nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Wednesday, 01 June 2011 21:13
Joseph Lyimo, Babati
HALI bado ni tete kwenye Bonde la Kiru, Wilaya ya Babati, mkoani Manyara baada ya Meneja wa Shamba la Kampuni ya Kiru Rift Valley, Sifael Jackson kuchinjwa na kisha kukatwakatwa kwa mapanga na kutenganishwa mwili na kichwa chake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Parmena Sumary alisema jana kwamba Jackson aliuawa juzi jioni na kwamba mbali ya kuchinjwa, alikatwa mguu wa kushoto na mkono wa kulia.
Alisema kwamba marehemu alifikwa na mauti alipokuwa akitokea shambani kuelekea Babati Mjini. Alisema kuwa Jackson alikuwa na gari aina ya Toyota Hilux, Pick Up na alipofika katika Kijiji cha Imbiriri, Kata ya Kiru, alikuta mawe yamepangwa barabarani hivyo kumzuia kupita na gari hilo.
Baada ya kuona hali hiyo alilirudisha gari nyuma, lakini likamshinda, akateremka chini ndipo kundi la watu lilipojitokeza na kuanza kumkimbiza na kumkatakata kwa mapanga na kumwua kikatili papo hapo, alisema Kamanda Sumary.
Alisema mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi kwenye Hospitali ya Mrara Mjini Babati na unatarajiwa kukabidhiwa kwa ndugu zake wakati wowote kwa ajili ya mazishi.
Kamanda Sumary alisema hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa kwa kuhusika na tukio hilo na kwamba polisi inaendelea na uchunguzi. Alitoa wito kwa wakazi wa Kiru kutoa ushirikiano endapo wanawatambua wahalifu wa tukio hilo la mauaji.
Mmoja wa wawekezaji wa eneo hilo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini alisema kwamba, juzi wakulima hao walimrushia mawe Mbunge wa Babati Vijijini (CCM), Virajilal Jituson akiwa kwenye gari lake na kuvunja vioo viwili: Juzi hiyo hiyo, wakulima hao pia waliingia kwenye shamba la mbegu za mahindi la Kampuni ya Krishna linalomilikiwa na Babu Hatia na kuteketeza kwa moto ekari 10 na ekari nyingine 10 za shamba la miwa.
Mgogoro wa wawekezaji na wakulima wadogo wa Bonde la Kiru ni wa muda mrefu. Januari 27, mwaka huu mali mbalimbali zikiwamo viwanda, mashamba na nyumba zenye thamani ya mamilioni ya shilingi za wakulima wakubwa, Suresh Odedra na Mukesh Ogan zilichomwa moto huku Jituson akichomewa moto shamba lake la miwa.
Alisema vurugu na mauaji vinavyoendelea hivi sasa siyo ishara nzuri: Siyo kitendo kizuri kwa kweli, leo imekuwa kwa Jackson kesho inaweza kuwa kwangu au kwa mwekezaji mwingine, hali hii inatisha, tunataka kuziona jitihada za serikali kumaliza mgogoro huu.
Akizungumza kwa simu jana mchana, Jituson alisema hali katika Bonde la Kiru kwa sasa ni tete na kwamba wakati huo alikuwa katika mkutano wa hadhara eneo la bonde hilo kujadili matukio hayo.
Mwanzoni mwa Machi mwaka huu, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwaagiza mawaziri watano kufika Bonde la Kiru na kuzungumza na wawekezaji pamoja na wananchi juu ya njia muafaka za kumaliza mgogoro wa mara kwa mara baina ya wakulima wadogo na wakubwa.
Mawaziri waliofika walikuwa wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk Mary Nagu, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk David Mathayo na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Aggrey Mwanry.
Mawaziri hao walifanya mkutano mkubwa wa hadhara uliojumuisha wananchi na wawekezaji na kisha kuwaagiza viongozi wa mkoa huo kuunda tume ya usuluhishi kabla ya Machi 23 mwaka huu. Hata hivyo, tume hiyo haijaundwa na mgogoro huo unaendelea kupamba moto.
Baadhi ya wakulima wadogo wa Vijiji vya Kiru Six, Imbiriri, Kiru Diki na Kimara, Kata ya Kiru wanataka wawekezaji hao waondoke na kuwaachia wenyeji maeneo yao