Hali tete kwa CHADEMA kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015

Wanabodi.

Kuingia kwa Abdulrahaman Kinana na Philip Mangula katika timu ya uongozi wa CCM, kunasafisha kabisa matumaini ya Chadema kuingia Ikulu ifikapo mwaka 2015. Ni jambo lililo wazi Kinana, heshima aliyojijengea mkoani Arusha na mikoa mingine ya kaskazini, kila Mtanzania mkweli anajua.

Heshima aliyojijengea Mangula Iringa na mikoa mingine ya Nyanda za Juu Kusini, kila Mtanzania mkweli anajua. Kutokana na sababu hizo kiongozi au mwanasiasa yeyote makini ndani ya Chadema, atakubaliana na ukweli kwamba chama hicho sasa hakitakuwa na chake tena kanda ya kaskazini na nyanda za juu kusini mwaka 2015.

Chadema kama ina viongozi wanaona mbali wanaweza wakaanza kuitumia ruzuku wanaoipata sasa kwa umakini wa hali ya juu, ikiwa ni pamoja na ruzuku hiyo kutumika kujenga vitega uchumi vya baadae vya chama hicho baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, cha hicho hakitapata tena ruzuku. Hakuna kipindi kigumu ambacho Chadema itapitia kama kipindi hicho kwenye historia ya chama hicho.

Pamoja na kwamba hakuna kiongozi yeyote ndani ya Chadema anayeweza kwenda kinyume na amri ya Mbowe kuhusu matumizi ya ruzuku ya chama hicho, lakini mwelekeo wa sasa utakuwa tofauti, Chadema sasa wana hiyari ama kuacha hazina ya ruzuku yao kidogo kutoka serikalini inayopatikana sasa iendelee kuboresha maisha ya viongozi na familia zao, au waseme hapana, sasa tuanze kujenga ofisi za chama chetu kila mkoa na wilaya ili pindi ruzuku hiyo itakapopungua baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 walau chama kibakiwe na ofisi.

Mbowe na Dr Slaa sidhani kama watakubali wazo hilo lenye maana moja ya kupunguza maisha yao kifahari waliyonayo sasa hawatakubali kuona wanaachana na mipango yao ya kujiwekea hazina ya baadaye ya maisha ndani ya chama ambayo haitakuwa na ruzuku.

peleka huu utoto kwa watoto wenzio facebook!
 
Ni mapema mno kusema lolote kwa sasa. Tusubiri kipindi cha miezi sita aliyoiomba Mangula ndio tutaweza kufanya tathmini iwapo ni kweli CCM imeweza kufunguka au la.:target:
 
If u dont know the place you are going then no way can take you there! Ritz n ua nincompoops..... If Cdm r nat aware with what r they doin then what is bothering you old man? Its a wearer who know where the shoe pinches and u aint not! U better shut ua buccal cavity so as to hide the damn stinking!!
 
Ritz:Tukiachana na propaganda za kisiasa pamoja na yale mambo ya kupeana moyo ama ushabiki kwenye masuala ya kisiasa,katika hili ccm wanaweza kidogo wakawa wamejipatia Credit na JK anaweza akawa amechanga karata zake vizuri kwa sababu kama ni vuijembe kapigwa sana hadi na wanaccm wenyewe mara ameamua kuwaachia wapinzani nchi?!,mara CCM imemshinda lakini kumbe Usiomuona Kobe ameinama,anatunga sheria.

Ni ukweli usiopingika kwamba watendaji hawa wapya wa ccm wametoa mstuko kwa vyama vya upinzani na hasa cdm ambayo ilikuwa imeshakaa kwenye line kwa ajili ya kuhakikisha kwamba inachomoka mita 100 na kuindoa ccm madarakani,hakuna ubishi kwamba kwa hili lililofanyika ni lazima wakae chini wajipange upya na kuangalia waingilie mguu gani katika kama kweli wanan nia ya dhati katika kuhakikisha kwamba wanaichukua nchi.

Hata hivyo kwa ccm sio tu kwa sababu kinana na Mangula wapo basi wajisahahu waache kufanya kazi ka sababu majina ya watu hao ni makubwa,hakuna kitu kama hicho,ni lazima,ni lazima watumie nafasi hiyo na majembe hayo katiika kuhakikisha kwamba wanakisafisha chama kama ambavyo alisema mangula siku ile Dar!!!!!!!!!.

Ni ukweli usiopingika kwamba ndani ya ccm bado kuna mzizi ya uharibifu inayotakiwa kung'olewa ili imani ya wananchi na wanachama wake iliyokuwa imetoweka irejee.

Otherwise ni azi kwamba hali si shwari saana kama ilivyokuwa hapo awali kwa cdm kwa vyovyiote ni lazima wastac,wakae warudi nyuma wajipange.

Hawa sio wapya mbona mliwatoa? upya wao ni nini, hakuna jipya. Vinginevyo subirini nguvu ya umma.

Kinana ana kabiriwa na tuhuma nyingi, magogo yetu mengi yamesafirishwa nje na meli ya Kinana.
CCM mmekosa mtoto wa kuwaambia kwamba mfalme yuko uchi. Ni vicheko vitakavyowashitua.
 
Naona umejiunga juzi tu umeingia na Moto wa kuipigia Debe ccm.
Hongera zako

Nenda kwenye hoja mimi humu ndani sina chama hata wewe ukija na hoja ya mana nitakuunga mkono,mimi si kama wewe ambaye unashabikia hata mabovu madam yanahusu CHADEMA!!!!

Tatizo ni kwamba unapenda kusikia yale unayopenda kuyasikia,yale usiopenda kusikia ni tatizo kwako na lazima ulalamike na kuona unaonewa,acha hiyo tabia jifunze kusikia ama kuona hata yale usiyoyapenda.
 
..Inawezekanaje Mangula awe maarufu Mkoani kwao wakati huo huo alipata kura pungufu katika kura za uenyekiti? Kule kwao kulikuwa na tajiri mmoja alikuwa na magari yake yaliyoandikwa "FIKIRI KWANZA".
 
Ni maskini kabisa, tena mfu na kimeo wa fikra mgando!! Au wewe unasemaje!! amekutuma umfagilie ee!!! anakulipaje kutwa?!!!

Mi naona huna tofauti naye kama yuko hivyo unavyodhani basi naomba niamini kwamba wewe ni mwenzake~~~~~~~~~~~~~samahani niwie radhi.
 
Inabidi niheshimu mawazo yako, ina maana mafisadi wote wa ccm wataondoka baada ya kinana kuwa katibu mkuu? Unakumbuka list of shame kuna mafisadi papa kama rostam,kikwete na wengine je kinana ataweza? Ccm ni ileile leo, jana na daima. Ni chama kinacholinda wala rushwa, kinachoanzisha mfumo wa kulindana. Watanzania wapo tayari kwa mabadiliko na si kutawaliwa na janga la taifa ccm!
 
Wanabodi.

Kuingia kwa Abdulrahaman Kinana na Philip Mangula katika timu ya uongozi wa CCM, kunasafisha kabisa matumaini ya Chadema kuingia Ikulu ifikapo mwaka 2015. Ni jambo lililo wazi Kinana, heshima aliyojijengea mkoani Arusha na mikoa mingine ya kaskazini, kila Mtanzania mkweli anajua.

Heshima aliyojijengea Mangula Iringa na mikoa mingine ya Nyanda za Juu Kusini, kila Mtanzania mkweli anajua. Kutokana na sababu hizo kiongozi au mwanasiasa yeyote makini ndani ya Chadema, atakubaliana na ukweli kwamba chama hicho sasa hakitakuwa na chake tena kanda ya kaskazini na nyanda za juu kusini mwaka 2015.

Chadema kama ina viongozi wanaona mbali wanaweza wakaanza kuitumia ruzuku wanaoipata sasa kwa umakini wa hali ya juu, ikiwa ni pamoja na ruzuku hiyo kutumika kujenga vitega uchumi vya baadae vya chama hicho baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, cha hicho hakitapata tena ruzuku. Hakuna kipindi kigumu ambacho Chadema itapitia kama kipindi hicho kwenye historia ya chama hicho.

Pamoja na kwamba hakuna kiongozi yeyote ndani ya Chadema anayeweza kwenda kinyume na amri ya Mbowe kuhusu matumizi ya ruzuku ya chama hicho, lakini mwelekeo wa sasa utakuwa tofauti, Chadema sasa wana hiyari ama kuacha hazina ya ruzuku yao kidogo kutoka serikalini inayopatikana sasa iendelee kuboresha maisha ya viongozi na familia zao, au waseme hapana, sasa tuanze kujenga ofisi za chama chetu kila mkoa na wilaya ili pindi ruzuku hiyo itakapopungua baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 walau chama kibakiwe na ofisi.

Mbowe na Dr Slaa sidhani kama watakubali wazo hilo lenye maana moja ya kupunguza maisha yao kifahari waliyonayo sasa hawatakubali kuona wanaachana na mipango yao ya kujiwekea hazina ya baadaye ya maisha ndani ya chama ambayo haitakuwa na ruzuku.

Nafikiri ifikie wakati uweke nchi mbele (pamoja na wazalendo) alafu tumbo lifuate baadae.
 
Nilishasema na ninarudia tena,sijawahi kuona thread aliyoandika Ritz isitaje jina la Dr. slaa.
Mara nyingi ukiona mtu anamtaja mtu kila mara ujue anamkubali au anamuogopa.
Mimi sio Cdm wala CCm ila nimekuwa nasoma thread zako na nyingi uwa zinamtaja Slaa. Sasa bwana Ritz unamchukia au unamkubali moyoni ila machoni au mdomoni unashindwa kudhibitisha.
 
Kinana si lolote si chochote, kwa ujumla wananchi tumechoka na ccm, tunataka chama kingine kitawale nao tuwaone. si semi kwamba Chadema ndio watawale, na seme chama kingine kiingie madarakani kwani hata chadema nao sio wasafi sanaaaaaa, zito alikuwa kwenye kamati tanesco kafanya madudu tu na ndio chadema hao.
 
Inaonekana Ritz pandikizi la ccm. unataka kutuaminisha kwamba ccm sasa safi, umenoa. mafisadi yote ya nchi hii yamejificha ccm, wakwepa kodi wote wapo ccm.
 
Mulize kinana vp ile meli china na pembe za ndovu ameshauza...si msafi??

Hii ni fimbo safi ya kumchapia huyu bwana Kinana. Ajitokeze hadharani aseme vizuri. Rostam Aziz ana kampuni yake ya uwindaji haramu kwenye mbuga zetu. Nashawishika kusema kuwa huenda hii biashara ya pembe za ndovu ni biashara ya Rostam akishirikiana na mwenye meli bwana Kinana. Maana kupita ukaguzi wote huo mpaka kufika huko zilikokamatiwa lazima kuwe na uhusika wa watu wakubwa hapo.
 
Ritz heshima zipi hizo walizojijengea .wakati tunaona kila kukicha chama kinaboronga namna hii
wenyewe kwa wenyewe mnagombana mpaka kurushiana viti
 
Last edited by a moderator:
Tusubiri tuone hicho unachosema,hata akina Mkama walianza hivyo hivyo!.Wako kama mbwa koko wanaofoka tuu!.Hata wao akina Kinana sio waadilifu kiasi kwamba wanaubavu wakuwawajibisha wenzao walioko CCM.
 
ni ujinga tu, watu hawajaanza kazi tayari wanawaita tishio, msisahau hiki ni kizazi kipya ni vijana wachache sana wanamfahamu kinana na mambo yake, hata mimi katika umri huu wa zaidi ya miaka thelathini simkumbuki kinana kwa lolote la maana, ukija kwa mangula nadhani kilichosaidia kumjenga ni vyama vya upinzani kuwa na usingizi mzito baada ya mrema kuvurunda NCCR na hivyo wananchi kupoa kuhusiana na siasa za upinzani kipindi cha mkapa, lakini wote watatambulika sasa kama wana uwezo ama la watakapokutana na moto wa wananchi wanaolaumu ugumu wa maisha chini ya utawala huu wa CCM na imani mpya waliyoijenga na inayokuwa kila siku kwa Chadema.

Hivi si ni kinana huyuhuyu aliyekuwa kampeni meneja wa kikwete katika kipindi ambacho kura zake zimeshuka sana katika historia ya chama hicho? hivi kama Mangula ana nguvu sana Iringa ilikuwaje akadondoshwa na Jah People kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa mkoa wa iringa? nadhani ni upuuzi kuwahofia hawa watu kama ni kweli kuna watu wanaowahofu!
 
Kinana si lolote si chochote, kwa ujumla wananchi tumechoka na ccm, tunataka chama kingine kitawale nao tuwaone. si semi kwamba Chadema ndio watawale, na seme chama kingine kiingie madarakani kwani hata chadema nao sio wasafi sanaaaaaa, zito alikuwa kwenye kamati tanesco kafanya madudu tu na ndio chadema hao.
kuna nani zaidi ya hao wawili? Zitto amechemka vipi issue ya tanesco, au umekaririshwa tu!
 
Ritz nae huwa anatoka na vituko! sasa hapa tutachangia nini kuhusu thread uliyopost?
Nakushauri OMBA UZIMA,na endelea hivi hivi kuingiza siku ili payment list ya Nape usifutwe
 
Back
Top Bottom