Nakuja na Hii ya Kufungua Mwaka.........Watanzania lazima tubadilike......Ukiangaliza 85% ya Forum nyingi humu ndani,ni mambo ya Siasa tuu......Siasa ni mchezo mchafu......
Katika Maandamano mengi ya Siasa,ulishawahi kuwaona watoto wa wakubwa nao wapo kwenye Maandamano?????
Mfano hai ni huu....Kipindi cha Machafuko Zanzibar....,,,,Maalimu Seif na Familia yake nzima,,walikimbilia Nchi za nje kwenda kula raha na kuwaacha ndugu zetu Wakichinjana kama kuku...
Arusha watu kadhaa walijeruhiwa na kufa huku Watoto wa Vigogo wakiwa ama makwao,au wanakula zao Maisha ...
Ushauri wangu ni huu..
1:Watanzania tukubali kwamba,wanasiasa kamwe,hawawezi kufanikisha maisha yetu na familia zao..
2:Wanasiasa ni watu wanafiki na hawafai kabisa kufuatwa....
3:Hupandikiza chuki kwa Jamii na hata kugawa Jamii na kusababisha Maafa Makubwa...
4:Watanzania Msipoteze muda wenu bure,kwa masilahi ya wanasiasa ,,huku familia zenu zikiwa zinataabika..
Mwenye akili timamu atakuwa amenielewa vizuri,,Ila mwenye akili finyu,atanipinga na kunikosoa sana...
Nawasilisha