WanaJF,
Kwa siku ya nne (4) hostel za Mabibo hazijafanyiwa usafi na watoa huduma wa kampuni mojawapo iliyoingia mkataba na chuo kikuu cha Dar es Salaam kufanya hivyo.Taarifa zilizozagaa ni kwamba wafanyakazi hao (vibarua) wapo kwenye mgomo dhidi ya mwajiri wao wakiwa na madai mbalimbali mojawapo likiwa la kutokulipwa mshahara wao wa Januari hadi sasa. Sasa kutokana na hali hiyo hali ya corridor na vyoo ni mbaya sana. Kuanzia jana wanachuo walianza kujimobilize na kutaka waonane na uongozi wa chuo juu ya mstakabali wa afya zao.
Hii Taarifa ingependeza zaidi jukwaa la Habari Mchanganyiko, By the Way Poleni sana,inabidi Mchukue hatua Mapema Maana Viongozi wetu kwa sasa ni utamaduni Wao kua Kuwajibika ni mpaka Washinikizwe ,Suala la Afya si la Mzaha hata Kidogo.
Mhhh! Ni hatari maana wanalala wengi sana katika room moja approximately eight students angalau Block F. Mishahara yao nimidogo na pia wanafanya kazi ktk mazingira magumu xana. Wapeni mpunga wao japo ni kidogo warejee kazini.
Usomi wao utakuwa hauna maana wakishindwa kutatua tatizo hili japo kwa muda wakisubiri hatma yake. Wajikusanye dk 15 wafanye usafi, ni kitu kinawezekana mbona, si wana viongozi wao!!!?