Hali ya nchi yawatisha maaskofu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali ya nchi yawatisha maaskofu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 24, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,480
  Likes Received: 81,771
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Hali ya nchi yawatisha maaskofu
  • Wakiri viongozi kuwatelekeza wananchi

  na Datus Boniface
  Tanzania Daima  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  MAASKOFU wakuu wawili wa makani ya Anglikana na Kilutheri Tanzania, wameonyesha huzuni na wasiwasi wao juu ya mwelekeo mzima wa taifa kutokana na mambo ya kusikitisha na kutikisa nchi kwa sasa.

  Akizungumza jana katika ibada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Kanisa la Usharika wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, alisema taifa linaelekea kubaya kutokana na baadhi ya watu kuwa tayari hata kuua wenzao kwa ajili ya mali na madaraka.

  Alisema kuwa hali imekuwa mbaya zaidi baada ya kujitokeza kundi la baadhi ya viongozi waliopewa dhamana ya uongozi kutowajali kabisa wananchi na kuwatumikia kama walivyoahidi na kuaminiwa wakati wakitafuta nafasi za uongozi.

  Dk. Malasusa alionyesha kusikitishwa kwake na hatua aliyoiita ya kuchafuana majina na heshima kwa baadhi ya viongozi ili mmoja aonekana msafi katika jamii badala ya kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi.

  Katika hilo, Malasusa alikemea vikali waumini wa Kikristo wanaoshiriki katika matendo maovu yakiwemo ya kutowatumikia watu ipasavyo na kuongeza kuwa hatanyamaza kuwakemea hadi watakapobadilika na hivyo kuiokoa nchi na janga la maangamizi.

  Alisema ni wajibu wa Wakristo wenye dhamana ya madaraka kuiga mfano wa Akida aliyejitoa kumsaidia mfanyakazi wake aponywe na Yesu. Alisema kwa jinsi hali ya taifa ilivyo, ni wajibu wa viongozi wa Kikristo wenye madaraka kuiga mfano wake na kuwatumikia wananchi.

  “Akida ni mfano wa mtu mwenye cheo ambaye alidiriki kujitoa kwa ajili ya kumsaidia mfanyakazi wake aponywe na Yesu, kwa jinsi taifa lilivyo leo ni jambo gumu kwao kuwajali wengine (wananchi),” alisema.

  Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk Valentino Mokiwa, amesema ana huzuni kubwa kutokana na taifa kukabiliwa na mambo mazito likiwemo suala la ukosefu wa umeme, wakati huu taifa linapotimiza miaka 50 ya uhuru wake.

  Akizungumza katika ibada ya harambee ya ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Askofu Mkuu John Sepeku, Buza jijini Dar es Salaam jana, Mokiwa alisema hali ya taifa inaleta hofu kwa vile suala zima la umeme limeleta mtikisiko mkubwa kwa uchumi wa taifa.

  Akizungumzia juu ya maendeleo ya elimu nchini, kanisa hilo limeitaka serikali kurudisha shule zote za dini ilizozitaifisha kabla ya Azimio la Arusha, ili zisaidie kuleta maendeleo ya elimu nchini.
  Askofu Mkuu Mokiwa aliongeza kuwa serikali ilitumia nguvu kuchukua shule za dini zikiwemo zile za Kikristo na Kiislamu na sasa umefika wakati wa kuzirudisha kwa wamiliki wa mwanzo kwa vile kuna shule za serikali.

  Askofu huyo alienda mbali zaidi na kusema kuwa kitendo kilichofanywa na Serikali wakati huo ingekuwa nchi za nje wangepelekana mahakamani, lakini kwa kuwa Tanzania ni nchi ya watu wapenda amani, wameamua kutumia busara kuzidai.

  Askofu Mokiwa alisema Kanisa la Anglikana ndilo lililokuwa na shule nyingi ukilinganisha na madhehebu mengine na zilipokea wanafunzi bila kujali ni wa dhehebu gani.
  Alizitaja shule hizo kuwa ni pamoja Sekondari za Minaki, Chidya, Loleza, Mazengo na Chuo cha Ualimu Korogwe na Ndwika. Aidha, kulikuwa na Hospitali za Mkomainda, Hospitali Teule ya Muheza na ile ya Mvumi Mission.

  Alisema kutokana na kupokwa shule hizo dayosisi hiyo mpaka sasa hivi ina shule mbili tu ikiwemo Shule ya Msingi ya Mtakatifu Augustino ambayo inafundisha masomo yake kwa lugha ya Kingereza na shule hiyo ya Sekondari ya Askofu Mkuu John Sepeku ambayo ina kidato cha kwanza hadi cha nne.
  Hata hivyo alisema kurudishwa kwa shule hizo kwenye taasisi za dini ikiwemo zile zilizokuwa zikimilikiwa na dini ya Kiislaam, zitasaidia kuleta changamoto kwa shule za Serikali kutoa elimu iliyo bora tofauti na sasa.

  Naye Waziri Mkuu aliyejiuzulu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa, aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, alizitaka taasisi za dini kuwekeza katika vyuo vya ufundi.
  Lowasa alisema watu wengi wanakimbilia kuwekeza katika shule za sekondari na kusahau kwamba kuna wale ambao wakimaliza kidato cha nne hawana pa kwenda ambapo vyuo kama hivyo vingekuwa ni kimbilio lao.

  “Jamani vyuo vya ufundi ni muhimu sana kwa sasa, kwani takwimu zinaonyesha kuwa vijana wengi wameishia kidato cha nne na wanazurura mitaani, lakini hawa wangepelekwa katika vyuo vya ufundi, ni wazi kwamba tungezalisha ajira nyingi,” alisema.

  Lowasa alirudia usemi wake kuwa tatizo kubwa la ajira kwa vijana hapa nchini ni bomu ambalo linaweza kulipuka siku yoyote na kuifikisha nchi pabaya iwapo juhudi za makusudi zisipochukuliwa kukabiliana na janga hilo.
  Katika harambee hiyo, Lowassa na rafiki zake walichangia jumla ya shilingi milioni 20. Aidha alishiriki kuendesha mnada ulioweza kukusanya jumla ya shilingi milioni 126.941 kati ya hizo milioni 60 zikiwa taslimu na zilizobaki zikiwa ni ahadi.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  duh!!! lowasa
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Bakwata watasemaje hapa ? Au Tamko lao lazima kulichuja kwanza ?Au bakwata watasikika kwa Chadema na Kanisa katoliki ?
   
 4. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #4
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Jamani eeeeeeehhh, nani alikubali kujiuzulu kwa Lowasa jamani??? Nakumbuka jakaya hakuijibu barua ya lowasa kujiuzulu, alivunja bunge na kumtimua uwaziri mkuu. Tutamuitaje mtu aliyejiuzulu kw akutangaza tu nia ya kujiuzulu wakati bosi wake hajakubali?

  Ina maana mtu akitangaza nia ya kugombea ubunge basi tumuite mbunge kwa kuwa ametangaza nia?

  Si mpaka achaguliwe? sasa kama JK angekubali ile barua ya lowasa na akina bangusilo kutaka wajiuzulu, angewajibu na kisha angejaza nafasi wazi, lakini hakujibu mtu na badala yake alivunja baraza la mawaziri na KUMTIMUA LOWASA.

  Kwa hiyo lowasa sio wasiri mkuu aliyejiuzulu, ni ALIYEWAHI KUWA WAZIRI MKUU........
   
 5. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Tunawashukuru viongozi wetu hawa kwa kuliona hilo. Hakuna sababu yoyote ya watu kuacha kufanya shughuli za maendeleo na badala ya kupaka wengine matope na kuponda kila ljambo jema ifanywalo na serikali.
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,060
  Likes Received: 6,507
  Trophy Points: 280
  Hawa wakuu wa dini wajitahidi sana kulichunga kundi la Bwana
  haya ya siasa siyo yao
  ya MUNGU mpeni MUNGU ya kaisari mwacheni ahangaike nayo kaisari mwenyewe.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Lakini Serikali ya Tanganyyika si wana MOU waliosaini na kanisa.

  sasa inakuwaje tena
  .
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Duu EL chaguo la yesu 2015!
   
 9. O

  Omr JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa mapadri na mashehe siasa wanaitakia nini? Wao wana yao na yanawashinda. Sikuhizi kila mtu amekua mwanasiasa. Akipewa mic basi lazima alete siasa. Tumeaza kuwa kama wananchi Ghana sasa.
   
 10. Nish

  Nish JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 732
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  maaskoofu hawana lolote warudishe kwanza hela za memorundum of understanding
   
 11. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 160
  Hawa viongozi wa dini wasituzuge wao na UFISADI, madawa ya kulevya kitu kimoja. Jukumu lao ni kuwaasa waumini wao kuachana na ufisadi ndipo maendeleo yawepo. Mie siwafagilie kitendo cha kumtumia Lowasa kwenye harambee ya kukusanya michango. Huyu Lowasa kwenye CCM tumeshampa low profile hivyo anaibukia makanisani na misikitini!!
   
 12. K

  Kisamo Member

  #12
  Oct 24, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tatizo la watu wenye majibu ya chapchap kama hilo ni kwamba hamtafakari mambo na kutumia elimu mliy nayo kuangalia mambo. Yaani unataka kuwadanganya watu kwamba Wakristo wana MOU na serikali? Kama unayo, iweke hapa jukwaani, kwa vile watu wanajua kusoma
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hizo kauli sio za maasikofu ni uzushi tu zingekuwa za maasikofu kama zingetolewa na baraza la maaskofu Tanzania kwa ujumla wao. Hizo ni kauli za viongozi wa dini na madhehebu yao ya KKKT na Anglikana ambao sio wawakilishi wa baraza la maaskofu
   
 14. d

  dotto JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mwasapila design!!
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Lowassa alikuwepo napata kigugumizi inawezekana sio kauli za maaskofu bali za Lowassa kwani katika siki za karibuni Lowassa naye amekuwa analalama kuwa serikali haifanyi maamuzi magumu na mara ajira kwa vijana wakati yuko ndani ya vyombo vyenye haki ya kutoa maamuzi kama NEC -CCM, bungeni angeweza kutoa hoja binafsi ya ajira kwa vijana, yeye na kikwete hawakukutana barabarani angeweza kwenda Ikulu kumshauri mwenzie na rafiki yake wa muda mrefu..... anazunguka nje ya system kummaliza mwenzie.....vuguvugu la Urais 2015
   
 16. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 1,522
  Trophy Points: 280
  Ndugu yangu naomba nikusaidie kidogo kufikiri, hawa tunaowaita wanasiasa pia ni wa madhehebu ya kikristo, kiisilamu na hata wasio na dini pia, mathalani ww ni mkristo, kukicha wanakuandika kwa ufisadi (kweli/uongo), mchungaji akikemea utasema anafanya ama anataka kuwa mwanasiasa hapo, hivyo tuache wanasiasa wafanye watakavyo? wachungaji na/ama mashehe nao wanahaki kikatiba kwa sababu ni watanzania kuchagua/kuchaguliwa ktk nafasi za uongozi wa nchi hii, na kujadili pia. MNAPOAMINISHWA NA WENYE DHAMANA KWAMBA VIONGOZI WA DINI WASIONGELEE SIASA MJIONGEZE KUFIKIRI, OTHERWISE KICHWA CHA NINI SASA KAMA HUWEZI KUKITUMIA KUFIKIRI SI HERI UBAKI NA SHINGO PEKEE
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Gazeti lenyewe Tanzania Daima linavutia upande wake kwa lengo lilelile na dhamira ileile ndio maana suala la maaskofu wachache limefanywa kuwa ni tamko la Baraza la Maaskofu Tanzania kwa madhumuni yaleyale ya kuupotosha umma
   
 18. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Maneno ya maaskofu ni mazuri sana, ni maneno mazito kwa ajili ya taifa letu na kwa kweli yanawalenga viongozi wote lakini kichwa cha habari ni kichokonozi hakiko kwa ajili ya habari yenyewe ya maaskofu hao bali kwa lengo lingine
   
 19. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Batu bale bale
   
 20. joseeY

  joseeY Senior Member

  #20
  Oct 24, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tanzania imebarikiwa kwa kila aina ya rasilimali za kuifanya kua taifa la uchumi wa kati kama indonesia,taiwa ni nk tatizo rasilimali akili tu ndio inayo tukwamisha.fikiria kabisa mtu anasifu jambazi lowasa
   
Loading...