Hali si swari mkutano wa CHADEMA kata ya Ndago (Singida); watu 2 wafariki

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,974
785
mods niko ndago msifute ni kweli.

wabunge wa chadema walifika saa
8.30 mchana huu lakini fujo na kuendelea kati ya mashabiki wa ccm na chadema watu wawili nimeona wamekufa na wengine kujeruhiwa kwa mawe. hali si shwari nitaleta taarifa zaidi baadaye natumia simu
KWENYE MKUTANO KUNA JOHN MNYIKA NA KITILA MKUMBO KIJANA ALIYEKUFA ANAITWA YOHANA MPINGA MIAKA 30 MKAZI WA KIJIJI CHA SONGAMBELE KATA YA NDAGO JIMBO LA IRAMBA MAGHARIBI LA MBUNGE MWIGULU NCHEMBA INADAIWA NI MFUASI WA CCM KAPIGWA KWA MAWE. WANA CDM TISA WAMEKAMATWA NA POLISI.

NAAMBIWA YULE WA PILI ALIKUWA BADO KUFA KAKIMBIZWA HOSPT.

CDM walipofika eneo la mkutano kabla ya utambulisho WAITARA akaanza kumtukana MWIGULU NCHEMBA kuwa ni malaya, fisadi na mwongo ndipo mtu mmoja wa ccm akasisimama kwa amani na kutaka wasitoe matusi bali waongee sera. ghafla mawe yakaanza kuporomoshwa na kutupwa ikawa vurugu hadi mauaji.


UPDATES..

Wakuu na Mods

Njia ya muongoni fupi sana. Wabunge wa CHADEMA wasiokuwa na majina wamefika Ndago saa 8.30 mchana?????!!!!!!

Wakuu, kuna Operesheni ndogo kwa Mkoa wa Singida yakiwa ni maandalizi ya operesheni kubwa kwa mikoa mitano, Singida, Iringa, Dodoma, Manyara na Morogoro, kama ilivyoazimiwa na Kamati Kuu mapema wiki hii.

Kazi hiyo iko chini ya timu inayoongozwa na Kamanda Mwita Mwikabwe Waitara, yeye ndiye mratibu wa ziara hii fupi na leo ilianzia katika Wilaya ya Iramba, Jimbo la Iramba Magharibi, ambapo mikutano ya hadhara imefanyika katika maeneo ya Ndago na Kinampanda.

Kulikuwa na taarifa tangu siku tatu zilizopita, timu ikiwa bado Dar es Salaam, kuwa kuna kikundi cha vijana wamekodiwa, wananunuliwa pombe, wakiandaliwa kufanya fujo ili mkutano huo usifanyike kisha ionekane CHADEMA wameshindwa kufanya mkutano kwa Mwigulu Nchemba. Bahati mbaya sana kitumbua chao kimeingia mchanga. Nafikiri hata huyu mleta maada ni sehemu ya hiyo propaganda.

Sasa wakati mkutano umefunguliwa tu, Kamanda Mwita akawa-preempty kwa kuwaambia kuwa taarifa hizo tayari zinajulikana na polisi wawe makini. Haa! Jamaa waka-panic. Walikuwa mbele kabisa pale. Wakaanza kurusha maneno, wanapiga makelele, wanazunguka zunguka pale mbele ya hadhara. Mbele ya polisi. No action.

Kelele za kundi lile, hazikuwa zikivumilika. Wananchi hawakukubali uvunjifu wa amani wa makusudi uliokuw aukifanywa mbele ya polisi. Yaani sinema ile ilikuwa Ilemela-type, kule ambako wabunge wa CHADEMA walivamiwa, kukatwa mapanga mbele ya polisi wenye silaha. Brothers, huwezi kuamini lile kundi likajitenga pembeni na kuanza kurusha mawe.

Wananchi wengi waliokuwa pale mkutanoni kwa mamia, hawakukubali ufidhuli ule. Wakawafukuzilia mbali wale wahuni. Mkutano ukaendelea kwa amani kabisa, kisha tukaelekea mkutano wa pili Kinampanda, ambako John Mnyika, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi na Mbunge wa Ubungo, amemaliza kupiga nondo kama alivyopiga Ndago.

Wananchi wamemskiliza John kwa makini, sasa kazi zinanunuliwa. Nondo zinawagusa wananchi wa Iramba Mashariki, yakiwa ni maandalizi ya Opereseheni kubwa inayokuja mikoa hii muda si mrefu.
 
Masikini Tanzania sijui inaelekea wapi tunaingia kwenye siasa za kuuwana sisi kwa sisi...inasikitisha sana.
 
mods niko ndago msifute ni kweli.

wabunge wa chadema walifika saa
8.30 mchana huu lakini fujo na kuendelea kati ya mashabiki wa ccm na chadema watu wawili nimeona wamekufa na wengine kujeruhiwa kwa mawe. hali si shwari nitaleta taarifa zaidi baadaye natumia simu

Mkuu chanzo ni nini mpaka imefikia hivyo watu kupoteza maisha?
 
Ngoja tusubirie kidogo from other sources, maana hii habari ya kuletwa na mama porojo, lazima uiwekee question mark nyingi tuu??????????
 
tumia hiyo hiyo simu unayo tumia kutupa chanzo cha vurugu.
 
Kama ni kweli, hivi mkutano ulikuwa wa chama gani? Harafu what really transpired? Yaani mkutano ilikuwa ya vyama viwili
 
Tunaomba taarifa zaidi sisi tulioko nje ya nchi tujue kinachoendelea,walikuwa ni wabumge gani hao.,hilo mbona ni jimbo la mwigulu wao walifuata nini huko.
 
Kwahiyo hao watu wa CCM wamelipwa kwenda kufanya fujo kwenye mkutano wa Chadema?!, mbona wanawafuatafuata na kuwachokonoa sana Chadema!
 
Watu wa singida huwa wapole na wastaarabu sana ukiona wanafikia hatua ya kumchapa mtu ujue wamechokozwa.mama porojo tupe taarifa kamili
 
Mbona husemi chanzo cha mauaji ni nini hasa?

Si amesema yuko huko, unataka source gani?
Kama ni kweli ni jambo la kusikitisha sana, kinachonishangaza, hao CCM wameingiaje kwenye Mkutano wa Chadema? Hata wewe Mama Porojo umejiingizaje kwenye Mkutano wa Chadema wakati unajulikana msimamo wako uko chama gani?
 
Back
Top Bottom