Hali ya Mtwara mchana huu

Hali ya Mtwara mchana huu

JEMEDARI .H.

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Posts
341
Reaction score
63
Wana JF, updates kutoka Mtwara zinasema wananchi wameitikia wito wa kutofanya kazi yeyote na kwamba ofisi za serikali tu ndio zinatoa huduma huku kila mwananchi akiwa nyumbani kwake.

Hali ya usalama katika mji wa mtwara bado jeshi la polisi wakishilikiana na jeshi la wananchi j.w wanaendelea kufanya dolia ili kuzuia aina yeyote ya fujo inayoweza kujitokeza kutoka kwa wananchi wa mtwara ambao wanasubiri tamko la serikali kuhusu kuwepo au kutokuwepo mradi wa kutandika bomba la gas kwenda dar es salam kupitia wizara ya nishati na madini inayotegemewa kuwasirisha budget yake siku ya jumatatu.

Maeneo ya BIMA, Bank ya N.M.B. na CCM mkoa hali si kama kawaida kwani hakuna huduma za kijamii kama usafiri wa bajaji,taxi na boda pia maduka mahoteli yamefungwa kwa kuhofia vurugu hali ni hivyo hivyo katika maeneo ya soko kuu na stand kuu hakuna huduma ya kuuza vyakula,maduka na huduma ya mabasi kwenda mikoani.

Baadhi ya abiria waliojitokeza kupanda kwenye basi moja la kwenda vijijini walishushwa na kundi kubwa la vijana waliokusanyika stand hapo,pia ukionekana unapakia abiria kwenye boda au bajaji kundi hilo linazuia,licha ya magari ya FFU na JW kuendelea kuzunguka vijana wanaonekana kutokuyaogopa bali wanaendelea kusimama ktk makundi huku wakishangilia.

Lengo kuu la wanamtwara kusimamisha huduma za kijamii siku ya leo wanadai ni kufikisha ujumbe kwa serikali kuacha mala moja mpango wake wa kujenga bomba la gas asilia kupeleka gas Dar kwani wao wanataka mtwara iwe special energy zone,ambayo shughuli zote za production, procesing na exportation zifanyike kupitia bandari ya mtwara,na hata umeme utoke kwa njia ya nguzo kwenda Dsm

Naomba kuwasilisha moja kwa moja toka eneo la tukio

MADUKA YA BIMA YOTE CLOSED:
ao15om.jpg


JUCTION YA BIMA HAINA WATU KABISA, HATA NMB IMEFUNGWA:
2wfkdhg.jpg


KWA MBALI UTALIONA GARI YA ASKARI IKIRANDARANDA...KOKOBICHI, KIMYA KABISA YANI
33v2lmr.jpg
 
Ebu fafanua, kuna nini hasa?
Tafuta kuna thread ya jana inahusu MTWARA KWANZA, GESI HAITOKI. Kwa ufupi, wakazi wamehamasishwa kusikiliza kauli ya serikali kuhusu geni iliyopatikana mikoa ya kusini leo kuanzia saa 3 wakati bajeti ya wizara husika itakapokuwa inasomwa bungeni.
 
wananchi wapate fursa ya kutizama bunge, wafahamu hatma ya gesi ili hatua zichukuliwe "na wananchi wenyewe"

mbona leo ni kuna muendelezo wa mjadala wa bajeti ya uchukuzi ya dr.mwakyembe..nani kawaambia leobajeti ya wizara ya nishati na madini...ukweli hili jambo la gas kuna watu wako nyuma ndio wanahamamsisisha wananchi vyema serikali ikawa makini na hawa watu wachache wanao chochea vurugu baada ya mshakamano na kuwaeleza wananchi ukweli.....
 
Tafuta kuna thread ya jana inahusu MTWARA KWANZA, GESI HAITOKI. Kwa ufupi, wakazi wamehamasishwa kusikiliza kauli ya serikali kuhusu geni iliyopatikana mikoa ya kusini leo kuanzia saa 3 wakati bajeti ya wizara husika itakapokuwa inasomwa bungeni.

Nashukuru Mkuu, nimeiona unajua wengine tunashinda mashambani, kiujumla hili suala Serikali wasilichukulie kirahisi, jamaa wa Mtwara wako serious na hii issue
 
i like this ipo siku ata tanga wataamka na kuhoji kilimo cha mkonge unavowanufaisha wananchi na vipi ahadi ya rais kuwa tanga itakua mji wa viwanda tanzania? I THINK IT IS TIME NOW TO OTHER REGIONS TO FOLLOW MTWARA'S FOOTSTEPS.OVER.
 
wananchi wapate fursa ya kutizama Bunge, wafahamu hatma ya Gesi ili hatua zichukuliwe "na wananchi wenyewe"
Kweli Mungu anataka kuikomboa Tanzania dhidi ya Shetani .........................................
 
hatutaki kuletewa habari nusunusu humu jf kama habari yako bado haija kamilika hakuna umuhimu wa kuipost humu.
TUPE SASA MKASA MZIMA WA HUKO MTWARA CZ UJATUPA PICHA KAMILI YA KWANN KUNA HALI HIYO HUKO MTWARA?
 
CCM watakata umeme ili mshindwe kusikiliza hotuba ya wizara...
 
Ni muda wa kila mmoja wetu kuamka na kusimama kuitetea mali yake ili sote tuugawane umasikini huu sio wachache tuu ndio waufaidi kama ilivyokuwa kule kilwa

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
ni kwa mtwara mjini huku wilayani shughuli zinaendelea kama kawaida.
 
Tuleteeni habari kwa utimilifu wake wakuu hasa The Big Show na mwenzio Nsizigwa.tuwekeeni hata picha za maduka yalivyofungwa,jinsi mitaa haina watu na mambo ambayo yatatupa uhalisia wa jambo lenyewe.ila ushauri wa bure mjiandae kwa kuwasha generator pia,hata hivyo sin uhakika kama bajeti ya wizara ya nishati itasomwa leo.
 
Ngoma inogile, aminia wamakonde. swali sasa hayo mabomuwaliyopeleka watayapiga wapi?[/QUOTE]

Ukizingatia hawajazoea kuona wananchi WAMETULIA (siyo kuandamana).........Itabidi mzigo wauweke AKIBA!!!!
 
Wao wakitaka wakae hata mwaka bila kufanya kazi hamna atakae wasumbua.
 
mbona leo ni kuna muendelezo wa mjadala wa bajeti ya uchukuzi ya dr.mwakyembe..nani kawaambia leobajeti ya wizara ya nishati na madini...ukweli hili jambo la gas kuna watu wako nyuma ndio wanahamamsisisha wananchi vyema serikali ikawa makini na hawa watu wachache wanao chochea vurugu baada ya mshakamano na kuwaeleza wananchi ukweli.....
Na hao watu wana nguvu sana na wanakubalika huko Mtwara. Ndio demokrasia huyo.
 
Back
Top Bottom