Hali tete Masasi

Jikusanyeni muite Pipooz Power muingie barabarani kufanya maandamano ya amani kupinga manyanyaso haya ya jeshi la policcm.
 
Kuna taarifa za ndani kwamba wale viongozi na wanachama wa CDM waliokamatwa na kufikishwa mahakamani jana wamenyimwa dhamana. Wapo waliokaa mahabusu takribani wiki moja sasa. Eti wanashikiliwa kwa kosa la kula njama.

Mkuu Basil Lema kama sikosei wewe ni mmoja wa Makamanda wa ukweli toka Moshi na umezunguka sana ktk harakati za M4C, na kwa mamlaka uliyonayo mjulishe Dr.W.Slaa ikiwezekana Kesho ktk mkutano atoe tamko kuhusu hali hii, na tukubaliane ni hatua gani za kuchukua kukomesha unyanyasaji huu.

HUU NI MWAKA WA NGUVU YA UMMA sio mwaka wa kuendelea kulalamika tunaonewa bali ni wakati sasa wa kusema basi tumechoka kunyanyaswa.

Raia tunyanyaswe na Bungeni wabunge wetu wanyanyaswe, sasa nani mkombozi wetu?

"Msiogope, simameni tu mkauone wokovu wa BWANA atakaowafanyia leo…BWANA
atawapigania,nanyi mtanyamaza kimya"
(Kutoka14:13,14)
 
Unajua yanayokea Misri sasa ? so called peoples power nje ya kura ni uhaini tu... na dawa yake inapatikana baada ya mudamfupi...Misri is a good case study ... Tunis same..Syriaa same.
 

Mhalifu ni mhalifu tu, Ni lazima achukuliwe hatua hakuna cha kukiomba chama labda mtuaminishe kuwa mmetumwa na chama chenu.
kufanya uhalifu kwa kisingizio cha chama! Mtashughurikiwa tu hata na hao wanaowatuma.
 
Viongozi wa CDM hawajajulishwa na wamechukua uamuzi gani?
 
Tutegemee hali hiyo kusambaa nchi nzima kasoro Bagamoyo tuu.
 

wapi big show?tiririka
 
Kuna taarifa za ndani kwamba wale viongozi na wanachama wa CDM waliokamatwa na kufikishwa mahakamani jana wamenyimwa dhamana. Wapo waliokaa mahabusu takribani wiki moja sasa. Eti wanashikiliwa kwa kosa la kula njama.

kama alievamia kiwanja amenyimwa dhamana,itakua hao ambao wamechoma nyumba za waheshimiwa.
 
hivi CDM ni chama cha waasi na hakitambuliki na ofisi ya Tendwa? maana huu upuuzi uko hadi kwenye ajira za serikali. kama umeomba ajira serikalini, ukafanyiwa vetting na kubainika ni mwanachama wa CDM eti tayari ishakuwa dosari! stupid of them!
halafu hivi vyombo vya habari vina unafiki kweli. wanadai uhuru wa habari wakati wanafiki watupu. wakiitwa Ikulu na kula mapochopocho na kupewa bahasha za khaki basi wanaandika ama habari za kuiponda CDM au hawaandiki chochote kizuri juu ya CDM. anyway acha waendelee lakini wakumbuke licha ya serikali ya Tunisia kudhibiti vyombo vya habari lakini wananchi wa nchi hiyo walitumia mtandao wa ;Face Book' kutumiana habari na kuhamasishana kuuangusha utawala wa Rais fisadi! ... Time will tell...
 
Wacha uongo wako kusini huku hakuna Chadema,nyinyi mulitubagua zawani kwa ukabila wenu na udini wenu...huku kama Zanzibar vyama ni viwili tu....CCM na CUF
 
tupe uthibitisho wa tuhuma zako
 
Hatua za kuwinda mahasimu wa kisiasa kwenye operation kama hizi zitapelekea machafuko.Hakuna chama chochote cha siasa kinachoweza kukubali wanachama wake kunyanyaswa kwa sababu za kisiasa.
 
sasa sijui tuwasaidiaje jamani?kwani kabla hamjaanza harakati zenu hamkujua reaction itakuaje?au mlidhani watawakubalia madai yenu.
Mbona hayo yanaeleweka tangu enzi za Nyerere, kwamba ukiandamana kudai haki yako dhidi ya serikali, wewe ni adui mkubwa wa serikali. Kwani akini Ulimboka hawakujua wangepatwa na nini? Lakini hatutanyamazishwa na kuvaa mioyo ya uoga kwa kuwa tu wenye mamlaka wana uwezo wa kutumia dola kutunyamazisha. Ufike wakati, wenzetu wakikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya uongo, sisi tuandamane kupinga kukamatwa kwao. Tukifikia kwenye spirit ya aina hiyo, Udikteta wa Kikwete utafika mwisho kama si kupungua. Huyu bwana anaongoza nchi kimabavu kupita kawaida. Na hii haishangazi hasa kwa mtu asiye na hekima ya kuwashawishi watu ili wamsikilize.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…