Hali ya Stendi ya Bukoba inasikitisha sana

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Kinachoendelea kwenye jimbo la Bukoba ni hatari tupu nimekaa kimya kwa muda ila hali ya stendi inasikitisha sana kuna uongozi wa Wilaya na Mkoa lakini hali inatisha.

Najua kunahatua zisizoridhisha zinaendele stendi mpya lakini pia Mkurugenzi wa mji alihaidi kufanyia marekebisho stendi hii mpaka sasa hali inazidi kuwa mbaya uku wasiojulikana wakimwaga uchafu katikati ya stendi kuziba mashimo bila kuusambaza na matokeo ndio kama mnavyoona hali hii mpaka lini? @⁨Neema Lugangira (MP) 2020-2025⁩ @⁨Mh. MB. Byabato Bukoba⁩ mbunge wa jimbo, @⁨Njovu Mkurugenzi Bukoba 2022⁩ mkurugenzi wa mji wa Bukoba mmeridhika na hali hii?

Sisi ni watu sio nguruwe tuondolee matope na madimbwi katikati ya mji kwa hali hii mnaweza kutuletea magonjwa ya mlipuko kutokana na uchafu huu. Katikati ya ugonjwa wa Murbug katikati ya mkoa kuwa wa mwisho kwa umaskini na utapia mlo na miundombinu mibovu bado hali ya jimbo na mkoa wa Kagera kiujumla sio nzuri

Katikati ya taarifa ya upotevu wa matillion ya shilingi yaliyoibuliwa na CAG uku watu tukiwa hoi na makovu ya wizi wa kodi zetu bado mnaendeleza ubabe nashindwa kujua ni kitu gani mnatafuta kwetu.

Narudia ushauri wangu kwamba BE ASHAMED Tuondolee uchafu katikati ya mji.

By Mujun Katikabakama sauti ya wasio na sauti.

 
Back
Top Bottom