Hali tete mgogoro wa wakulima, Meneja wa shamba achinjwa, Wapiga mawe Mbunge wa Babati Vijijini(CCM) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali tete mgogoro wa wakulima, Meneja wa shamba achinjwa, Wapiga mawe Mbunge wa Babati Vijijini(CCM)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 2, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Wednesday, 01 June 2011 21:13
  Joseph Lyimo, Babati

  HALI bado ni tete kwenye Bonde la Kiru, Wilaya ya Babati, mkoani Manyara baada ya Meneja wa Shamba la Kampuni ya Kiru Rift Valley, Sifael Jackson kuchinjwa na kisha kukatwakatwa kwa mapanga na kutenganishwa mwili na kichwa chake.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Parmena Sumary alisema jana kwamba Jackson aliuawa juzi jioni na kwamba mbali ya kuchinjwa, alikatwa mguu wa kushoto na mkono wa kulia.

  Alisema kwamba marehemu alifikwa na mauti alipokuwa akitokea shambani kuelekea Babati Mjini. Alisema kuwa Jackson alikuwa na gari aina ya Toyota Hilux, Pick Up na alipofika katika Kijiji cha Imbiriri, Kata ya Kiru, alikuta mawe yamepangwa barabarani hivyo kumzuia kupita na gari hilo.

  “Baada ya kuona hali hiyo alilirudisha gari nyuma, lakini likamshinda, akateremka chini ndipo kundi la watu lilipojitokeza na kuanza kumkimbiza na kumkatakata kwa mapanga na kumwua kikatili papo hapo,” alisema Kamanda Sumary.

  Alisema mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi kwenye Hospitali ya Mrara Mjini Babati na unatarajiwa kukabidhiwa kwa ndugu zake wakati wowote kwa ajili ya mazishi.

  Kamanda Sumary alisema hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kwa kuhusika na tukio hilo na kwamba polisi inaendelea na uchunguzi. Alitoa wito kwa wakazi wa Kiru kutoa ushirikiano endapo wanawatambua wahalifu wa tukio hilo la mauaji.

  Mmoja wa wawekezaji wa eneo hilo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini alisema kwamba, juzi wakulima hao walimrushia mawe Mbunge wa Babati Vijijini (CCM), Virajilal Jituson akiwa kwenye gari lake na kuvunja vioo viwili: “Juzi hiyo hiyo, wakulima hao pia waliingia kwenye shamba la mbegu za mahindi la Kampuni ya Krishna linalomilikiwa na Babu Hatia na kuteketeza kwa moto ekari 10 na ekari nyingine 10 za shamba la miwa.”

  Mgogoro wa wawekezaji na wakulima wadogo wa Bonde la Kiru ni wa muda mrefu. Januari 27, mwaka huu mali mbalimbali zikiwamo viwanda, mashamba na nyumba zenye thamani ya mamilioni ya shilingi za wakulima wakubwa, Suresh Odedra na Mukesh Ogan zilichomwa moto huku Jituson akichomewa moto shamba lake la miwa.

  Alisema vurugu na mauaji vinavyoendelea hivi sasa siyo ishara nzuri: “Siyo kitendo kizuri kwa kweli, leo imekuwa kwa Jackson kesho inaweza kuwa kwangu au kwa mwekezaji mwingine, hali hii inatisha, tunataka kuziona jitihada za serikali kumaliza mgogoro huu.”

  Akizungumza kwa simu jana mchana, Jituson alisema hali katika Bonde la Kiru kwa sasa ni tete na kwamba wakati huo alikuwa katika mkutano wa hadhara eneo la bonde hilo kujadili matukio hayo.

  Mwanzoni mwa Machi mwaka huu, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwaagiza mawaziri watano kufika Bonde la Kiru na kuzungumza na wawekezaji pamoja na wananchi juu ya njia muafaka za kumaliza mgogoro wa mara kwa mara baina ya wakulima wadogo na wakubwa.

  Mawaziri waliofika walikuwa wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanry.

  Mawaziri hao walifanya mkutano mkubwa wa hadhara uliojumuisha wananchi na wawekezaji na kisha kuwaagiza viongozi wa mkoa huo kuunda tume ya usuluhishi kabla ya Machi 23 mwaka huu. Hata hivyo, tume hiyo haijaundwa na mgogoro huo unaendelea kupamba moto.

  Baadhi ya wakulima wadogo wa Vijiji vya Kiru Six, Imbiriri, Kiru Diki na Kimara, Kata ya Kiru wanataka wawekezaji hao waondoke na kuwaachia wenyeji maeneo yao
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Wakati wa Utawaka wa Mwl. Nyerere hatukuwa na wawekezaji walafi wanaopendelewa na serikali kuchukua Ardhi za wananchi.

  Kulikuwa na Wawekezaji walipewa Maeneo ya Maporini ambapo wananchi hawaendi mfano mzuri ni Hanang ambapo kulikuwa na Mashaba ya Wakanada ya Ngano... hakuwapa maeneo wananchi wanaishi kama sasa.
   
 3. The Mockingjay

  The Mockingjay JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  We have a bigger problem than what we think.
  Haya ndio yaleyale ya Barrick Tarime. Except this time wananchi wameua mfanyakazi wa mwekezaji.

  Hizi kesi ziko nyingi sana siku hizi sababu watumishi wa serikali na middlemen wanawadanganya wawekezaji na wananchi. and ofcourse wananchi lazima wamshambulie mwekezaji na mwekezaji inabidi ajikinge sababu wote wawili wanaona wanahaki ya hiyo sehemu.

  Land ownership na reforms lazima ziwe very clear. Wananchi lazima wapate haki zao na wawekezaji vilevile. They can coexist in harmony kama mipango iliwekwa sawa na kwa haki pande zote mbili.
   
 4. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Kiru ni kwamba wawekezaji ni wakatili mno,hao wawekezaji na walinzi wao ni watu wakatili sana,ilikuwa miaka ya 2002-2003 ng'ombe wa mwananchi hata akiingia kwa bahati mbaya kwenye shamba la miwa la mwekezaji ng'ombe au mfugaji anapigwa risasi,ilishatokea mfugaji alipigwa risasi wananchi wkapiga yowe,walichoma mashamba,waliwachinja vibaraka wa hao wahindi,wahindi wao wenyewe waliuawa kama 5 hivi,watoto na wake zao walibakwa.kwa hiyo tatizo ni ukatili wa wawekezaji
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,946
  Trophy Points: 280
  nchi haitawaliki tena
   
 6. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Reactive govt, mpaka watu wachinjane ndo migogoro inapatiwa ufumbuzi! tume ya usuluhishi haijaundwa mpaka leo, yaani wakisha toa maagiza then hakuna anaefatilia, uwajibikaji nada! Taifa linaangamia kwa watu kukosa maarifa!
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  piga nikupige ndiko serikali inakotupeleka
   
 8. s

  sawabho JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Tatizo hapa ni kuchelewa kutatatua matatizo ya wananchi. Ina maana viongozi hawakusomea uongozi na utawala. Wanasubiri tatizo litokee, ndipo Tume iundwe kuchunguza na kushauri nini kifanyike.
   
 9. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  uwekezaji katika kilimo lazima ufanyike kwa makini mno. Tukumbuke ardhi pekee ndo rasilimali ya masikini, ndiyo kila kitu kwa masikini. Kama tunataka kujua kama masikini ambao wamedharaulika kuwa hawazijuwi haki zao basi tucheze na swala la ardhi ndo tutajua kuwa wao ni werevu zaidi ya wenye Phd.

  Tunasema kila leo kuwa nchi hii imekosa uongozi ndiyo maana mambo yanaenda kama tunavyoyaona sasa.
  Anahitajika mtu mwenye uwezo wa kusimamia mambo haya boldly bila kumtetemekea mwekezaji au mkulima wala mfugaji.
  Sheria ya kwamba ardhi ni mali ya umma na hivyo Raisi ndo owner haiwaingii watu akilini. Masikini anajua eneo analoishi ni mali yake haijalishi kama kuna hii sheria.
  Swala na kufikiri kuwa kutojua sheria basi si utetezi basi hawa masikini hawaijui hii sheria japo ipo kwenye katiba na viongozi wanachukulia mdhaha na kudhani kuwa wanaweza kuitumia sheria hii kirahisi tu k kuwanyang'anya hawa masikini wakati wowote wanapoihitaji kuwapa wawekezaji.
  Sheria hii haiwezi kutumika kama ilivyo tu kwa sababu sheria hii imewakuta watu tayari wakitumia hii ardhi kwa kufuata utaratibu waliokuwa nao kabla ya kuwepo kwa jamhuri ya Tanzania na wamekuwa wakirithishana kizazi hadi kizazi.

  Kama tunataka sheria hii ifanye kazi ni lazima tutambue kwanza umiliki wa ardhi ya masikini hawa na ardhi ambayo itabaki ndo tunaweza kuifanya kuwa ni mali ya umma.

  Naupongeza mradi wa majaribio wa kuwamilikisha ardhi maskini kule vijijini ambao nadhani utakuwa ni suluhisho la migogoro mingi ya ardhi.

  Changamoto iliyopo pia ni kuweza kuhifadhi ardhi kwa ajili ya kuwapa watu wananoongezeka. Hapa nadhani kunahaja ya kutenga maeneo ya ziada kwa kila kijiji ili yabaki kwa matumiza ya ongezeko la watu. Hivi sasa viji vinauza maeneo yote na kubaki bila akiba yoyote kitu ambacho kitakuja kuleta mgogoro mkubwa hapo baadaye.

  Mwisho narudia kusema hatuna uongozi uliotayari kuleta suluhisho la migogoro ya ardhi nchini. Ukienda katika mahakama za ardhi leo utakutana na kesi za kipuuzi kabisa na nyingi zinasababishwa na uongozi wa serikali za vijiji ,kata,wilaya na hata taifa.

  Tunahitaji mtu makini pale juu ili kuleta mabadiliko ya dhati katika swala hili tete la ardhi.

  Tunaomba wapinzani watuambie wao wanajiandaa vipi kuyakabili haya matatizo pindi watakapo ingia madarakani. Hili ndo linawagusa wapiga kura wengi zaidi kuliko jambo lingine lolote.

  CDM wake up and provide directives maana tunaona magamba wanafuata maelekezo yenu.

  Mungu rejesha amani yetu inayotoweka, tusamehe kwa kutokukusikiliza wewe tunapotafuta viongozi wa nchi yetu.
   
 10. N

  Nguto JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 635
  Trophy Points: 280
  Nabii Isaya alishatabiri kuwa itafika wakati nchi na chi zitapigana, watu watapigana wenyewe kwa wenyewe, ndugu kwa ndugu nk. Hii ni hatari!!1 Tunauana wenyewe kwa wenyewe kisingizio uwekezaji!!!!!!!!
   
 11. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni uongo wa viongozi wetu,kama mwekezaji na wananchi walikubaliana kutekeleza miradi ya maendeleo then mwekezaji hafanyi hivyo hapo hakuna muafaka wala kuunda tume.watekeleze ahadi zao na wawaheshimu wananchi hakutakuwa na fujo mkubwa.mwekezaji ni raia wa wapi?kama ni wahindi fujo hazita isha.
   
 12. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Viongozi wa nchi hii wengi ni wababaishaji. Tume iliyotakiwa kuundwa tangu Machi, 2011 haijaundwa mpaka leo. Hakuna ufuatiliaji. Acha wananchi wachukue sheria mkononi wameshoshwa. RIP Sifael Jackson, viongozi wako ndiyo wamekuua.
   
 13. p

  politiki JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Ulitegemea wananchi wafanye nini ardhi yao inaponyanganywa na kupewa wageni wakati huo wenyeji wakiangaika kutafuta sehemu ya kulima.
   
 14. k

  kakin Member

  #14
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dah safi sana natamani halii hii iendelee ifike tanzania nzima
   
Loading...