zangu nirejee tena kwenu kwa mtu yoyote humu mahala popote mwenye connection ya kazi aina yoyote ile basi tusaidieane asihofie hali yangu kwa kuwa sio ya kutisha ni tinnitus tu ndo inayonitesa binafsi Nina Diploma ya ukutubi na uhifadhi wa nyataka (Ordinary Diploma in Library, records and information studies) Nina uzoefu mzuri na wa muda mrefu mbali na kazi kuhusu fani yangu nimehudumu kama Quality Control QC, office attendant, warehouse attendant, Leaf Account Clerk and Greenleaf Data Clerk katika viwanda tofauti tofauti(TTPL,21st century textile LTD,Allionce one international) tangu 2015.

Mbali na hapo kazi yoyote ile halali nafanya naomba msaada wenu wapendwa..Asanteeni na Mungu awabariki

Mwinuka Frank D.

Morogoro
Chamwino-Shule street
House no 060
Simu:0654204670
0744204670
Email.Frankdmwinuka@gmail.com
Soma elimu maalum kaka ujue lugha ya alama ndugu
 
Pole sana ndugu yangu! na mimi nina tatizo la kusikia na kuongea vizuri!
Nilisomea Certificate ya IT 2007-2008(UCC), Diploma ya IT 2008-2010(UCC) na Shahada ya Sayansi ya Kompyuta 2014(IAA). Tangu nimalize chuo nilianza kuomba kazi na kufanya usaili mbalimbali kuanzia mwaka 2015. Na Mwaka 2017 TRA walitoa nafasi za kazi katika kada mbalimbali, nilibahatika kupita kwenye usaili wa mchujo, vitendo hadi mahojiano (TRA) . Kabla ya usaili wa mahojiano nilikuwa nimeshawapa taarifa kwamna Nina matatizo ya kusikia vizuri na uongeaji, hivyo katika kufanyia mahojiano nakumbuka yalikuwa maswali Saba na baadhi ya vipengele vyake, swali la kwanza niliongea kwa mdomo ambayo ilikuwa inaongelea kuhusu background ya elimu. Baada ya hapo wakanipeleka chunba maalumu nifanye maswali kwa kuandika. Baada ya kumaliza wakaniliuza unafbaya kazi wapi nikawaambia sina kazi, na japo la waliokuwa wananihoji walikuwa wababa wawili na wamama wawili.
Pamoja na hayo yote sikuweza kuitwa kazini. Na walikuwa wanahitaji watu wanne kati ya wasailiwa 28. Na kwenye vitendo tulikuwa 80, na mchujo wa kuandika walikuwa karibia 400 nchi nzima kwa kada ya System Administrator.
Nakumbuka mama mmoja alionea huruma sana. Na huyo mama alishaaga dunia mwaka jana akiwa kwenye mwajiriwa wa sekretariat ya ajira.

Ndio hivyo watu wenye shida ya kusikia wanapata shida hawathaminiwi

Mungu atusaidie sana
Mimi mwenyewe nina hilo tatizo japo niko kada ya elimu.
 
Pole sana mkuu, mimi binafsi nina hilo tatizo tangu 2008 niko form one. Tulishazunguka sana hospital zote Tanzania mpaka ujerumani ila holla.

Hearing devices hazikusaidia, sijfuatilia tena kama zipo more advanced siku hizi.

But trust me my friend, with time tatizo linapungua. Now mtu hawezi jua kama nina tatizo labda akikaa na mimi kwa muda mrefu sana.

Zamani ilikua hatuelewani na mtu kabisa, but now miaka inavozidi kwenda hali inazidi kuwa better.

Nishapitia hali zote hapo umetaja, kuchekwa, dharau etc.

Naweza kubaliana na wewe kuhusu kubaniwa ajira sababu ya tatizo lako, lakini pia naweza kutokubaliana na wewe (based on my own experiences). Nadhani kikubwa zaidi Onyesha uwezo wako, mimi napata deals kibao kwenye mashirika mbalimbali na ni wao wananitafuta mimi (nina masters katika kada ya afya).

Kuwa na tatizo kusikufanye mnyonge au kuona haufai (ingawa kibinadamu **** wakati nilikata tamaa) but amini nakwambia ukijikubali WEWE NI BORA KABISA. Mimi pamoja na kuwa na tatizo langu nimekua mwanafunzi bora kitaaluma kuanzia sekondari, bachelor degree mpaka masters pale MUHAS kote nimekua nikatunukiwa best final year student. Je, tatizo la kusikia ni sababu ya kukata tamaa? HAPANA. Naamini kabisa tatizo hili haliwezi kuwa kikwazo kwako maana kwangu haijawa kikwazo (ukiachana na changamoto za kawaida za kijamii)

All in all pole sana, unayopitia i can feel you kutoka moyoni kabisa. Nimejisikia simanzi sana maana umenikumbusha changamoto nilizopitia.

NB: kama utaweza kujiajiri itakua poa zaidi, hapo you will set your own rules

cheers
 
But trust me my friend, with time tatizo linapungua. Now mtu hawezi jua kama nina tatizo labda akikaa na mimi kwa muda mrefu sana.

Zamani ilikua hatuelewani na mtu kabisa, but now miaka inavozidi kwenda hali inazidi kuwa better.
Ni nini ulifanya mpaka tatizo liwe linaenda linapungua ? Au kuna lifestyle ulibadili kama diet nk
 
Sikufanya chochote mkuu.

Ilifika mahali nikakubaliana na tatizo. Maana ilifika mahala tunatumia costs kubwa sana bila ahueni.

Nadhani pia ni genetics, mdogo wangu wa kike nae alipofika form two nae tatizo likaanza.

Nadhani kadri miaka inasogea tatizo linapungua. Maana mimi ni miaka almost 15 niko na tatizo
 
hazina msaada kabisa naona ni kama biashara za madaktari wa ENT na hospitali za masikio.
Mkuu, upo sahihi kabisa. Mimi baada ya kukutana na shida hiyo, ndugu walimshauri mzee tuje dar, hospital inaitwa EKENYWA, ENT akanisafisha masikio, then wakaniambia nirudi alhamis nionane na audiologist kwa ajili ya kupima usikivu, siku hiyo nikarudi wakanipima, then nikarudi tena kwa ENT, akasema hapo tujaribu hearing aids. Nikapewa namba ya muhusika.

Kuja kumtafuta muhusika, katuambia tumfuate Mlongazila Hospital, kufika kule ni jamaa wa audiology alinipima Ekenywa, akasoma tena ripoti yake, akaanza kuniandikia bei za hearing aid zitakazofaa, akasema kwa level yangu itakayofaa ni ya 1.4M za kitanzania, sawa tukamwomba jina la pharmacy au duka la vifaa tiba, jamaa aligoma kabisa kutupa jina na location. Akisema pesa tumpe yeye halafu atatuletea. Najua tulipigwa parefu tu, na hearing aid ndo hivyo tena.
 
Pole sana mkuu
Huko kote mimi nimepita pia.
 
Back
Top Bottom