Hali ya usikivu mdogo inavyonikosesha ajira/fursa

mwinuka2023

Member
Apr 29, 2023
26
56
Habari zenu wana jamvi natumaini wote ni wazima.

Bila kupoteza muda Niende kwenye mada kuu...Ni wazi kabisa kwamba Mimi nasumbuliwa na changamoto ya usikivu (tinnitus) "hali ya kusikia sauti mfano wa honi au kengele ndani ya sikio hali inayopolekea sauti kuingiliana na kushindiwa kuelewa kilichoongelewa na mtu anaekuongelesha kwa wakati huo hadi arudie tena na uconcetrate kwake kwa kuupuuzia sauti za ndani ya sikio".

Changamoto hii inaniepeleka Mimi kukosa Ajira sehem mbali mbali nikiomba kazi nikifika hatua ya usaili wa mahojiano nimekuwa nikiingia na presha kubwa mno hali inayopolekea kufeli interview wakishajua kama Nina shida hiyo wakati mwingine huwa naanza kwa kuwaeleza shida yangu ili wanifanye kama mtu mwenye uhitaji maalumu ili hata nisipoelewa swali waweze kurudia nilielewe lakini bado ni changamoto

Mwaka 2021 nilibahatika kupata kazi kiwanda kimoja kama DATA CLERK lakini mwaka huu nikakataliwa kurejea kazini licha ya kwamba tatizo langu linafahamika ofisi ya waajiri na OSHA lakini daktari mkuu wa kiwanda amenigomea kurudi kazini kusaini mkataba maana kazi ni ya msimu na kila mwaka mnaporejea lazima mfanye vipimo ndo muungie kazini miaka yote hiyo nimekuwa nikipita hatua zote na kupelekea kupangiwa eneo zuri kulingana na hali yangu.

Ni Rasmi sasa nimekuwa baba wa nyumbani sina pa kwenda kila kona ni majaribu nafsi yangu inaumia nikiamka asubuh nikiona wenzangu waliokuwa wananipitia kwenda kazi sasa wanakwenda peke yao Mimi nikiwa nimebaki nyumbani.

Ndugu zangu nirejee tena kwenu kwa mtu yoyote humu mahala popote mwenye connection ya kazi aina yoyote ile basi tusaidieane asihofie hali yangu kwa kuwa sio ya kutisha ni tinnitus tu ndo inayonitesa binafsi Nina Diploma ya ukutubi na uhifadhi wa nyataka (Ordinary Diploma in Library, records and information studies) Nina uzoefu mzuri na wa muda mrefu mbali na kazi kuhusu fani yangu nimehudumu kama Quality Control QC, office attendant, warehouse attendant, Leaf Account Clerk and Greenleaf Data Clerk katika viwanda tofauti tofauti(TTPL,21st century textile LTD,Allionce one international) tangu 2015.

Mbali na hapo kazi yoyote ile halali nafanya naomba msaada wenu wapendwa..Asanteeni na Mungu awabariki

Mwinuka Frank D.

Morogoro
Chamwino-Shule street
House no 060
Simu:0654204670
0744204670
Email.Frankdmwinuka@gmail.com
 
Pole kaka !

Hali hyo imekuwa ni changamoto sana na wengi inawakumbuka hata siku nne kulikuwa na uzi kama wako mtu akiwa na changamoto kama hyo...

Ndugu yangu usikate tamaa maana ndo ulivyo tinnitus ni hatar kwa sababu matibabu yake ni pata potea utaoewa madawa kama neuroton,neuro support hata device ola finally ni mtihani ..

Usikate tamaa riziki yako ipo tu inshallah.!
 
Habari zenu wana jamvi natumaini wote ni wazima.

Bila kupoteza muda Niende kwenye mada kuu...Ni wazi kabisa kwamba Mimi nasumbuliwa na changamoto ya usikivu

Morogoro
Chamwino-Shule street
House no 060
Simu:0654204670
0744204670
Email.Frankdmwinuka@gmail.com
Pole sana Mwinuka.

Kwani umefanyiwa vipimo na wataalam? Umefanya mipango yoyote ya kupata vifaa vya kusaidia kusikia (hearing aids)?
 
Pole sana Mwinuka.

Kwani umefanyiwa vipimo na wataalam? Umefanya mipango yoyote ya kupata vifaa vya kusaidia kusikia (hearing aids)?
Nilishapita huko kote mara ya mwisho nilipata hearing aids za msaada kutoka taasisi ya starkeys foundation lakini sikuweza kutumia nilirudi kwa Daktar TMJ akaniambia hazinifai kwasababu tatu langu sio kwamba sisikiii hapana ipa moja frequency zimeshuka hivo kuna muda mishipa ya fahamu inashindwa kutafsiri sauti hadi mtu arudi niwe makini pili ni hiyo tinnutus hivo akaniambia hivo vidude ni kwa ajili ya viziwi tu ambao hawasikii kabisa mimi sijafika huko natakiwa kutafuta vinavyoongeza frequency na kuzuia tinnittus hivo tu.
 
Pole kwa changamoto!!
Nakushauri utumie hearing Aids zinaweza kupa msaada sana hasa kwenye eneo la kazi na kwenye kufanya interview!

Back
Top Bottom